Tanzania na Vifurushi vipya vya Data na Sauti (Aprili 2021) - Mwitikio wa wananchi

Tanzania na Vifurushi vipya vya Data na Sauti (Aprili 2021) - Mwitikio wa wananchi

Kiukweli yule jamaa anayejiita Kigogo2014 anasababisha hata wasiohusika kusomeshwa namba,halafu cha ajabu haijulikani hiyo bifu yake na hayatti Magufuli itakwisha lini,mimi nilitegemea angenyamaza baada ya mzee kufa ila ndo kwanza kama amepata starter

Ila serikali iangalie namna ya kuwaregezea baadhi ya tovuti bei za vifurushi mfano tovuti za .org na sio kutoa corporal punshment
 
Weka halo pesa 3000 nunua GB3 dakika 30 na sms ngapi sijui, Halotel wana afadhari,achana na Vodacom hawafai hata kidogo
Unakipatia wapi .... Na hii ndio afadhali kidogo kwa halotel
Screenshot_20210401-044439.png
 
Hii ndio ilikuwa sera ya Magufuli katik akuhakikisha mitandao ya kijamii watu washindwe kuitumia, maana alishasema anatamani malaika washuke wafungie mitandao.
Eeeh hiyo avatar yako sasa
 
Leo tar 1/4/2021 makampuni ya simu yamefanya mabadiliko makubwa katika vifurushi vyao.

Wamepunguza vifurushi kwa kias kikubwa hasa vifurushi vya data, sitaweka hapa kifurushi kimoja baada ya kingine lkn kwenye mitandao yetu hilo lipo.

Nenda kwenye menu tu nadhani utakutana na upuuz wote

Nini nataka kusema?
Wakati dunia inakimbia kwa kasi kwenye technolojia sisi tunajirudisha nyuma tena kwa kasi kubwa na wala hapa siyalaumu haya makampun ya simu kwani yenyewe yanapokea tu order toka serikalini.

Kama wananchi wa kawaida kabisa tunaiomba serk iweze badilisha hiv vifurush haraka sn mana wanachokifanya ni kurudisha juhud za maendeleo ya kisayans nyuma.

Na kwa vile tuna serikali mpya nina hakika watashughulikia hili haraka sana na wala hawatasubiri hadi mwezi upite mana kilichofanyika ni zaid ya upuuz wa hali ya juu.

Kama serikali itashindwa rekebisha hili bas tutajua hamna mpango na wananch wa kawaida na mengi mnayoyaongea ni porojo tu

Naomba kuwasilisha
Haya bwana
 
Leo tarehe 1/4/2021 makampuni ya simu yamefanya mabadiliko makubwa katika vifurushi vyao.

Wamepunguza vifurushi kwa kiasi kikubwa hasa vifurushi vya data, sitaweka hapa kifurushi kimoja baada ya kingine lkn kwenye mitandao yetu hilo lipo.

Nenda kwenye menu tu nadhani utakutana na upuuzi wote

Nini nataka kusema?
Wakati dunia inakimbia kwa kasi kwenye technolojia sisi tunajirudisha nyuma tena kwa kasi kubwa na wala hapa siyalaumu haya makampuni ya simu kwani yenyewe yanapokea tu order toka Serikalini.

Kama wananchi wa kawaida kabisa tunaiomba Serikali iweze badilisha hiv vifurushi haraka sana maana wanachokifanya ni kurudisha juhudi za maendeleo ya kisayansi nyuma.

Na kwa vile tuna Serikali mpya nina hakika watashughulikia hili haraka sana na wala hawatasubiri hadi mwezi upite maana kilichofanyika ni zaidi ya upuuzi wa hali ya juu.

Kama Serikali itashindwa rekebisha hili basi tutajua hamna mpango na wananchi wa kawaida na mengi mnayoyaongea ni porojo tu

Naomba kuwasilisha.
Mitandao gani hiyo?? Mbona mtandao wangu bado upo gado?
 
Wadau ni vyema tukapeana mbinu kipindi hiki cha mb kiduchu jinsi ya kuzi-handle
Mimi naanza na instagram.ili kutumia data kidogo ni vyema ukaingia instagram through browser mfano chrome (mf.www.instagram.com),utatumia data kidogo na video unaweza ukaamua kuiplay ukitaka usipotaka unaacha tu kuliko app yenyewe ya instagram video zinaplay automatic na ndo zinazomaliza mbs.
 
Zantel walikuwa wanafanya vizur sana lakini baada ya tiGO kuungana nao naona wameshusha sana vifurushi...1500 mb 550???
 
Mmezidi kuisema sana hasa kupitia mitandao ndiyo maana stone alikuja na hili wazo
Kuna watoto na watu waIma wanapata maarifa tele kupitia online classes na lessons ,
Internet ni uwanja mpana sana
 
Wapuuzi wameununua mtandao wa Zanzibar Telecoms washafanya vituko vyao tayari. Zantel sio mtandao rafiki tena sababu wadhulumati Tigo washauingilia.
Hata mimi nmeshangaa sana jana nmeona vifurushi vimebadilika sana...nimejuta kujiunga nao.1500 dk 30 na 550 mb????
 
Back
Top Bottom