Tanzania tuachane mfumo wa kupandishia watu mishahara bila kuwa na vigezo vya utendaji (performance)

Tanzania tuachane kabisa na mfumo wa kuwapandishia watu mishahara au vyeo bila kuwa na vigezo na vipimo vya "performance" zao.

Nashauri kwanza viwekwe vigezo na vipimo vya "performance" kazini ndivyo vitumike kuwapandisha watu vyeo na mishahara.

Ni wepesi sana kupanga vigezo vya ubora wa utendaji kwa kila kazi katika kila sehemu ya kazi. Tena siku hizi kila kitu kinakuwa kwenye data base kidigitali ni wepesi sana. Wale watendaji bora (best performers) watapanda mishahara na vyeo haraka na wale wazembe (kama ilivyo kwa Watanzania wengi) watasota hapo hapo na mshahara wa "entry level" mpaka wabadilike au wajiachishe wenyewe kazi.

Mfumo huu wa "performance based" upo na unatumika sana ulimwenguni, hususan kwenye kazi zisizo za Serikali, pia serikali nyingi zimeanza kutumia mfumo huo, bila kuoneana aibu wala huruma za kijinga.

Uzoefu wangu wa kufanya kazi za kuajiriwa kwa muda mrefu sana katika nchi zilizoendelea umenifundisha hayo.

I totally agree. Hii itaongeza ufanisi na uwajibikaji.
 
Hizo peanuts mnazolipa watumishi ndo muwapimie performance, lipeni kwanza mishahara inayoeleweka ndo mlete ishu ya performance....
Kwani wanafuatwa majumbani kwao ili wapewe kazi? Zi wanaziomba wenyewe? Si wanaomba wao tena kwa kuzigombania? Wakubaliane na masharti ya KPI
 
Tanzania tuachane kabisa na mfumo wa kuwapandishia watu mishahara au vyeo bila kuwa na vigezo na vipimo vya "performance" zao.

Nashauri kwanza viwekwe vigezo na vipimo vya "performance" kazini ndivyo vitumike kuwapandisha watu vyeo na mishahara.

Ni wepesi sana kupanga vigezo vya ubora wa utendaji kwa kila kazi katika kila sehemu ya kazi. Tena siku hizi kila kitu kinakuwa kwenye data base kidigitali ni wepesi sana. Wale watendaji bora (best performers) watapanda mishahara na vyeo haraka na wale wazembe (kama ilivyo kwa Watanzania wengi) watasota hapo hapo na mshahara wa "entry level" mpaka wabadilike au wajiachishe wenyewe kazi.

Mfumo huu wa "performance based" upo na unatumika sana ulimwenguni, hususan kwenye kazi zisizo za Serikali, pia serikali nyingi zimeanza kutumia mfumo huo, bila kuoneana aibu wala huruma za kijinga.

Uzoefu wangu wa kufanya kazi za kuajiriwa kwa muda mrefu sana katika nchi zilizoendelea umenifundisha hayo.
Asante sana ndicho nilichozungumza, watu wako bize kudai mshahara wakati ni wavivu katika kufanya kazi
 
Unajua wasio-perform ndio wanakula mishahara mikubwa, kuliko wanao-perform? Wengi wanajua kucheza na akili za maboss wao.
 
I totally agree. Hii itaongeza ufanisi na uwajibikaji.
Sawa kabisa mradi mfumo ufumwe kwa mtazamo mpana (broader perspective) ya tathmini (evaluation) ya nguvu kazi. Kila nafasi ya kazi iwe na tathmini ya misingi (fundamentals), malengo, nidhamu, miiko, mafunzo endelevu kazini, nukta chanya na hasi (positive and negative points). Aaah mlolongo wa vipimo (measures) ni mrefu sana na inabidi ufatwe kimadhubuti (strictly).

Of course utekelezaji wa tathmini ya wafanyakazi kwa mtazamo mpana ya kila muda (periodical) fulani ina gharama (costly) zake kubwa lakini ikifanywa kwa misingi yenye makali (stringent fundamentals) kwa wanao tathminiwa na wanaotathmini itazaa matunda ndani ya miezi 12 mpka 24. Gharama zitajilipa maradufu kwa ufanisi wa muda mrefu utakao patikana.

Na mfumo huo utaifanya serikali kuwa ni kweli mtoa huduma kwa wateja wake(raia).

Wale wakubwa wa serikalini watakaopenda niwape ushauri wa kina kuhusu huu mpango wanitafute inbox, nipo tayari kuutoa ujuzi wangu bure kwa serikali yangu. Na mashirika binafsi wanaweza pia kunifata inbox lakini kwa mashirika kutakuwa na malipo, tena wakumbuke, huduma zangu siyo rahisi na non negotiable.
 
Sisi madereva wa halmashauri za wilaya ni uchafu tu.Gari ikifika muda wa matengenezo,basi itakaa gereji mwaka mzima.Sasa hapo utanipimaje kwa mfano na kosa ni la mwajiri mwenyewe?.
 
Asante sana ndicho nilichozungumza, watu wako bize kudai mshahara wakati ni wavivu katika kufanya kazi
Siyo wavivu tu, ni wazembe wa hali ya juu. Utamkuta muda mrefu anaupoteza kwenye simu kwa mambo yake binafsi kuliko kazi iliyomuweka pale, ni uzembe wa hali ya juu.
 
Tanzania tuachane kabisa na mfumo wa kuwapandishia watu mishahara au vyeo bila kuwa na vigezo na vipimo vya "performance" zao.

Nashauri kwanza viwekwe vigezo na vipimo vya "performance" kazini ndivyo vitumike kuwapandisha watu vyeo na mishahara.

Ni wepesi sana kupanga vigezo vya ubora wa utendaji kwa kila kazi katika kila sehemu ya kazi. Tena siku hizi kila kitu kinakuwa kwenye data base kidigitali ni wepesi sana. Wale watendaji bora (best performers) watapanda mishahara na vyeo haraka na wale wazembe (kama ilivyo kwa Watanzania wengi) watasota hapo hapo na mshahara wa "entry level" mpaka wabadilike au wajiachishe wenyewe kazi.

Mfumo huu wa "performance based" upo na unatumika sana ulimwenguni, hususan kwenye kazi zisizo za Serikali, pia serikali nyingi zimeanza kutumia mfumo huo, bila kuoneana aibu wala huruma za kijinga.

Uzoefu wangu wa kufanya kazi za kuajiriwa kwa muda mrefu sana katika nchi zilizoendelea umenifundisha hayo.

Nakuunga mkono 100%. Tuache mfumo wa kupandishana vyeo bila kujari uchapakazi wa mtu.
Anayefanya vizuri ndio apewe promotion na kulipwa vizuri
 
Rais amehoji, mbona hakuna bango linaloonyesha jitihada za wafanyakazi katika kuboresha uchumi wa nchi ila kila bango ni kuhusu mishahara tuu.
Hahaha wakajibuje? Kila mwaka tunaona wanadai mishahara tuu, bidii katika kazi hatuiioni
 
Iendane na facilitation,anapanga bajeti yake kama mtumishi,inaletwa kama ilivyo kama huko private,tuone kama atashindwa kuperform
Hilo pia ni tatizo kubwa sana. Ili uweze kufanya kazi zako kwa ufanisi unahitaji say bajeti ya billion 7 unapangiwa 2.6 na unapata 2.2. Utafanyaje?
 
Sisi madereva wa halmashauri za wilaya ni uchafu tu.Gari ikifika muda wa matengenezo,basi itakaa gereji mwaka mzima.Sasa hapo utanipimaje kwa mfano na kosa ni la mwajiri mwenyewe?.
Kwa mfumo madhubuti wa tathmini, itajulikana tu seli ya kuzalisha saratani iko wapi na seli hiyo itasambaratishwa mapema sana kabla haijazalisha saratani. Cha msingi ni mara tu baada ya mfumo tajwa kuanza kazi ni kusambaratisha (kukata) kabisa saratani iliyokwisha anza kushamiri, mapema sana.
 
Siyo wavivu tu, ni wazembe wa hali ya juu. Utamkuta muda mrefu anaupoteza kwenye simu kwa mambo yake binafsi kuliko kazi iliyomuweka pale, ni uzembe wa hali ya juu.
Yaanii, kuchelewa kazini wao, kuchelewesha submission za documents ila wao wacheleshewe mshahara Hapo utaelewa
 
Sidhani kama unajua namna kazi za serikali zinavyofanya ( hasa Watumishi wa chini Kama Halmashauri ambako ndio Kuna Watumishi wengi ).

Hivi unajua Watumishi wengi mishahara yao ni 300,000 hawana nyumba, hawana overtime, pesa za mawasiliano, nauli Wala chochote ). Hivi hujui kiwa hata pesa za stationeries wanatoa mifukoni na sometimes mpaka wanachangia Mwenge.

Jamani ukiona hata Rais anakaa kimya ujue anajua hali HALISI.
Hizo sio wasifanye kazi. Pia sio sababu za kutofanyiwa tathmini ya kina. Tathmini ya kina itabaini uozo uko wapi na pia itakuwa ni mkombozi wa wafanya kazi. Kuliko sasa wajanja wachache hawaishi kukaa vikao vya kulipana pesa za bure.
 
Hahaha wakajibuje? Kila mwaka tunaona wanadai mishahara tuu, bidii katika kazi hatuiioni
Hakuna jibu hapo, watu wanaangalia tumbo tuu kila mwaka stori n ile ile kuongezewa mshahara
 
Tukicopy ya Saud Arabia itapendenza
Sana tena, katiba yao ni Qur'an na implementation zake ni Sunna.

Si unawaona wanavyoendelea, tutawapata wapi sisi? Tena wana standards za hali ya juu sana.
 
Lichama linaiba kura miaka nenda rudi halileti maendeleo vs rasilimali mkilichalenji linauwa na kuteka watu kwanini msianze kuliondoa lichama la hivi kabla hamjaenda kwa walimu na watumishi wanyonge?
Kazi hii ya kuiondoa tunakupa wewe mkuu
 
Kwa mfumo madhubuti wa tathmini, itajulikana tu seli ya kuzalisha saratani iko wapi na seli hiyo itasambaratishwa mapema sana kabla haijazalisha saratani. Cha msingi ni mara tu baada ya mfumo tajwa kuanza kazi ni kusambaratisha (kukata) kabisa saratani iliyokwisha anza kushamiri, mapema sana.
Asante.
 
FaizaFoxy umeongea point kubwa Sana... Mimi naogopa sana Kufanya kazi Serikalini sababu ya Kudumaza Career growth na bigger opportunities, Serikalini unahudhuria tu ofisini na Kudumaza uwezo wako...

Serikali ukishapata 1M ukaongezewa 2% unasherekea wiki nzima, this is very bad
 
Back
Top Bottom