Tanzania kuchoma tena vifaranga kutoka Kenya?

Tanzania kuchoma tena vifaranga kutoka Kenya?

Vifaranga kutoka nchini Kenya vyenye thamani ya Milioni 40 vimekamatwa na mamlaka ya serekali Tanzania bila ya kuwa na vibali halali. Kwa kujibu wa taarifa toka mamlaka husika Tanzania wamesema wataviteketezwa kwa mujibu wa sheria inavyotaka.

Japo vifaranga hivyo havijathibitika kuwa na magonjwa ila kwa kua vimeingia bila kibali vitachomwa moto.

Source; ITV
Duuuh, yaani huu ukatili wa namna hii mimi sijawahi kuuelewa, si wavirudishe Kenya tu?!
 
Huyu importer kweli kabisa hajui kwamba tulishateketeza vifaranga enzi za Magufuli?
Huyu nadhani hata magazeti ya udaku hasomi
 
Ng'ombe wa Kenya wakiingizwa tunapiga mnada tunakula nyama.
Kuku kwasababu hawawezi kuliwa tuna teketeza.
Kwani magonjwa wanaleta kuku tu ng'ombe hawaleti?
I am asking for a friend.
 
Huu ni ukatili dhidi ya wanyama na haukubaliki tuziepuke njia za yule wa mavumbini
 
Ng'ombe wa Kenya wakiingizwa tunapiga mnada tunakula nyama.
Kuku kwasababu hawawezi kuliwa tuna teketeza.
Kwani magonjwa wanaleta kuku tu ng'ombe hawaleti?
I am asking for a friend.
Utakula kifaranga?
 
Ndiyo kama sheria zao zinasema hivyo.
Sheria za kipumbavu zisizijali uhalisia??
Mbona ngombe waliokamatwa toka kenya Walitaifishwa hawakuchomwa?? Kwan hawamuweza kua na magonjwa??
 
Kama sheria inasema hivyo wavichome tu ili liwefundisho kwa hao wanaingiza vifaranga bila kibali.
Sawa kabisa. Ni uhujumu uchumi uliowazi. Kuna siku wataingiza nchini vifaranga wenye magonjwa na kuisababishia nchi mlipuko wa magonjwa yasiyoeleweka.
 
Watumie njia nyingine isiyo na maumivu, mfano watumie gas chambers kwa gesi ya sumu...
 
Back
Top Bottom