Tanzania na Vifurushi vipya vya Data na Sauti (Aprili 2021) - Mwitikio wa wananchi

Tanzania na Vifurushi vipya vya Data na Sauti (Aprili 2021) - Mwitikio wa wananchi

Hongera zake ndugu yetu huyu. Holotel ukiweka vocha unaliwa sh 100, Mega bando ilikuwa Gb1 kwa sh 1000 kwa wiki, leo ni Mb 400 kwa sh 1000 kwa wiki. Hongera sana
 
Nimeangalia vifurushi vya voda kwa kauli moja nikakubali nahama moja kwa moja. Nikataka niwakope MPAWA ili niwaachie vumbi wasenzi wameniongezea masharti siruhusiwi leo eti.
 
Neno sahihi Ni
"Stupidity"
Mwovu huwaza uovu na hutenda uovu.
Hivi sijui Ndugulile anaona fahari gani watanzania wakiteseka. Hajui kwamba Kuna Dada poa, mama ntilie, madalali, ma MC n.k wanatangaxia biashara zao kwenye mtandao?
Tatizo la viongozi wetu dhamila zao siyo kuwasidia wananchi wanao waongoza bali ni kutetea uhai wa chama chao.
 
Tatizo leno mmekariri vibando vya buku mbili sijui buku jero.

Jiunge na bundle la mwezi 30k linatosha kabisa.

Kauli yako ya Kifedhuli na Kidharau kama hii ndiyo ilisababisha hata kule nchini Ufaransa mwaka 1789 kukawa na French Revolution ( Mapinduzi ya Ufaransa ) baada ya Mke wa Mfalme Louis XVI aitwae Malkia Marie Antoinette kusimama katika Balcony na Kuwaambia Waandamanaji waliokuwa wakilakamika Bei ya Mkate kuwa juu na Yeye akawaambia Wanunue Keki wale.

Hivi Bei ya Mkate na Keki ni sawa? Na Wewe unavyowakejeli hapa wanaonunua Bando za Buku Buku na kuwataka Wanunue za Tsh 30,000/= hii siyo Dharau iliyovuka Kiwango?

Usisahau huyo huyo aliyekupa Wewe huo Utajiri ndiyo huyo huyo pia amewapa wengine Umasikini. Sikutegemea Member kama Wewe kuwa na Kejeli hivi kama alizokuwa nazo Malkia Marie Antoinette wa Ufaransa.

Mpaka nimesema hivi jua umekera sana.
 
Wamefanya ujinga Sana stupidness aisee
Stupidness kabisa
Ujinga mkubwa ujinga mkubwa Sana
Kivipi Mkuu?

Huenda wameona mawasiliano sio basic need!

Hivyo wanataka kubadili tabia, kutoka ktk kutumia rasimali zetu katika masuala yasiyo ya msingi.
 
Mimi ninavyojua offer hutolewa kwa wateja kama motisha. Maana wanakuwa wamekuchangia na umepata faida

Kulikuwa na ofa ya kwako tu au zile za kikanda ambazo mtu uliweza kupata Mb 500, na hamsini. Sasa wamefuta. Ina maana walitoa ofa sababu waliibia wateja?
Kama mazingira yako yanaruhusu karibu ttcl walau bei fair kidogo
 
Back
Top Bottom