Tanzania yaongoza Afrika kwa kuwa na asilimia chache ya raia wake ambao ni diaspora

Kwa kiswahili chetu hiki na teknolojia yetu hii ya "umbea na unafiki" mtanzania atavuna utajiri gani nchi za watu?

Nchi haina misingi ya kuandaa watu wake kupenya ktk soko la uchumi wa nje
 
Ni umasikini na ushamba wetu ndiyo unaotusumbua
Uswahili, umbea, unafiki na uzandiki unatufanya tusitoke hata nje. Na tukitoka hatutoboi.

Nitajie mtanzania aliyevuna hela nje hata mmoja mwenye makampuni hapa bongo. Hayupo! (Watakuja na visingizio ooh tunaogopa kuinvest kwasabb ya kukosa uraia pacha)
 
Kwa upande wangu naona watanzania hua ni watu wakulizika na wanachikipata na wakat mwingne watanzania weng hawapendi kusumbuka yan mtu afuatilie ubarozini visa au kadi ya kuishi nje Mwaka watanzania weng ni hawawezi na hawana mda uwo

Lakin pia kuna suala la watu kutoroka wakifika ulaya ila kwa mtanzania ni ngumu kutoroka akifika ulaya ntakupa mfano mtu akijifungua au mwaliko wa kuja kumsalimia ndugu ulaya weng mda wa kuishi ulaya ukiisha kwa watanzania weng wanatabia ya kurudi tz ila kwa wenzetu weng hutoroka na kubakia uko

Tunalalamika roho mbaya kwa waliotangulia inaweza ikawa kwel au pia isiwe kwel sabu nafasi za kwenda ulaya zipo ni suala la kufuatilia ttzo wabongo tunapenda sana kushikwa mkono kwenye kila kitu vtu vingne km unania unafanya mwenyewe ni kutafuta tu vyanzo vya kueleweka na kuaminika bas
Opportunity za kusoma au kufanya kaz ulaya kla sku znatangazwa ila wabongo tuntaka ad tushikwe mikono na watu

Ukifuatilia waafrika weng wanaoishi ulaya na marekan weng ni wazamiaji illegal alien
Kitu ambacho wabongo weng hatuwezi fanya.
Umenda kusoma, kufanya kazi, kusalimu ukimaliza unazamia uko uko wabongo ilo hatuwezi
 
Hati ya kusafiria tu kizungumkuti kuipata licha ya kwamba ni chanzo kizuri kabisa cha mapato kwa serikali kupitia wizara ya mambo ya ndani (uhamiaji) Serikali imewekeza pesa nyingi sana kwenye mfumo mpya wa hati za kusafiria lakini tunaambiwa utoaji wake ni chini ya hati laki mbili (200,000) toka wameanza tena kwa tabu sana hapo
 

Labda Tanganyika na sio Zanzibar
 
Na nchi zinazoongoza ni zile zenye machafuko......
Middle east na ukanda wa Red sea, ndio zinaongoza hapo.
Unataka watanzania waondoke wanakimbia nini?
Wanakimbia CCM na mateso yake
 
Umekazwa ujamaa na uswahili wa kina Nyerere saa ngapi utapata exposure ya kwenda Nje? Ndio maana Nchi Ina washamba na mbumbumbu wengi.
 
Sio roho mbaya ni madhara ya mfumo wa Kijamaa
 
Watanzania tunapaswa kutembea kifua mbele kwa takwimu hizo. Hii inaonesha kuwa nchi yetu ni nzuri ndiyo maana kila mtu qnatamani kubakia hapa hapa nchini.

Diaspora kuwa wengi Ina maana nchi haikaliki, haivutii, haina potential kwa watu wake.
Ujinga mwingine wa kiwango Cha Ujamaa Sugu πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Ndio maana nyie Wanyonge na walima mahindi mnalazimisha Watoto wenu wasome Kiswahili harafu Watoto wao wanawasomesha Shule za Kingereza za ndani au Nje ya Nchi 😁😁
 
Kusafirisha unapanua wigo wa fursa za biashara, connection na Ajira pia exposure ya kujifunza wenzenu wanachofanya na kuja kujifanya vyema zaidi kwako.
 
humu wanasema mutu akiongea madini apewe mauwa yake.mm nasema upewe maua mukuu umetema manyongo makari ya ukweri.
 
Ujinga mwingine wa kiwango Cha Ujamaa Sugu πŸ˜‚πŸ˜‚
Shida umeshikiwa akili. Unadhani ukienda nje ndiyo utatoboa. Nonsense!

Unaondoka Tanzania ili uende wapi?
Tanzania imejaa neema tupu hii.
1. Ni nchi ya pili kwa vivutio vya utalii duniani baada ya Brazil.
2. Ni nchi ya pili kwa wingi wa madini Afrika.
3. Ni nchi yenye ardhi kubwa yenye rutuba ya kutosha.
4. Nchi yenye amani mpk ikabatizwa kuwa kisiwa cha amani.

Unataka ukabebe maboksi nje? Hizo akili ama matope?
 
Kwa hili nchi ni mseto wa choroko na wali unaosababisha haya. Kuanzia ujamaa ulitufanya kuwa mazezeta, roho mbaya, fitna na majungu na mauchawi, waliotoboa kubania wenzao, elimu mbovu, lugha shida. Hayo tu mkulugenzi.
 
Kwa mwaka jana tu wametoa PP 136000
 
Tanzania uswahili mwingi na ushamba mzigo

Si unaona dp world tu mtu hata hajui mkataba ulivyo anaukataa na kusema nchi imeuzwa miaka 100
 
Wewe umetoboa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…