Horseshoe Arch
JF-Expert Member
- Aug 10, 2009
- 13,402
- 12,792
View attachment 636895
TAARIFA YA AWALI:
Wadau nimepata taarifa muda huu zinasema mbunge wa Songea mjini Mh. Leonidas Gama hatunaye tena....
UPDATE:
JamiiForums imepata uthibitisho wa taarifa za kifo cha Mhe. Gama ambacho kinadaiwa kutokea muda wa Saa 6 kuelekea Saa 7 usiku wa kuamkia leo.
Amefariki akiwa mbunge wa Songea Mjini na amefariki dunia usiku wa kuamkia leo hii Songea katika Hospitali ya Peramiho.
Gama amewahi kuwa mkuu wa wilaya ya Muheza, Nachingwea, Newala, Mbeya na Ilala. Vilevile amewahi kuwa mkuu wa mkoa Kilimanjaro.
Inadaiwa marehemu Gama alianguka nyumbani kwake saa saba usiku juzi huko Likuyu; akapooza upande wa kushoto akawa hajitambui kabisa na akapelekwa Hospitali ya Peramiho ambako aliwekewa mashine za kumsaidia kupumua.
Mungu ailaze roho ya Marehemu Mahali pema peponi.
Vizuri kabisa!!!Mungu wala hapambwi na maneno yetu eti "kalale pema peponi" baada ya kifo ni hukumu,na mtu akisha kufa matendo yake yanafuatana nae na atakaa ambapo panastahili.Sipendi kumpangia Mungu majukumu ya wapi pa kumuweka nani..Mwenyezi Mungu aiweke nafsi yake mahali panapostahili kulingana na matendo aliyotenda enzi za uhai wake!
Ni mgonjwa siku nyingi tu na inafahamika wazi. Sio kila unene ni matatizo wengine ndio walivyo.ule mwili lazima ungemletea athari,RIP
Aliyekuwa mpinzani wake joseph fuime alisharudi ccm.alimsumbua sana. Angebaki chadema angepita, amepishana na gari la mshahara.jimbo lipo wazi hilo, kazi kwenu ukawa
Kwa hili la kulinda mazingira kwa Kilimanjaro alifanikiwa kwa jitihada zake RIPR. I. P mhe Gama nakukumbuka sana ulivyokua mkuu wa mkoa wa kilimanjaro ulijitahidi sana kulinda mazingira kwani kaka yangu ulimnyanganya chensoo yake ambayo alikua anafyeka nayo miti ya mbao
RIP = Rest In Peace (Pumzika kwa Amani)Kila mtu ataonja mauti japo naona kama vile mauti inatuwahi mno kabla ya wakati muafaka wa kudhania tungestahili kufa uzee wa kutosha. Poleni familia ya Songea yote na jf. Hivi RIP nini maana yake wadau?
Kwa simu zetu hizi unaandika 'kama' inakuletea '****' usipokua makini unatukanaHiki ni nini?
Nilipata kusikia hadithi za kale kwamba ikiwa mtu alikuwa mwema duniani akifa nafsi yake huingia kwa kiumbe kingine mathalan mtoto mdogo ila hufutwa kumbu kumbu zote kwamba aliwahi kuishi, ila kama mtu hakuwa mwema akifa nafsi yake humwingia kiumbe kingine kisicho binadamu na kumbu kumbu kwamba aliwahi kuishi hazifutwi...tunajisumbua tu kwa kumtakia pepo mwanasiasa, ni ukweli mchungu kwamba katika kundi la wanasiasa 1000 ni mwanasiasa sifuri atakayeionja pepo ya Mwenyezi Mungu!Vizuri kabisa!!!Mungu wala hapambwi na maneno yetu eti "kalale pema peponi" baada ya kifo ni hukumu,na mtu akisha kufa matendo yake yanafuatana nae na atakaa ambapo panastahili.
~Huko ni kupamba makaburi kwa malumalu wakati ndani ni mifupa.huo ni ubatili mtupu
na kujilisha upepo
Luka 16:15-20,tajir na masikin kila mtu alienda anapo stahili.
Kwa style ya sasa ndo amekutana nalo.Ali
Aliyekuwa mpinzani wake joseph fuime alisharudi ccm.alimsumbua sana. Angebaki chadema angepita, amepishana na gari la mshahara.
Tusiendekeze sana uzito mkubwa, ni hatari kwa afya!Mbunge wa Songea Mjini ndugu Gama Leonidas amefariki usiku wa kuamkia Leo. Rip Mheshimiwa Gama.
View attachment 636894
Poleni sana wafiwa.
Sijui ni nini kimempata, lakini kwa mwili ule aliokuwa nao, hatari za kupata Presha, Kisukali na Mshtuko wa Moyo zilikuwa haziwezi kuepukika.