Tanzania yashindwa kwenye kesi, yaamuriwa kulipa fidia ya zaidi ya Tsh. Bilioni 260

Tanzania yashindwa kwenye kesi, yaamuriwa kulipa fidia ya zaidi ya Tsh. Bilioni 260

Kwa kuwa kiboko yao alishakufa, serikali itashindwa kesi zote na kulipa fidia, kama ilivyokuwa kabla ya Magufuli kupanda jukwaa.
 
Kituo cha Kimataifa cha Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji (ICSID) kimeiamuru Tanzania kulipa dola milioni 109.5 (zaidi ya bilioni 260 za Tanzania) kwa kampuni za uchimbaji madini zilizosajiliwa Uingereza, Ntaka Nickel Holdings Ltd na Nachingwea UK Ltd, kufuatia uamuzi wa mwaka 2018 kufuta Leseni yao ya Kuhifadhi madini ya Nikeli.

Kampuni hizo zilifanikiwa kuishitaki Tanzania katika mahakama ya Benki ya Dunia kwa kukiuka majukumu yake chini ya Mkataba wa Uwekezaji wa Nchi Baina ya Uingereza na Tanzania (BIT) na sheria za kimataifa kwa kunyang'anya leseni hiyo.

Tanzania pia imetakiwa kulipa dola milioni 3.859 za gharama za kisheria kwa wadai, pamoja na ada na gharama za mahakama ya ICSID.

Kampuni ya Indiana Resources Ltd iliyoorodheshwa kutoka Australia, ambayo ndiyo wanahisa wengi wa mradi wa nikeli wa Ntaka, iliwahi kutishia kukamata ndege zinazoendeshwa na Kampuni ya Air Tanzania (ATCL). Indiana inasema sasa itachukua hatua haraka kutekeleza tuzo ya mahakama

Kampuni za EcoDevelopment na EcoEnergy za Uswidi mwaka jana zilishinda uamuzi wa $165m dhidi ya Tanzania kwenye ICSID kufuatia uamuzi wa serikali ya Magufuli kuwanyang'anya wawekezaji hao ardhi ya Bagamoyo, kinyume na Mkataba wa Uwekezaji wa Nchi Baina ya Sweden na Tanzania (BIT)

Kampuni hizo zilikamata ndege ya Airbus inayomilikiwa na Wakala wa Serikali wa Ndege za Serikali (TGFA) inayoendeshwa na ATCL ili kutekeleza hukumu ya ICSID.

Ndege hiyo yenye namba za usajili 5H-TCH hivi karibuni ilirejea Tanzania baada ya serikali kumaliza kesi hiyo.

View attachment 2691787

Pia soma: Maamuzi ya Magufuli yaigharimu Tanzania zaidi ya Bilioni 266
Hii ninpicha ya kitakachokuja baada ya kulazimishes mkataba wa Bandari
 
DP world kikiumana huko mbele ya safari, watakamata ndege hazitatosha kulipa...unaweza ukazuka msako wa kukamata DIASPORA wakatumikishwe kazi uarabuni hadi deni liishe...
Labda watawapa Serengeti, Ruaha, Mikumi, au Kilimanjaro, Gesi au madini mengine kama Fidia.
 
Hili balaa moja tu la bandari la shangazi yako linayazidi yote ya mwendazake.
Kweli kuna Sababu, silaha, madawa, wanyama, madini yatapishwa na wao wanavyojikisia. Sio tu Tanzania itaathiri nchi zote jirani.
 
We subiri tu...

Hata Lissu kasema huu mkataba ni lazima uvunjwe hata tulipe pesa kiasi gani ni sawa tu...

Magufuli ndiyo alitumia maguvu kuvunja mamikataba haya ya hovyo lakini kimsingi alikuwa sahihi. Sema
sasa hakuna uzalendo na tumerudi kule kule. Hawa hawa wanaotushinda mahakamani wanaweza kurudi na wakasaini tena mikataba kama ile ile aliyoivunja Magufuli...Hovyo tu!

View attachment 2691843
Kushinda ni lazima washinde kesi maana mikataba waliingia wao na nilazima wawasaidie kushinda kesi
 
Kituo cha Kimataifa cha Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji (ICSID) kimeiamuru Tanzania kulipa dola milioni 109.5 (zaidi ya bilioni 260 za Tanzania) kwa kampuni za uchimbaji madini zilizosajiliwa Uingereza, Ntaka Nickel Holdings Ltd na Nachingwea UK Ltd, kufuatia uamuzi wa mwaka 2018 kufuta Leseni yao ya Kuhifadhi madini ya Nikeli.

Kampuni hizo zilifanikiwa kuishitaki Tanzania katika mahakama ya Benki ya Dunia kwa kukiuka majukumu yake chini ya Mkataba wa Uwekezaji wa Nchi Baina ya Uingereza na Tanzania (BIT) na sheria za kimataifa kwa kunyang'anya leseni hiyo.

Tanzania pia imetakiwa kulipa dola milioni 3.859 za gharama za kisheria kwa wadai, pamoja na ada na gharama za mahakama ya ICSID.

Kampuni ya Indiana Resources Ltd iliyoorodheshwa kutoka Australia, ambayo ndiyo wanahisa wengi wa mradi wa nikeli wa Ntaka, iliwahi kutishia kukamata ndege zinazoendeshwa na Kampuni ya Air Tanzania (ATCL). Indiana inasema sasa itachukua hatua haraka kutekeleza tuzo ya mahakama

Kampuni za EcoDevelopment na EcoEnergy za Uswidi mwaka jana zilishinda uamuzi wa $165m dhidi ya Tanzania kwenye ICSID kufuatia uamuzi wa serikali ya Magufuli kuwanyang'anya wawekezaji hao ardhi ya Bagamoyo, kinyume na Mkataba wa Uwekezaji wa Nchi Baina ya Sweden na Tanzania (BIT)

Kampuni hizo zilikamata ndege ya Airbus inayomilikiwa na Wakala wa Serikali wa Ndege za Serikali (TGFA) inayoendeshwa na ATCL ili kutekeleza hukumu ya ICSID.

Ndege hiyo yenye namba za usajili 5H-TCH hivi karibuni ilirejea Tanzania baada ya serikali kumaliza kesi hiyo.

View attachment 2691787

Pia soma: Maamuzi ya Magufuli yaigharimu Tanzania zaidi ya Bilioni 266
Duh!
 
Wana ccm wote wanaishi bila UBONGO na ndio maana miaka yote ya utawala wao ni hasara kwa nchi!!!
Ha ha ha [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] kwahiyo wapo empty, sasa wataishije jamani!
 
Wale wana sheria wetu waliotuwakilisha huko wanatosha kweli? Vilaza kweli
 
Kilichosalia ni sisi wananchi kuuzwa na kuishi kama watumwa au wakimbizi
 
Magufuli alifuta mkataba mbovu.msiwe vilaza kwa kusapoti mikataba ya ovyo.
Sasa huo unaousema wewe mbovu qatu wanajichotea mi dollars bila kufanya kazi.

Kumbuka huo siyo wa kwanza na huo siyo wa mwisho. Juzi ndege imetoka kukombolewa Uholanzi, na hizi tukichelewa kulipa deni linaongezeka kila kukicha, wazungu walivyo wahuni wanawacha ziongezeke, wajiingizie ziyada bila jasho.
 
Magufuli alifuta mkataba mbovu.msiwe vilaza kwa kusapoti mikataba ya ovyo.
Kufuta ni kitu kimoja ila namna unavyofuta ndio kitu kingine. Unaweza tafuta kipengeke kilichovunjwa ukaenda ICSID huko ukadai mkataba uvunjwe. Ila sio unaamka tu asubuhi unaenda kunyang'anya leseni hata kama una haki ila mchakato uliotumika utaku-cost.
 
Kutokana haya
1.Kushindwa mara kwa mara kwa hizi kesi za madai kwenye Mahakama za Usuluhishi
2. Mgawo wa Umeme
3.Upatikananji duni wa Maji Mijini na Vijijini
4.Uendeshaji duni wa mradi wa DART+ ATCL
5.Uendeshaji mbaya wa Bandari zetu
6Uendeshaji duni na mbaya wa TAZARA+ TRC na mengine mengi
NI KIELELEZO CHA UONGOZI MBOVU WA SERIKALI YETU CHINI YA CHAMA CHAKAVU
 
Back
Top Bottom