Tanzania na Vifurushi vipya vya Data na Sauti (Aprili 2021) - Mwitikio wa wananchi

Waziri ametuingiza mkenge mbaya.
 
Vodacom naamini wanapata sana faida huko kuliko hata walikotoka maana huko ujambazi wote wa makampuni haupingwi kabisa wakati SA unapata 2gb kwa kama 4500 tsh rand 30 maeneo mengine mpaka rand 20 na 25 rand vifurushi vya mwezi sijui Nani anabaliki huo ujambazi kwetu kampuni ya serikali hao Telcom ndio kabisaa wana gb za kumwaga harafu bei reasonable Ttcl ilikua kipindi cha kupata hela nao wamekua na bei za kibeberu unategemea nini...
 
Hawajui kuwa kupunguza gharama za vifurushi kunachochea kukua kwa uchumi biashara nyingi zitafanyika mtandaoni bila kujali ukubwa wa faili hiyo multiplier effect wao wanataka faida moja kwa moja na hao tcra watoke kwenye mfumo wa kupeleka gawio la kuvunja record wanawanyonya wananchi wao wapo kwa ajili ya kusimamia huduma za mawasiliano wakiweka faida mbele wanaiua Tanzania kwenda na kasi ya maendeleo ya Dunia bila kujua sijui wanakua na matatizo gani mama angefumua huko kuna uozo sana..
 
Kweli mkuu wanamwaga ugali nasi tunamwaga mboga inakua ngoma droo nimegundua maisha bila mtandao inawezekana. Sms. Zinatosha.
 
Acha kutumia simu Sanaa hizi kero itaisha mm nimehamia sehemu isiyo na network ya internet
Tumejipanga mwaka huuu,mwaka huuu tutaisoma namba
 
Yani huyu amezingua..sasa mkongo wa Trillion 1.5 za kiTanzania una manufaa gani kwetu kama tuna bei za data sawasawa na landlocked countries?
 
Wanyonge wamefurahia sana bei mpya za bandoo uliliipigania Sana suala hiloo hakika wewe ni mkombozi Wa wanyonge,utaacha bongee la legacy
 
Tigo washenzi sanaaaaaaaa.....

Voda ndo weziii wa ajabu
 
Nachukua fursa hii kwa mabadiliko ya gharama za vifurushi vya Internet yaliyofanywa kuanzia hivi leo tarehe 02)04/2021 Kama alivyokuwa ameagiza Dr. Faustine Ndugulile, Waziri wa teknolojia.

Kutokana na kupanda kwa Bei za vifurushi, Nina imani umaarufu wa watu mitandaoni utapungua sana.
Pia wale waliokuwa wakisaka umbeya na ubuyu Instagram watapungua mno.
Status viwers kule WhatsApp itabidi wawe wanachagua status za kuangalia.

Kwa upande mwingine ongezeko hili litaathiri sana biashara za mtandaoni. Nadhani Ndugulile hakuangalia vyema upande huu.

Nawashauri mawaziri waachane na mawazo ya ngwe iliyopita, kufanya kazi kwa hofu na kumfurahisha mtu mmoja huku mkiumiza watu zaidi ya milioni hamsini.

Tumpe Rais wetu Samia Suluhu Hassan ushirikina kwa vitendo na si kwa maneno matupu. Kwa muda mrefu Tanzania imekuwa ikitajwa kwenye orodha ya mataifa yenye huzuni zaidi duniani, sasa tunataka watu wetu wawe na furaha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…