Tanzania kuendesha mnada wa vitalu vya uwindaji; wawindaji kuruhusiwa kuua Tembo, Simba na wanyama wengine wazee

Tanzania kuendesha mnada wa vitalu vya uwindaji; wawindaji kuruhusiwa kuua Tembo, Simba na wanyama wengine wazee

Tuko pamoja mkuu. Yaan sijui afisa wanyamapori anayelipwa laki tano akutane na milioni tano tumchape Simba kijana kweli anapingana na hilo? Ni suala la muda tu najua
Uwindaji umekuwepo tangu awamu ya nyerere kuna wakati tu wanafunga dirisha lakini baada ya muda tena wanafungua yani mwa kifupi hapa hakuna jipya ni utaratibu wa kawaida kabisa hata wakati wa magufuli wanyama wamewindwa na kuuliwa na trophies zinachukuliwa.
 
Professional hunters wanapopewa kibali cha kuwinda wanaambiwa kabisa aina ya mnyama watakaemuua na wanaambatana na wawindaji wa TANNAPA
Wewe Tanapa na Ncaa kazi zake kuu ni kuhifadhi wanyamapori tu for next generation na haifanyi ya uwindaji kabisa bali kuna Utalii wa macho na picha pia ni sehemu ya mafunzo na tafiti mbalimbali zihusuzo wanyamapori na mazingira yao.
Utalii wa kuwinda ufanyika kwenye Mapori ya Akiba (Game Reserves)mf;Maswa GR,Ikorongo GR, Muyowosi Kigosi GR, nk. Huko ndo utakuta vitalu ambavyo viko chini ya TAWA
 
Hela za misaada tumeshazimaliza tunapoelekea daah
 
Tanzania inakusudia kuendesha mnada wa vitalu vya uwindaji, ambapo wawindaji wataruhusiwa kuwaua Tembo, Simba na wanyama wengine wazee.

Mnada huo unakusudiwa kuzalisha TZS bilioni 69.6, na 25% ya fedha hizo zitaelekezwa kuzisaidia jamii zinazoishi jirani na vitalu hivyo.

View attachment 2160537
Hapo hapo mwananchi mmoja huko Kijijini aliekamatwa na nyama ya swala mmoja kwa ajili ya wanae kafungwa miaka 20!!
Nchi hii tunajitafutia laana ujue
 
Authenticity ya hii habari please...

Sababu ni stranger than fiction..., na hizo nyara zitakazopatikana baada ya kuua tembo anachukua nani ?

Nadhani hii habari ila walakini, hopefully ni upotoshaji
Bbc wameongea na mh. Ndumbaro anethibitisha.

*Ikumbukwe ni manyama wazee tu
 
Una utoto mwingi Sana,unajua Tzn ninua ngapi Kwa tembo na Simba? Mara ngapi unasikia tembo wanaharibu mashamba na nyumba za watu?

Kwa taarifa yako Tzn inaongoza kwa tembo wengi Dunia shida wewe ni kichwa maji.

Ilitakiwa serikali ianze kuua nyumbu kama wewe
Na wewe ni kichwa uji nani kakwambia kwamba wingi wa tembo ndiyo sababu ya kuvamia na kuharibu mazao au makazi ya watu? unajua ecosystem ya tembo ilivyo? Mbona Nyumbu hawajavamia mashamba kama issue ni wingi wa wanyama? Shirikisha kiwiliwili chako ubongo wako. USIJIBU KWA MIHEMUKO.
 
Hii nchi mkuu ina wajinga wengi kweli kweli.
Vitalu vya uwindaji vipo miaka yote sasa hapo kuna jipya gani
Vya kuja Tembo AKA endangered species
Bbc wameongea na mh. Ndumbaro anethibitisha.

*Ikumbukwe ni manyama wazee tu
Kwahio wakiwa wazee ndio wanawekwa pamoja ili waweze kuwauwa..., na ikitokewa bahati mbaya tukaua na wadogo tutafungana mahakamani au ndio collateral damage
 
Na wewe ni kichwa uji nani kakwambia kwamba wingi wa tembo ndiyo sababu ya kuvamia na kuharibu mazao au makazi ya watu? unajua ecosystem ya tembo ilivyo? Mbona Nyumbu hawajavamia mashamba kama issue ni wingi wa wanyama? Shirikisha kiwiliwili chako ubongo wako. USIJIBU KWA MIHEMUKO.
Nyumbu sio wanyama waharibifu,hao sio predators.

Kwa hiyo tuhamishe watu kipisha wanyama wanaoongezeka,acha ujinga.
 
Sikubaliani na suala la kuwahamisha wamasai kwenye maeneo yao. Lakini pia sioni maana ya kufuga simba na tembo wanaozaliana kwa wingi bila faida.
Simba na Tembo wanaelekea kuwa extinct, halafu we unasema nini sijui
 
Hivi vitalu vimetengwa maalumu kwa ajili ya kuendesha uwindaji kwa kulipia, na serikali inapata fedha kwa kupitia huu uwindaji kwenye vitalu
Ukishaanza kuwapiga risasi tembo na simba maana halisi ya asili inapotea, hao wanyama walitakiwa waachwe wafe kifo cha asili kama wanyama wengine wanavyokufa kiasili na still ngozi na pembe zingeuzwa tu na watalii wangeendelea kuwaona ili wajue tembo na simba wazee wanafananaje na fedha zingeingia serikalini kwa sababu serikali haigharamii matibabu, malazi wala chakula chao kwahiyo hakuna hasara kama wangeachwa, hoja ya kwamba wauliwe serikali ipate fedha sioni kama ina mashiko, ina maana kwingine kote kumeshindikana kupata mapato au kusimamia vema vyanzo vya mapato mengine kwenye migodi gesi nk
 
Back
Top Bottom