Tanzania Labour Law (Sheria ya Kazi Tanzania)

Nipo dar mkuu

Nipo dar mkuu

Cha kufanya hapo fanya ufuatiliaji kimaandishi (kwa barua) mkuu, andika barua ya ku-querry suala lako hilo, ielekeze barua kwenda PPF ambako ndio mfuko wako, kisha mwisho wa barua wacopy SSRA (social security regulatory authority), na mwajiri wako pia na Ofisi ya Idara ya Kazi (mkoa wa Dar es Salaam); (nakala uwapelekee hawa uliowacopy)
 
Ok thanks mkuu ngoja nilifanyie hilo kazi
 
Poa poa chief, usisahau kuambatanisha na evidence zako mfano nakala ya card yako ya PPF, nakala ya form uliyojaza kumwelekeza mwajiri kuwa sasa michango yako aanze kupeleka PPF, na vielelezo vinginevyo utakavyoona vinafaa kujustify issue yako mkuu.
 
Wengi hatujui hili na ndio maana tunafanya kazi ktk misingi ya uwoga sana hata haki zetu hatuzijui.
 
Tafuta mwanasheria ufungue kesi kwenye tume ya usuluhishi wa migogoro ya wafanyakazi,
 
Upo mkoa gani chief?
Mkuu asante kwa juhudi zako za kutuelimisha_Mungu akulipe.
Nina swali,
....unafanya kazi kampuni binafsi na kampuni inatoa mkataba wa mwaka mmoja mmoja,..say_umepewa mkataba wa March 2017 to April 2018...mkataba umesema in case mmoja wenu hataki kuendeleza basi one month notice na in case of redundancy ni 2 month notice.
.....Mwajiri anakuja kupa barua ya kusema hata renew mkataba Mwezi wa 5 ,2018...stating the reason kuwa wanafanya restructuring.
.....hapo kisheria imekaaje..?
 
...barua unapewa baada ya kufanya nao kazi kwa zaidi ya week,..say kwenye tar 9
 
Mkuu asante kwa juhudi zako za kutuelimisha_Mungu akulipe.
Nina swali,
....unafanya kazi kampuni binafsi na kampuni inatoa mkataba wa mwaka mmoja mmoja,..say_umepewa mkataba wa March 2017 to April 2018...mkataba umesema in case mmoja wenu hataki kuendeleza basi one month notice na in case of redundancy ni 2 month notice.
.....Mwajiri anakuja kupa barua ya kusema hata renew mkataba Mwezi wa 5 ,2018...stating the reason kuwa wanafanya restructuring.
.....hapo kisheria imekaaje..?

Kwa hiyo kwa maana nyingine mwajiri anataka kufanya upunguzaji wa wafanyakazi kutokana na mahitaji mapya ya uendeshaji (termination of employment based on grounds of operational requirements). Upunguzaji wa wafanyakazi kwa reason kama hii sio kosa kisheria ilimradi mwajiri afuate utaratibu uliowekwa na kanuni za sheria ktk zoezi hili.

Taratibu nnazosema hapa ni kama;

1. Kutoa taarifa mapema iwezekanavyo kuhusu kusudio lake la kupunguza wafanyakazi (nadhani kwenye mkataba wenu wa ajira kuna 'clause' itakuwa inazungumzia muda wa notisi kama mmojawapo kati ya mwajiri au mwajiri anataka kuterminate mkataba). Lakini kwa case hii isiwe notisi ya chini ya siku angalau 30. Lengo la kutoa taarifa ya kusudio hilo mapema ni ili kutoa nafasi kwa watakaoathirika na zoezi hilo wapate muda wa kuchambua na kuchukua hatua stahiki za kisheria (kama kuna ulazima), kwa mfano kuweka zuio mahakamani n.k

2. Kuainisha vigezo vitakavyotumika katika zoezi la upunguzwaji unaokusudiwa....kwamba je vitatumika vigezo gani ktk kuselect watakaopunguzwa; mfano ufanisi kazini, waliokaribia umri wa kustaafu, walioajiriwa hivi karibuni ndo waanze kupunguzwa (Last In First Out), au walioajiriwa zamani zaidi ndio waanze kupunguzwa (First In First Out), n.k

3. Kuainisha mafao watakayolipwa hao wanaotarajiwa kupunguzwa....hiyo notisi lazima iainishe mafao ya kila mmoja ili hao watakaoathirika na zoezi hilo waone kama kuna kitu ambacho ni stahiki yake hakijaingizwa ktk mfumo wa ulipwaji mafao husika basi waweze kufanya consultation na mwajiri mapema ili kuepusha usumbufu pindi tarehe yenyewe ya kupunguzwa kazini ikifika.

NB; Kama kuna chama cha wafanyakazi chenye wanachama hapo katika eneo la mwajiri, lazima kishirikishwe katika hatua zote za zoezi hili.

Kwa marejeo zaidi unaweza kuona kifungu cha 38 cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Namba 6 ya mwaka 2004; na pia kifungu cha 23 cha Kanuni za Sheria hii niliyoitaja Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini (Kanuni za Utendaji Bora) ama "The Code of Good Practice" za mwaka 2007.
 
deonova, Asante saaana mkuu,

Hakuna notice yoyote iliyotolewa ,..all over sudden siku kama 9 kupita baada ya mkataba wa mwaka wa mwazo kupita unapewa barua kuwa hakuna kurenew mkataba mwingine sababu ya restructuring.

.....Hapo ndipo ninapo uliza kisheria imekaaje.
Nb:mkataba ni from march 2017 to April 2018.
....unafanyakazi mpaka tarehe say,May 9,2018 na kuambiwa tunata kurestructure hivyo hakuna kazi.
....no prior notice no anything.
 
Mkuu deonova nimefanya kazi katika sekta binafsi zaidi ya miaka mitano na sijawahi pewa barua ya kuajiriwa wala nilikuwa sikatwi nssf .Leo nimeamua nataka kuacha kazi naambiwa niandike barua ya kuacha kazi wakati wao hawakuwahi kunipa barua ya kuniajiri. Je hapo sheria inasemaje naweza kataa kuandika barua au inanilazimu.

Asante
 
IGWE,

Mnaweza kwenda kufungua shauri Tume ya Usuluhishi na kuomba kuwekwa zuio wakati shauri lenu likiendelea kupatiwa ufumbuzi chief, mkoa wowote uliopo ulizia tu zilipo ofisi za Tume ya Usuluhishi na Uamuzi wa Migogoro ya Kikazi (yaani CMA) ili mfungue shauri hapo mkuu.
 
Mfano nimepewa mkataba wa mwaka mmoja na nikausaini, baaada ya kufanya kazi miezi mitano mwajili anatangaza kuwa kampuni imefilisika hivyo itafungwa mwezi wa sita (kwa barua), sheria inasemaje hapo kuhusu malipo ya mwajiliwa??
 
Wewe kweli umeiva katika tasnia hii hongera sana.

Back
Top Bottom