Tanzania yaongoza Afrika kwa kuwa na asilimia chache ya raia wake ambao ni diaspora

Tanzania yaongoza Afrika kwa kuwa na asilimia chache ya raia wake ambao ni diaspora

Kwa kiswahili chetu hiki na teknolojia yetu hii ya "umbea na unafiki" mtanzania atavuna utajiri gani nchi za watu?

Nchi haina misingi ya kuandaa watu wake kupenya ktk soko la uchumi wa nje
Hapo kwenye kuandaa Sasa ndio tupafanyie kazi hasa kwa kuangalia mitaala ya elimu tunazotoa katika nyanja zote na sio kusifia kuwa hatuendi sana nje wakati hata hapa ndani tulipo tumeanza kupoteza umiliki tunaogopa hadi Mnyarwanda
Imagine kazi ya ndani ya nchi mtanzania hawezi compete na foreigner bila back up ya serikali inauma ila basi tu acha tuendelee kujisifia
 
Mm nawazidi diaspora wengi tu ambao wananyanyasika huko Ulaya kwa kubeba maboksi na kuosha/kuchamba wazee
Unawazidi sababu hao diaspora bongo walikuwa mateja ama walizamia meli ama walikimbia vita ya pemba hawana elimu wakati wewe ukute una degree unajilinganisha nao.

Siyo kwamba kuwa nje lazima uwe tajiri kama wewe unavyotaka kuliweka, bali nikuwa na muono wa upande wa pili wao wanafanya je na pia kuwa na ile mindset sahihi linapokuja suala la mustakbali wa Taifa na kukabiliana na changamoto.

Mtu aliyehuhishwa na kuona upande wa pili wa maisha kwa mfano, asingeweza kusaini mkataba wa DP na wala tusingekuwa tunabishana nani aongoze nchi na kwanini sisi masikini wala kusingekuwa na ubishano wa chawa, bali wote tungekuwa ktk mstari mmoja.

Kinachosumbua TZ ni ujima. Na akili ya wengi kuwa haijaiva haina exposure nzuri sababu haijawekwa ktk stress test. wengie hufikiri ya kwamba ukipata pesa basi wewe umemaliza na unamzidi asiye na pesa kwa wakati huo na huna haja yakutoka popote.

Kwa kumalizia tu hakuna ukombozi uliofanyika duniani kwa mtu ambaye hajawahi kuwa diaspora fuatilia toka enzi za Yesu mwenyewe , Musa , nk wote walikuwa. Na hasa kasome kitabu cha Shaban Robert kusadikika kwanini nchi ile ilishindikana kabisa kuendelea mpaka yule mfalme akatuma wajumbe watoke waende nchi zingine.
 
Tanzania tupo sawa na Marekani
World Bank wametoa report inayoitwa 'Ratio of persons living abroad to origin country population' ambapo kwenye report hiyo Tanzania inapungufu ya asilimia moja ya raia wake wanaishi nje ya nchi.

View attachment 2667693

Asilimia hizo ni chache kuliko mataifa yote ya nchi za Africa.

Mind you, Tanzania ni nchi pekee yenye wazungumzaji wengi wa Kiswahili.

Je, huu uthibitisho kwamba Kiswahili hakivuki maji? Au ni kwamba watanzania wengi wana mapenzi na nchi yao?
 
Watanzania tunapaswa kutembea kifua mbele kwa takwimu hizo. Hii inaonesha kuwa nchi yetu ni nzuri ndiyo maana kila mtu qnatamani kubakia hapa hapa nchini.

Diaspora kuwa wengi Ina maana nchi haikaliki, haivutii, haina potential kwa watu wake.
No kweli nchi yetu nzuri, hivi mfano nchi za Marekani, Ujerumani, England nazo zina Diaspola wengi kuizidi Tanzania?

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
No kweli nchi yetu nzuri, hivi mfano nchi za Marekani, Ujerumani, England nazo zina Diaspola wengi kuizidi Tanzania?

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
Ukijibiwa unitag. Yaani mleta mada anataka tuone fahari watanzania kuikimbia nchi yao na kwenda kuishi nchi nyingine???!
 
Ukijibiwa unitag. Yaani mleta mada anataka tuone fahari watanzania kuikimbia nchi yao na kwenda kuishi nchi nyingine???!
Nchi yetu ni tajiri hakuna sababu yoyote ya kukimbia nchi, wazungu wanaipenda sana Tanzania na Africa kwa ujumla.

Ni ujinga mkubwa,mfano Mzazi ana watoto lakini watoto wanatoroka kwao na kwenda kuishi kwa majiea, halafu mzazi anajisifu na kulaumu watoto wa wengi kwanini hawaendi kuishi kwa watu.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Watz wengi kwa akili zetu fupi tunafikiri kuwa na diaspora wengi ndio mafanikio.

Ni kweli kuna changamoto katika taratibu za kutoka nje. Pia kuna shida na tabu nyingi ndani ya nchi hii, zikichangiwa zaidi na mfumo wetu wa kiutawala.

But all in all, we should thank God a thousand times for the way we are. Ukitaka kuelewa kidogo tu Tz tulivyo safi vuka border hapo Sirari uone maisha yalivyo tofauti kule utakakoingia, hata salamu utatamani uinunue.

Kuna watu humu juzikati nimeshangaa kuona wakiwasifia Somalia kwa kuwa na diaspora wengi, huku wakiwish nasi tuwe kama Somalia! Wonderful!
Tanzania kutokuwa na diaspora wengi siyo sifa. Na Somalia kuwa na diaspora wengi siyo sifa. Tanzania ina wachache kwa sababu ya uelewa wa watu uko chini. Somalia wako wengi kwa sababu ya machafuko.
 
Ukweli ni kuwa watz wengi hawaongei kiingereza fasaha sababu ya kusoma kwa Kiswahili. Nje kuna fursa nyingi tunazikosa na lugha inayotumika zaidi duniani ni English. Watawala wengi Wana roho mbaya hawataki watz kwenda kunufaika nje! Nchi inakosa remittance na kubaki maskini.
Solution ni kubadili lugha ya kufundishia kutoka Kiswahili kuwa English.
Watz wanapenda kwenda nje hasa vijana wasio na ajira ila Njia zote zimefungwa!
Wsethiopia wasomali hawajui hata English mbona wajaa ulaya na USA
 
Ni ujinga mkubwa,mfano Mzazi ana watoto lakini watoto wanatoroka kwao na kwenda kuishi kwa majiea, halafu mzazi anajisifu na kulaumu watoto wa wengi kwanini hawaendi kuishi kwa watu.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
Kuwa na diaspora wengi ni jambo zuri sana. Hata Shabaan Robert na waandishi wengi waliotukuka wameelezea kwa kirefu faida za kusafiri na kuishi nchi za wengine. Hivyo basi conclusion yako haijaangalia nje ya box. Fikiria hivi: Nchi A ina raia milioni 60. Mwaka huu wa 2023 kati ya hao raia milioni 60 kuna diaspora milioni 10. Baada ya miaka 5 wale diaspora milioni 10 wanarudi nchini kwao, na wengine milioni 10 wanaenda nje (wanabadilishana). Na nchi B ina raia milioni 60 na kati yake ina diaspora milioni 1. Baada ya miaka 5 wale diaspora wanarudi kwao na wengine milioni 1 wanaenda nje. Huoni kuwa ile yenye diaspora wengi ndiyo itafaidi? Kwa kifupi ni kuwa diaspora inaleta package ya faida kutoka sehemu mbalimbali za dunia.
 
Tanzania kutokuwa na diaspora wengi siyo sifa. Na Somalia kuwa na diaspora wengi siyo sifa. Tanzania ina wachache kwa sababu ya uelewa wa watu uko chini. Somalia wako wengi kwa sababu ya machafuko.
Umejibu kiusahihi lakini sijui kama wengine watakuelewa!
 
Shangaa serikali Yako.

Inatia ugumu upatikanaji wa passport ila kwenye mikataba fasta inatia Saini bila hata kufikiria.

Passport tu yaweza ongeza Pato kwa serikali just imagine raia milioni 15 waziombe na kupewa so Hela ndefu hio.
Huko tena, bila hata kusoma [emoji16][emoji16] wanaangusha signatory.
 
Back
Top Bottom