TANZIA: Mbunge wa Songea Mjini, Leonidas Gama(CCM) afariki dunia

TANZIA: Mbunge wa Songea Mjini, Leonidas Gama(CCM) afariki dunia

Sipendi kumpangia Mungu majukumu ya wapi pa kumuweka nani..Mwenyezi Mungu aiweke nafsi yake mahali panapostahili kulingana na matendo aliyotenda enzi za uhai wake!
 
View attachment 636895

TAARIFA YA AWALI:


Wadau nimepata taarifa muda huu zinasema mbunge wa Songea mjini Mh. Leonidas Gama hatunaye tena....

UPDATE:

JamiiForums imepata uthibitisho wa taarifa za kifo cha Mhe. Gama ambacho kinadaiwa kutokea muda wa Saa 6 kuelekea Saa 7 usiku wa kuamkia leo.

Amefariki akiwa mbunge wa Songea Mjini na amefariki dunia usiku wa kuamkia leo hii Songea katika Hospitali ya Peramiho.

Gama amewahi kuwa mkuu wa wilaya ya Muheza, Nachingwea, Newala, Mbeya na Ilala. Vilevile amewahi kuwa mkuu wa mkoa Kilimanjaro.

Inadaiwa marehemu Gama alianguka nyumbani kwake saa saba usiku juzi huko Likuyu; akapooza upande wa kushoto akawa hajitambui kabisa na akapelekwa Hospitali ya Peramiho ambako aliwekewa mashine za kumsaidia kupumua.

Mungu ailaze roho ya Marehemu Mahali pema peponi.

Hivi huyu jamaa na yule kiongozi wa zamani wa ccm marrhum Lawrence gama wana uhusiano gani je ni ndugu?
 
huyu mzee alipokuwa Kilimanjaro alitaka kusaidia wanaume Rombo waache pombe ili wapate nafasi ya kutimiza nyajibu zao ili wanaume wa Kenya wasizidi kuja kula mizigo
 
Kifo si cha kusikitikia kwa sababu ni fair outcome kwa kila chenye roho. Kinachonisikitisha mimi kwa kifo hichi ni kwamba hajaiwahi Chato Intl Airport!
 
Sipendi kumpangia Mungu majukumu ya wapi pa kumuweka nani..Mwenyezi Mungu aiweke nafsi yake mahali panapostahili kulingana na matendo aliyotenda enzi za uhai wake!
Vizuri kabisa!!!Mungu wala hapambwi na maneno yetu eti "kalale pema peponi" baada ya kifo ni hukumu,na mtu akisha kufa matendo yake yanafuatana nae na atakaa ambapo panastahili.

~Huko ni kupamba makaburi kwa malumalu wakati ndani ni mifupa.huo ni ubatili mtupu
na kujilisha upepo

Luka 16:15-20,tajir na masikin kila mtu alienda anapo stahili.
 
Huo unene inaelekea alizaliwa nao maana sio wa kushibia misosi ....ni Bahati mbaya.....kwaheri ..lala mahala pema peponi ......Amina
 
Kila mtu ataonja mauti japo naona kama vile mauti inatuwahi mno kabla ya wakati muafaka wa kudhania tungestahili kufa uzee wa kutosha. Poleni familia ya Songea yote na jf. Hivi RIP nini maana yake wadau?
RIP = Rest In Peace (Pumzika kwa Amani)
 
Vizuri kabisa!!!Mungu wala hapambwi na maneno yetu eti "kalale pema peponi" baada ya kifo ni hukumu,na mtu akisha kufa matendo yake yanafuatana nae na atakaa ambapo panastahili.

~Huko ni kupamba makaburi kwa malumalu wakati ndani ni mifupa.huo ni ubatili mtupu
na kujilisha upepo

Luka 16:15-20,tajir na masikin kila mtu alienda anapo stahili.
Nilipata kusikia hadithi za kale kwamba ikiwa mtu alikuwa mwema duniani akifa nafsi yake huingia kwa kiumbe kingine mathalan mtoto mdogo ila hufutwa kumbu kumbu zote kwamba aliwahi kuishi, ila kama mtu hakuwa mwema akifa nafsi yake humwingia kiumbe kingine kisicho binadamu na kumbu kumbu kwamba aliwahi kuishi hazifutwi...tunajisumbua tu kwa kumtakia pepo mwanasiasa, ni ukweli mchungu kwamba katika kundi la wanasiasa 1000 ni mwanasiasa sifuri atakayeionja pepo ya Mwenyezi Mungu!
 
Poleni sana wafiwa.

Sijui ni nini kimempata, lakini kwa mwili ule aliokuwa nao, hatari za kupata Presha, Kisukali na Mshtuko wa Moyo zilikuwa haziwezi kuepukika.

Inasemekana alitoka India for check-up hivi karibuni; akapita Dodoma, baadaye akaelekea Songea kumpokea Waziri mkuu ambaye alikuwa aanze ziara leo.

Kuna wakati aliugua akapelekwa India ila sikumbuki tatizo lilikuwa nini.
 
Back
Top Bottom