14 “Mwanadamu, aliyezaliwa na mwanamke,
+ Ana maisha mafupi
+ na yenye kujaa msukosuko.
+ 2 Amechanuka kama ua na kukatiliwa mbali,
+ Naye hukimbia kama kivuli
+ wala haendelei kuwako.
3 Ndiyo, umefungua macho yako juu ya huyu, Nami unanitia katika hukumu
+ pamoja na wewe.
4 Ni nani anayeweza kutokeza mtu safi kutoka katika mtu asiye safi?
+ Hakuna hata mmoja.
5 Ikiwa siku zake zimeamuliwa,
+ Hesabu ya miezi yake iko kwako; Umeweka amri kwa ajili yake ili asiweze kuvuka.
6 Geuza macho yako kutoka kwake ili apumzike,
+ Mpaka apate raha kama mfanyakazi wa kukodiwa anavyopata katika siku yake.
7 Kwa maana hata kwa ajili ya mti kuna tumaini. Ukikatwa, utachipuka tena,
+ Na tawi lake halitakoma.
8 Mzizi wake ukizeeka katika udongo Na kisiki chake kikifa katika mavumbi,
9 Utachipuka unaponusa harufu ya maji
+ Nao utatokeza tawi kama mmea mpya.
+ 10 Lakini mwanamume hufa na kulala akiwa ameshindwa; Na mtu wa udongo hukata pumzi, naye yuko wapi?
+