Dr Matola PhD
JF-Expert Member
- Oct 18, 2010
- 60,050
- 104,466
Wanajukwaa Mimi binafsi ni mfuatiliaji mzuri wa mambo mengi tu, mpaka nimeleta Uzi huu nimejiridhisha kuna tatizo sehemu au kuna kitu sisi binadamu au niseme Watanzania kuna sehemu tumekosea, sitaki kuhusisha dini labda Mungu tu ndio tumuhusishe.
Katika utafiti wangu usiyo rasmi nimeshuhudia watu waliokosa connection na kujikuta na hali ngumu kiuchumi ndoa zao zimekuwa ndowano, labda nikajidanganya hawa tatizo ni pesa tushauriane kutafuta pesa, kumbe nilikuwa najidanganya mwenyewe.
Mimi Kwa nafasi yangu katika jamii najichanganya na watu wa hadhi zote, nimekuja kubaini kumbe hata matajiri, hapa namaanisha matajiri kweli siyo kumiliki gari na nyumba, wote wana matatizo makubwa kwenye ndoa zao, na cha kusikitisha tatizo siyo usaliti kwamba wanagongewa wake zao hapana, Bali maelewano hakuna ndani ya nyumba, je tatizo liko wapi? Wanaume tumekosea wapi kuwaelewa wanawake? Iweje asiye na pesa na kwenye mihela wote wana kilio kimoja?
Nimeandika hii thread Leo baada ya kukutana na mwanangu mmoja tumepotezana miaka kibao nilipomuuliza Shemeji anaendeleaje akanijibu tumeshamwagana, Sasa kuanza kujumlisha watu ninaowafahamu wengi wamemwagana na wapendwa wao Tena ukifuatlia hakuna kesi ya usaliti wa ndoa au Mke anagongwa nje nimepata taharuki kubwa sana, tatizo liko wapi? tumekosea wapi ili tunusuru hizi familia ambazo bado hazijasambaratika?
Mimi naamini kuna tatizo sehemu ila sijui tatizo liko wapi ingawa wanawake nawabebesha sehemu kubwa ya lawama katika hili.
Wananzengo, nini kifanyike kunusuru ndoa za kizazi hiki?
N:b, hapa sijahusisha boy friend na girl friends naongelea wana ndoa, tatizo liko wapi?