Tanzania na Equinor / Shell yasaini mradi wa thamani dola bilioni 30

Tanzania na Equinor / Shell yasaini mradi wa thamani dola bilioni 30

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869
11 Juni 2022
Dar es Salaam, Tanzania

Serikali ya Tanzania yasaini mradi wa thamani ya dola za Kimarekani 30 bilioni na mashirika makubwa ya Equinor la Norway na Shell la Uingereza kwa ajili ya ujenzi wa mitambo ya kuchakata gesi asilia yaani LNG (Liquified natural gas) ambao umeshuhudia na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan leo jumamosi tarehe 11 June 2022.

Mradi huo wa kuchakata gesi upo baharini katika kina kirefu mkoani Lindi wenye thamani ya shilingi za kitanzania trilioni 70 (dola za Kimarekani 30 bilioni).

Ujenzi wa mradi huu utatoa ajira ya wafanyakazi 7,000 katika kujenga miundombinu pia mtambo wa kuchakata na utachukua miaka 7 kukamilisha ujenzi wake.
Equinor started exploration drilling activities in Block 2 Offshore Tanzania in 2011. A total of 15 exploration wells have been drilled, resulting in nine discoveries with estimated volumes of more than 20 Tcf of gas in place...source : Tanzania
Mradi huu ni wa aina yake unaotaka ujuzi wa hali ya juu kuukamilisha hivyo utajumuisha wataalamu wa ndani na nje kuhakikisha unakamilika kwa wakati na unategemewa kubadilisha kabisa uchumi wa mkoa huu wa kusini mwa Tanzania pia uchumi wa wakaazi wa eneo hili la Tanzania.

RAIS SAMIA AFICHUA MRADI ULIVYOMSHINDA AKIWA MAKAMU WA RAIS - "MAMBO YALIKUA MENGI"

Rais Samia ameshuhudia utiaji saini makubaliano ya awali ya mkataba wa nchi hodhi (HGA) wa mradi wa kuchakata na kusindika gesi asilia.

DAR ES SALAAM, June 11, 2022

Tanzania signs gas project deal with Equinor and Shell​

- Tanzania's government, Norway's Equinor and Britain's Shell signed a framework agreement on Saturday that will bring them closer to starting construction of a $30 billion liquefied natural gas (LNG) project, live video from the event broadcast on state TV showed.
 
11 Juni 2022
Dar es Salaam, Tanzania

Serikali ya Tanzania yasaini mradi wa thamani ya dola za Kimarekani 30 bilioni na mashirika makubwa ya Equinor la Norway na Shell la Uingereza kwa ajili ya ujenzi wa mitambo ya kuchakata gesi asilia yaani LNG (Liquified natural gas) ambao umeshuhudia na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan leo jumamosi tarehe 11 June 2022.
Huu sasa ndio mradi wa kweli wa maendeleo ya kweli wenye impact ya kweli kwenye uchumi wa nchi yetu kwasababu mradi huu ni mradi wa FDI, doleri bilioni 30 sawa na Trillion 70 za madafu, zinaletea kutoka nje zinakuwa injected ndani ya nchi yetu!, hii sio kitu ndogo!.

Japo bado hatujajua contents za huo mkataba, but definitely ule wasiwasi wangu kuhusu Gesi asili: Is it "day light robbery?" Watanzania tunaibiwa mchana kweupe! unakwenda kutokea!. Kuna kitu nilikisema hapo kuwa Tanzania tusipokuwa makini, kinakwenda kutokea, kwa ya juu juu niliyo sikia, nilichohofia kisitokee, ndicho kinakwenda kutokea!.

All and all, tumefika mahali lazima tukubali matokeo...

Pia Waziri wa Nishati, Mhe January Makamba, hili amelizungumza vizuri hapa

P
 
Serikali ya Tanzania yasaini mradi wa thamani ya dola za Kimarekani 30 bilioni na mashirika makubwa ya Equinor la Norway na Shell la Uingereza kwa ajili ya ujenzi wa mitambo ya kuchakata gesi asilia yaani LNG (Liquified natural gas) ambao umeshuhudia na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan leo jumamosi tarehe 11 June 2022. Mradi huo wa kuchakata gesi upo baharini katika kina kirefu mkoani Lindi wenye thamani ya shilingi za kitanzania trilioni 70 (dola za Kimarekani 30 bilioni)
Yule checkbob aliyetuingiza chaka asijekuwa amefanya yake tena mwisho wa siku anakuja kumnawia lawama huyu mama
 
11 Juni 2022
Dar es Salaam, Tanzania

Serikali ya Tanzania yasaini mradi wa thamani ya dola za Kimarekani 30 bilioni na mashirika makubwa ya Equinor la Norway na Shell la Uingereza kwa ajili ya ujenzi wa mitambo ya kuchakata gesi asilia yaani LNG (Liquified natural gas) ambao umeshuhudia na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan leo jumamosi tarehe 11 June 2022.

Mradi huo wa kuchakata gesi upo baharini katika kina kirefu mkoani Lindi wenye thamani ya shilingi za kitanzania trilioni 70 (dola za Kimarekani 30 bilioni).

Ujenzi wa mradi huu utatoa ajira ya wafanyakazi 7,000 na utachukua miaka 7 kukamilisha ujenzi wake.

RAIS SAMIA AFICHUA MRADI ULIVYOMSHINDA AKIWA MAKAMU WA RAIS - "MAMBO YALIKUA MENGI"

Rais Samia ameshuhudia utiaji saini makubaliano ya awali ya mkataba wa nchi hodhi (HGA) wa mradi wa kuchakata na kusindika gesi asilia.

DAR ES SALAAM, June 11, 2022

Tanzania signs gas project deal with Equinor and Shell​

- Tanzania's government, Norway's Equinor and Britain's Shell signed a framework agreement on Saturday that will bring them closer to starting construction of a $30 billion liquefied natural gas (LNG) project, live video from the event broadcast on state TV showed.
Mungu wabariki Wazungu
 
Attachments

  • Screenshot_20220612-021034_Samsung Internet.jpg
    Screenshot_20220612-021034_Samsung Internet.jpg
    110.2 KB · Views: 8
Mradi mzuri..ila uliopo unawasaidia vipi watanganyika?

Pia kuhusu kubadilisha mikoa ya kusini tutadanganyana tu kwa hilo..mana nani asiyejua mikoa yakusina licha ya utajiri huo wa gasi na korosho imebaki kuwa shamba la bibi.

Pia huo mkataba uwekwe wazi watanzania tuuone acheni mikataba ya siri...kwani mnaficha nini?

#MaendeleoHayanaChama
 
Uwekwe wazi kivipi
 
Umemlipa mshauri mwelekezi $2 million, halafu kama mtaalamu anaacha kukwambia aspects muhimu za upande wako kwenye kutengeneza framework ya HGA unayoenda ku sign; yeye amejikita katika masuala ya kugawana faida na kutatua mizozo. Issues zenye faida kwa mwekezaji.

Anaacha issue ambazo kwenye mradi mambo yakienda ndivyo sivyo mwekezaji inabidi agharamie kama; mazingira, au kufadhili miradi ya jamii husika. Hayo majukumu unajipa wewe kuyasimamia badala ya kuwa sehemu ya mkataba.

Halafu unajisifu, hiyo HGA as yet ni kwa manufaa yao sio ya jamii inayoizunguka wala kulinda mazingira. Na hakuna sector inayochafua mazingira kama oil and gas.

Crude ya baharini inakuja na maji ambayo inabidi yachujwe; unayapeleka wapi mziki wake sio mdogo na ndio kigezo kikubwa cha kuharibu biodiversity udhani kama hilo swala linahitaji kuwa kwenye mkataba na kuwapa wao hizo liability na wala mshauri uliomlipa akwambii umuhimu wake; bomba likipasuka pia kuna uchafuzi mwingine utaki kumpa mwekezaji gharama hizo kwa hela zake.

Only god intervention will save this continent.
 
Nakuunga mkono Mkuu Pascal Mayalla kuwa huu ndiyo mradi bomba, kuliko yote tuliowahi kuisaini, tokea nchi yetu ipate uhuru...........

Kwani mradi wa Trillion 70, siyo wa kitoto hata kidogo😄
Asilimia kubwa ya hizo hela ni za kununulia mitambo na vifaa vingine kutoa nje ya nchi; ni hela ndogo sana ndio itakayo inject uchumi wa Tanzania katika hizo trillion 70.

Sasa how do you justify that cost, yet ndio kitu cha kwanza kukatwa katika mapato. Wakati wanaofaidi ni mabank yao waliokopesha na viwanda vyao vinavyotengeneza mitambo. Wewe unapata masalia ya building costs tu.

Ujinga mnao sifia saa zingine, badala ya kuuliza hela inatoka wapi na interest ya mkopo au kupewa breakdown cost ya hiyo LNG plant if it’s justifiable mnashabikia ujinga msiouelewa.

People are overpricing the project nyie hooray wakati asilimia ndogo sana ya hiyo hela ndio inakuwa injected kwenye uchumi wa Tanzania.
 
Largest LNG capacity plant ni ‘Sabine Pass’ iliyopo Louisiana US, in uwezo wa kuzalisha 55.4 million metric tons per day na gharama ya ujenzi ni $5.6 billion.

Inayofuata ni ‘Ras Laffa’ Qatar inazalisha 41.1 million metric tons in a day; na gharama za ujenzi ni $2.3 billion.

Hiyo plant ya Mtawara inatarajiwa kuwa na capacity ya kuzalisha million metric tons kiasi gani kwa siku at peak level.

Ndio kuna gharama zingine kubwa za kutandaza bomba na probably kujenga offshore rigs kama tatu (then rigs sio lazima kwa technology ya leo) ndio gharama za mradi zinafika $30 billion kweli.

Kabla ya kushabikia haya mambo embu tujifunze nini tunachogawa. Hiyo $30 billion wanayotoa tunawalipa kwanza na interest ya mkopo; jumlisha mwekezaji ana share ya faida baada kuchukua hela za investment; is the cost justifiable.

It’s not as simple as you think; kushabikia huu upuuzi bila ya kuelewa what exactly you are getting yourself into.
 
Umemlipa mshauri $2 million, kama mtaalamu anaacha kukwambia aspects muhimu za upande wako kwenye kutengeneza framework ya HGA unayoenda ku sign; yeye amejikita katika masuala ya kugawana faida na kutatua mizozo.
Tena mshauri mwenyewe wa huko huko yatokako makampuni.

Hapa ilitakiwa apatikane mshauri wa kiChina, ndipo mambo yangenoga zaidi!
 
Asilimia kubwa ya hizo hela ni za kununulia mitambo na vifaa vingine kutoa nje ya nchi; ni hela ndogo sana ndio itakayo inject uchumi wa Tanzania katika hizo trillion 70.

Sasa how do you justify that cost, yet ndio kitu cha kwanza kukatwa katika mapato. Wakati wanaofaidi ni mabank yao waliokopesha na viwanda vyao vinavyotengeneza mitambo. Wewe unapata masalia ya building costs tu.

Ujinga mnao sifia saa zingine, badala ya kuuliza hela inatoka wapi na interest ya mkopo au kupewa breakdown cost ya hiyo LNG plant if it’s justifiable mnashabikia ujinga msiouelewa.

People are cooking figures nyie hooray wakati asilimia ndogo sana ya hiyo hela ndio inakuwa injected kwenye uchumi wa Tanzania.
EeeeenHeeeee, Kilatha Bhwanah!

Acacia alikuwa hapa mkuu, na wala hatukujifunza kitu chochote!

Miaka 60 na usheee, bado kila jambo tunaliona kama 'rocket science'; wakati baadhi ya wenzetu, kama India na Pakistan umri wa miaka 30 tu waliweza kutengeneza vitu, kama mabomu la nuklia; hata kama ingekuwa ni kazi ya kugezea kwa wengine tu, kwani sisi tunakatazwa kugezea au kuiba teknologia?

Nchi yetu hii inayo matatizo makubwa sana, kwa sababu hatuna malengo.
Watu wenye taaluma mbalimbali wamesomeshwa hata huko kwenye gesi wapo, lakini malengo yao makubwa ni kuwa ndani ya CCM ili wateuliwe kuwa maDC, n.k., badala ya kutumia utaalam wao kuliinua taifa letu.

Inauma sana na inakatisha tamaa kwelikweli.
 
Kabisa ila kwa miaka yote mpaka sasa kama nchi TPDC ilitakiwa kuwa na negotiators wenye walau basic knowledge.

Hawa watu ni kaput
EnHeee, nimeliandika hili sasa hivi hapo juu.
Ni kama laana inatuandama vile.
Kwa jinsi hii tunayokwenda nayo, sijui kama kutatokea wakati nasi tukawa watu wa kusema tuna uwezo wa kutengeneza chochote!
 
EeeeenHeeeee, Kilatha Bhwanah!

Acacia alikuwa hapa mkuu, na wala hatukujifunza kitu chochote...
ACCACIA wana anafadhali kulikuwa na mwekezaji Mbeya nadhani, alipomaliza kilichopo ardhini akatimuka na kuacha PPE assets; halafu tukaanza kumtafuta eti aje kuchukua vifaa vyake.

Baada ya miaka kadhaa ya kuto onekana serikali ikataifa ivyo vifaa. Sasa unajiuliza hivi hawa watu wanaelewa ya kuwa hizo investment alikuwa anazifidia kwenye mapato na kwa kufanya ivyo hizo mali zinakuwa za serikali ya Tanzania.

In other words beberu alituhurumia angetaka mali ambazo keshajilipa angetuuzia tena.

Sasa sidhani kama wamejifunza hiyo plant ya LNG na supporting infrastructure ni mali ya Tanzania mara tu mwekezaji akishachukua hela aliyowekeza.
 
Back
Top Bottom