Kuna kazi kubwa mbele yetu, baadhi ya sheria ziangaliwe upya, unapoamua kuwateketeza wale kuku eti kwa sababu za kiafya ,je imekwishabainika kuwa wana madhara?
Sisi tunaposafiri kwenda nje ya nchi hao kuku tunaokula huko huwa tumesafiri nao?
Tusikimbilie kutoa uhai kama haijathibitika wana madhara kwa binadamu.
Kwa upande wa kodi kuna taratibu zake, TRA wana seize mzigo, ukilipia kodi pamoja na faini unakabidhiwa mzigo wako ili uendelee na shughuli zako.Ukishindwa kulipia wanatangaza mnada,mwenye kununua atanunua na maisha yataendelea.
Hilo la kuua viumbe hai, ningependekeza sheria hiyo iangaliwe upya ,kuua kiumbe hai bila hatia si sawa kabisa,kama hawana magonjwa wasiwe wanauawa.Aliye tunga sheria hiyo ni binaadamu kama sisi, hatujui yeye kilimsukuma nini hadi kutunga sheria ambayo ni ya kinyama,nafahamu lazima ni pendekezo la mtu mmoja ambaye ndio mwenye nguvu ,kwa hiyo wajumbe waliishia kusema sawaa ipitee, bila kutafakari kwa kina.
Mungu ibariki Tanzania.