Tanzania kuna familia ambazo zinaishi kifalme bila Watanzania kuzifahamu au wamepiga kimya tu

Tanzania kuna familia ambazo zinaishi kifalme bila Watanzania kuzifahamu au wamepiga kimya tu

Unakuta kwenye familia moja baba ni Rais mstaafu, mama ni mbunge na mtoto ni mbunge na ni naibu waziri, hii familia inahitaji shamba kwa ajili ya kulima chochote au ni kuitegemea serikali tu?

Familia nyingine unakuta baba ni Rais mstaafu, Mtoto ni Rais na Watoto wengine wawili ni wabunge hii familia bila serikali inaweza kuishi?

Familia nyingine mama ni Rais , mtoto ni mbunge na mkwe ni mbunge na ni waziri.

Huu mfumo umekaa sawa au nimekuelewa tofauti?

Abdulla Ali Mwinyi: Ninagombea nafasi ya Naibu Spika, tuziache mamlaka husika zitimize taratibu kisha Wabunge wapige kura——Yale yale tunayoyasema​

Ukweli uliosema unatatizwa na Aina ya mifano yako Tu, bila shaka unaongozwa na hisia Fulani hasi Sana dhidi ya watu hao.....hayo mengine umetafuta Tu namna ya kuingilia. Imepangwa hivyo na Mola na itabaki hivyo Hadi atakapoamua mwenyewe lkn si Kwa sababu ya kuchukia Tu watu fulani. Poleni sana
 
Kuna wakati huwa namkubali sana J.K Nyerere jamaa alikua mzalendo wa kweli sana

1. Jaribu kumlinganisha Nyerere kwa mtazamo wa umuliki wa mali kwa kuwaangalia maraisi wengine wa Afrika katika kipindi chake, angalia maraisi hao walipokuwa madarakani na baada ya kustaafu

2. Nyerere alidiriki kufunga ubalozi wa Israili na kufuta mahusiano nao licha ya kuwa Nyerere alikua mkatoliki haswaaa, lakini alifanya hili kuonyesha kuchukizwa na uvamizi wa Israili katika ardhi ya Palestina

Na hili alilifanya licha ya msaada mkubwa tu wa ujenzi wa UDSM na MUHIMBILI HOSPITAL ya leo

3. Alikubali lawama za udini kwa Wazee wa Dar es Salaam lakini alisimamia misingi ya usawa kwa wote aliishia kutoa shukran za teuzi kwa nafasi mbalimabli za watoto wa waislamu walioshiriki katika kupigania uhuru wa Tanganyika na sio kuleta udini katika serikali kama walivyokuwa wakitaka wao

4. Jamaa alikua na uwezo mkubwa sana wa kuchomeka na kurithisha familia na watoto wake katika nafasi za meza kuu ya nchi lakini hakufanya hivyo na aliwaacha wapambane wenyewe kupitia demokrasia

Ukiachana na Hawa matapeli kama kina Kakobe, Lusekelo, Mwamposa n.k.

J.K Nyerere alikuwa nabii wa kweli Tanzania na unabii wake ulishatimia na wote tumeshuhudia kwa macho
Unauhakika?yaani MTU yupo madarakani Kwa Miaka 22 alafu familia yake ibaki kuwa masikini?kuna vitu bado hatujui nchi hii.
 
Unauhakika?yaani MTU yupo madarakani Kwa Miaka 22 alafu familia yake ibaki kuwa masikini?kuna vitu bado hatujui nchi hii.
Kwa ulimwengu huu wa kidigitali katika sayansi na technolojia tungekua tushaona au kujua mkuu familia ile hamna hata balozi aliewakilisha Burundi au Malawi

Kwa harakaharaka tu mfano Nyumba ya Kikwete pale Mikocheni Regent na Nyumba ya Mkapa pale seaview zote ni Nzuri kuliko ya Nyerere pale sasani sijui umenielewa

Pamoja na kuwa zote zimekarabatiwa kuendana na mazingira ya kisasa lakini utaiona ya Nyerere ni ya kawaida sana

Hivyo ni kwa vinavyoonekana kwa macho tu
 
Tatizo lenu huwa mnapigania masilahi ya wanasiasa wenu kuliko hata masilahi yenu, jitu mishipa inamtoka kwa Mbowe kupewa kesi na anataka atoke ila kuna ndugu yake alibambikiwa kesi na kahukumiwa yupo jela na hakutokwa mishipa ya shingo kama alivyokamatwa Mbowe.

Wanasiasa ni watu special sana ni tofauti na sisi wacha waishi maisha ya kifahari.
Wewe ndiyo umeguswa mpaka umechanganyikiwa,wewe hujui kila struggle ina starling Mandela alivyopiganiwa ni ndugu zake tu,waliomchangia nyererere kwenye kesi ni ndugu zake,struggle ya skua gang kutawala milele icon wao si mna wajuwa,ndugu kila struggle ina icon wake
 
ROBERT HERIEL aliwahi kusema hapa jeiefu kuwa..

Hata baba yako mleta uzi alikuwa n nafasi ya kufika hapo walipofika hao,,, na angepewa wanavyopewa...

So hizo ni rewards za jasho lao na sacrifices walizofanya kufika hapo walipo,, Life is not fair na halitakuja kuwa fair hata siku moja...

-mwisho wa kunukuu-

So Mkuu acha wivu.. Hao wanakula matunda ya juhudi zao.
 
Maji Hufuata mkondo
Kuna familia baba daktari. Mama daktari. Watoto madaktari na wajukuu madaktari na wanawaandaa vitukuu kuwa madaktari.. nao wafalme?

Familia ya wanasiasa akiwaandaa watoto wake kuwa wanasiasa kuna shida gani? Au kwa kuwa wao wanajulikana?
Sasa udaktar wa mil 2 una ufalme gani na wewe🤣
 
Mnaosema katiba mpya itaondoa hili suala ni wajinga watupu, wapumbavu na malofa. Bila kujuana hakuna kula hiyo keki ya taifa CCM wala upinzani. Hapo upinzani wanaofaidi ni ndugu au watu wa karibu wa vigogo wa upinzani. Kwa mfano Lema katoka kijiji kimoja na Mbowe na wana undugu. Zitto alishikwa mkono na marehemu Sita. Wale Covid19 karibu wote utakuta kama sio mke au hawara wa kiongozi basi ni ndugu. Mi naona kama huwezi kutafuta connections zako mwenyewe zikaja kuwabeba kizazi chako basi kubali tu hizo familia ndo ziko hivyo na wanapambana kutoachia nafasi.
 
Iko hivyo.

Walionacho wanapambana kukilinda na wasiokuwa nacho wanapambana wakipate.
 
Unakuta kwenye familia moja baba ni Rais mstaafu, mama ni mbunge na mtoto ni mbunge na ni naibu waziri, hii familia inahitaji shamba kwa ajili ya kulima chochote au ni kuitegemea serikali tu?

Familia nyingine unakuta baba ni Rais mstaafu, Mtoto ni Rais na Watoto wengine wawili ni wabunge hii familia bila serikali inaweza kuishi?

Familia nyingine mama ni Rais , mtoto ni mbunge na mkwe ni mbunge na ni waziri.

Huu mfumo umekaa sawa au nimekuelewa tofauti?
Utapewa kesi ya uhujum uchumi mkuu ohoo.. hutakiw kuhoji
 
Wewe ndiyo umeguswa mpaka umechanganyikiwa,wewe hujui kila struggle ina starling Mandela alivyopiganiwa ni ndugu zake tu,waliomchangia nyererere kwenye kesi ni ndugu zake,struggle ya skua gang kutawala milele icon wao si mna wajuwa,ndugu kila struggle ina icon wake
Sawa mkuu wacha tuendelee kupigania haki na masilahi ya wanasiasa.
 
Back
Top Bottom