Tanzania yasitisha vibali vya usafirishaji wa mahindi nje ya nchi

Wewe ndiye unazungumza mambo usiyoelewa. Vitu ulivyokaririshwa na wanasiasa. Fahamu lengo kuu la serikali kupiga marufuku uuzaji wa mazao ya chakula nje. Lengo si kuzuia wewe usife njaa, lengo ni ili serikali yenyewe isianguke. Moja ya mambo yanayoingiza watu barabarani ni bei ya chakula kuwa juu kwa watu wa mijini. So serikali zinazuia kupanda kwa kufunga mipaka na kuhakikisha bei ya nafaka ipo chini. Hili limefanyika tokea enzi za Waroma

Hili linamuumiza nani? Mkulima anayelima. Matokeo yake anashindwa kulima. Matajiri wanaacha kulima. Benki zinaacha kopesha wakulima na njaa inatokea, tena kubwa. Na hili si nadharia. China walikuwa na sera kama hizi zetu. Matokeo yake ni njaa iliyoua mamilioni. Mwisho wake wakaja na mpango. Mkulima anaiuzia serikali sehemu fulani ya mazao yake. Labda 10% yanayobaki yote anauza anakotaka na kwa bei anayotaka. Matokeo yake uzalishaji ukakua kwa mara kadhaa zaidi, leo China njaa ni historia.

Huo utaratibu mnaotaka ufanyike unaleta njaa badala ya kuzuia.
 
Bei ya nafaka kupanda sio chachu ya watu kulima, Bali ni suala la hali ya hewa na inflation kwa wakati huo. Mkulima Sasa hivi anauza mahindi gunia 150000 lakini bado hakuna aanachofaidi sababu bidhaa nyingine nazo zote zipo juu na bahati mbaya Hakuna mkulima anayelima mazao yote. Nae akienda kununua maharage anakutana na bei kubwa, anayelima maharage nae akienda kununua mahindi nae anakutana na bei kubwa. Wote hao ea maharage na mahindi wakienda kununua alizeti wanakutana na bei kubwa

Kikubwa ni kucontrol inflation
 
Hata hueleweki!!mala sio mwananchi asife njaa, mala inafanya hivyo ili mwananchi asiingie mtaani!!
Hapa kwetu ni wakulima wangapi wanaoweza kwenda bank na kupata mikopo? Ni matajiri wangapi hapa kwetu wanawekeza kwenye mazao ya chakula(mahindi, mchele)
Kwanza wanapofunga mipaka mkulima wala sio muathirika mkubwa kwani yeye alishauza vigunia vyake wakati tu alipovuna.Wafanya biashara ndio waathirika kwani walikwenda wakanunua mazao kwa bei ndogo wakayahifadhi, sasa wanapiga pesa.
 
sifurahii hili mana nililima kwa hela yangu nbolea bei juu.Niache nhuze kwa bei ghali nirudishe gharama zangu na faida kwanini mnafunga mipaka?
 
Bashe hafai, msimamo/Imani yake ya kuendekeza kupeleka chakula nje ndiyo iliyotufikisha hapa! Sasa anazuia nini wakati chakula limeisha! Endeleeni tu viongozi mnazidiwa ufahamu na mkulima! Umetuletea maisha magumu, ningekuwa rais wewe ungepumzika umeshachoka!
 
Bashe hafai, msimamo/Imani yake ya kuendekeza kupeleka chakula nje ndiyo iliyotufikisha hapa! Sasa anazuia nini wakati chakula limeisha! Endeleeni tu viongozi mnazidiwa ufahamu na mkulima! Umetuletea maisha magumu, ningekuwa rais wewe ungepumzika umeshachoka!
 
Tuliwaeleza muda mrefu wakashupaza mashingo, tuliwaambia mavuno hayakua mazuri wakaleta hadithi zao
Kama uliwahi ishauri serikali ifunge mipaka , basi ulikuwa huishauri vizuri na nina imani wewe ni mfanyabiashara wa mahindi wa hapa nchini,

Kutakuwa na njaa , ni kweli , lakini mwaka huu kwa mara ya kwanza mkkulima wa mahindi ame enjoy bei nzuri kutoka kwa wakenya na waganda

Ishauri serikali iweke mazingira mazuri kwa mkulima , ikiwepo punguzo la kodi na ruzuku kwa pembejeo., mfuko wa mbolea laki , halafu unataka mkulima auze mahindi kilo sh 250. Mkulima anadidimia , mfanyabiashara ananeemeka,
 
Sema huelewi. Ngoja nikueleweshe tena. Bei ya chakula ni moja ya kitu huingiza wananchi barabarani haraka sana na kupindua serikali. Sasa ili kuzuia hilo serikali huakikisha wanadhibiti bei ya chakula. Na njia mojawapo ni kuzuia uuzaji wa chakula nje. Hivyo, serikali haizuii uuzaji ili wananchi wasife njaa bali ni ili isianguke.

Wanapofunga mipaka mkulima na kilimo vinaathirika pakubwa sana. Usiangalie mwaka huo tu. Huyo mfanyabiashara akipata hasara unafikiri mwaka unaofuata mkulima atakuwaje? Benki gani itakopesha mkulima ambaye soko na bei ya mazao yake havieleweki? Unafikiri mkulima mkubwa aliyepata hasara sababu ya kufunga mipaka mwaka unaofuata atalima? Kuna kutumia matrekta na mbolea wakati bei ipo fixed chini kabisa? Hii unafunga leo, kesho unafungua ndiyo itatuletea njaa.
 
Hayo mahindi ni ya mkulima au serkali yanayozuiwa kuuzwa nje. Tuache ujinga, mkulima ananufaika na nini hapo. Pembejeo juu halafu soko anapangiwa .
Yeye ndio anaweka akiba kwa chakula chake. Kama serkali inaona kutakuwa na njaa inunue kwa mkulima iweke kwenye ghala zake.
Hii nchi haieleweki yaani wanasimamia nini

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
 
Cycle ya kutozalisha mahindi kwa msimu iliopita ilitokana na bei mbovu za mahindi, kwa msimu uliopita , mahindi yaliwahi kuuzwa 220 kwa kilo , wamati huo mbolea ya can na urea mfuko wa kilo 50 ni shilingi laki moja , , katika hali kama hii wakulima wengi walilima kwa ajili ya chakula tu wakenya wamekuja kwa bahati bahati tu,
 
Si wamesema Rutto ana mashamba ya mahindi ambayo akivuna ni mara tatu ya mahitaji ya mahindi kwa mwaka nchini Kenya.

Wamwambie rais wao awape mahindi wale sima.
Kwa hio na mimi nipatepo asara ya mahindi angu ama. Mi nitawauzia wakenya kwa bei naetaka. Asa mkianza mambo ya papatu papatu achen yakae ndani. Hayaozi
 
Kwan TISS ndii kazi yao? Wizara inafanya kazi gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…