Tanzania kuchoma tena vifaranga kutoka Kenya?

Tanzania kuchoma tena vifaranga kutoka Kenya?

Kama sheria inasema hivyo wavichome tu ili liwefundisho kwa hao wanaingiza vifaranga bila kibali.
Mnataka kumpoteza Mama kama mlivyofanya kwa mwendazake. Mnaanza kumpa sifa za kijinga
 
Vifaranga vinasambaza magonjwa kwa haraka sana mkuu. Ungekuwa umefanya biashara ya kufuga kuku ungejua ukweli huo. Nafikiri unajua ugonjwa wa mafua ya ndege.
Sasa kama vimeshasafirishwa toka kenya hadi uvikamatie Dar, kama vina magonjwa, utayakwepaje?? Sio busara kuvichoma moto, muhusika apigwe faini, na kusimamiwa kuvirudisha vilikotoka!! Au vipigwe chanjo zinazotakiwa wajue cha kufanya, tatizo liko kwenye maamuzi mabovu yaliyofanywa huwezi kuzuia kuingizwa kwa vifaranga nchini wakati uzalishaji wake nchini hautoshelezi, waulize wafugaji wanavyopata tabu sasa kupata hivyo vifaranga!! Na masharti kibao kuwa ni lazima ununue chakula toka kwa muuzaji huyo, huwezi kulinda wazalishaji wa ndani wakati hawana uwezo wa kutosheleza mahitaji!!?
 
Vifaranga hawana hatia, aadhibiwe mhusika, vifaranga wapimwe kujiridhisha kama wanafaa kuwepo nchini au warejeshwe walikotoka, kuna amri ya Mungu isemayo "usiue"
Usiue ili baadae uchinje ule ushibe.
 
Taarifa ya Habari ya ITV ya leo imeonesha mfanyabiasha wa Ukonga aliyeingiza vifaranga vyenye thamani ya milioni 40 kutoka Kenya bila kufuata utaratibu.

Hatua zinazotakiwa kuchukuliwa kulingana na sheria nikubinafsisha mali nakuteketeza vifaranga wote kwa mujibu wa sheria.

Je, kipi bora kumuita mfanyabiasha ukampiga faini pia akalipia gharama za kuhakiki usalama wa vifaranga( kwa afya ya binadamu) alafu umrudishie vifaranga? Au ukateketeza mtaji au fedha milioni 40?
Sheria ifate mkondo wake, hii mambo ya double standards katika kutoa adhabu haitakiwi.
Hata yeye alipokuwa anafanya hilo alijua kuwa anaweza kukamatwa mchezo ukaisha. Ila still alibeti na mkeka ushalost! Sheria zinavunjwa na watu wanaozijua kabisa ila tamaa ndio huponza watu. Afanyiwe anachostahili.

Haina tofauti sana na tunaobeti kwenye michezo kama mpira, basket n.k tunaelewa kama kuna kula na kuliwa so tunakuwaga Neutral.
 
Vifaranga kutoka nchini Kenya vyenye thamani ya Milioni 40 vimekamatwa na mamlaka ya serekali Tanzania bila ya kua na vibali halali.
Kwa kujibu wa taarifa toka mamlaka husika Tanzania wamesema wataviteketezwa kwa mujibu wa sheria inavyotaka. Japo vifaranga hivyo havijathibitika kua na magonjwa ila kwa kua vimeingia bila kibali vitachomwa moto.

Source ;ITV
Hichi kitendo cha kuchoma kimekaa kiukatili zaidi
 
Hakuna diplomasia ya biashara? Kama mtasikia tena kupiga kelele mahindi ya wakulima yakipigwa pini mpakani kuingia Kenya.
 
Kama vizima wavipige mnada kwa wafugaji. Tena wafanye fasta visije wafia. Huu ukatili wa kuchoma viumbe wanatoa wapi?
 
Vifaranga vinasambaza magonjwa kwa haraka sana mkuu. Ungekuwa umefanya biashara ya kufuga kuku ungejua ukweli huo. Nafikiri unajua ugonjwa wa mafua ya ndege.
Kha....
 
Back
Top Bottom