Taratibu za kufuata ili kumiliki Silaha ya Moto Tanzania

Taratibu za kufuata ili kumiliki Silaha ya Moto Tanzania

Maduka ya kununua bastola dar yapo kama 2 ninayoyafahamu moja lipo pale mitaa ya stesheni, nyuma ya jengo la TRA, linaitwa Tanganyika Arms. Hili ni private(meaning price pia ni kubwa). Pia unaweza kwenda kununua pale Makao Makuu ya Jeshi Upanga kuna duka la Mzinga(bei fresh sana pale ila nyingi ni za kutoka nchi za kisoviet). Vile vile unaweza kuagiza ulaya kama unataka quality like Colt 45 na ikifika unaiclear halafu inahifadhiwa pale Tanganyika Arms mpaka upate kibali(Ila kuwa makini sana hapo maana inabidi jamaa wakutumie serial number ya bastola, wakiiuza na kuleta ingine kazi utakuwa nayo kwenye kuprocess kibali)

Kupata kibali cha kumiliki ndo kimbembe maana procudure inaanzia kwa mtendaji wa kata ambaye anaitisha kikao cha usalama na wanaclear. Ukitoka hapo unaenda polisi wilayani, for clearance, then wilayani, baada ya hapo ni kwa mkuu wa mkoa ambapo unakuwa endorsed na kikao cha usalama cha mkoa. Kwa Dar nasikia kinafanyika mara chache sana. Ukimaliza hapo ndo unaenda Polisi Mkoa then Makao Makuu ya Polisi(Registry, na figure prints department) na finaly kibali kinatoka kwa DCI.KIbali kikitoka unaenda kuchukua "Ngoma yako".

Kuna watu imewachukua zaidi ya mwaka kwa hii process, lakini wengine inachukua miezi 2, depending on your connection.

Goodluck

hapo kwenye red, LOL, na huko kote lazima wakuchomoe!! I better consult Al Shabaab, i can get it without any bureaucracy!!
 
Habari zenyu bana! Muko poa natumaini,waungwana mi nna shida ya kumiliki silaa ndogo, je utaratibu ukoje ili mtu aweze kumiliki slaa ni ayo tu waungwana,
....Sawazisha kiswahili chako bana humo kwenye red kunatia kinyaa!!
 
nyani ngabu na faiza hebu njoeni muedit hii lugha hapa.

Utata mtupu, hapo namuachia Nyani Ngabu. Maana kuna Slaa katajwa humo na mimi najulikana ni Gamba orijino. naweza kuambiwa nimegeuza jina la rais wa magwanda.
 
Kama upo Dar, nenda "central police" wana kitengo cha kumiliki silaha pale watakupa maelezo au tembelea maduka ya silaha watakupa maelezo.

Hautaki mabomu?
Faiza hapo kwenye mabomu sikuelewi huyo kahitaji bastora sasa mabomu ya nini, kupasua miamba au kulipua mahala?
 
waaachina wana skendo ya kuwa na vitu ovyo, lakini si vifaa vyao vya kivita. ni bora kuliko vifaa vya nchi zote. Fikiri, SMG hata iingie mchanga kiasi gani, lakini bila hata kuisafisha, ikisha koki tu, inamaliza tukio, hali ni tofauti kwa bunduki za kimarekani, isirel na kijeruman

Acha story kila m2 anajua hiyo? We sema itapatikana vp?kwan 2nataka hzo Ak 47, 12 nako kazuri na kabazoka au ka rpg .acha uoga fidel castro alichukua inji akiwa kopolo sasa ata wewe? Wake up bro.
 
Nauliza utaratibu wa kumiliki silaha(bastola) ukoje? Naomba nijuzwe plse
 
Unatakiwa kuomba kibali kwanza. Kibali kinaombwa kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya yako, ukifika utapewa fomu ya kujaza na baada ya hapo utasubiri kamati ya usalama ya wilaya ikae na kuidhinisha upewe kibali cha kumiliki silaha au la (kutokana na historia yako).

Baada ya kupata kibali, unaenda either pale upanga jeshini kuna duka la silaha pale ndani au lugalo. Ukishapata kibali ni pm nikuelekeze aina gani ya silaha inakufaa kwa mazingira yako.

Pia natoa huduma ya kufundisha shabaha kwa fee kidogo (kwa sababu kumiliki silaha ni jambo moja na kujua kutumia ni jambo lingine).
 
Nauliza utaratibu wa kumiliki silaha(bastola) ukoje? Naomba nijuzwe plse
Unapotaka kumiliki silaha, unatakiwa kupeleka ombi /barua katika kamati ya ulinzi na usalama ya mtaa/kijiji ikiwa na maelezo ya lengo la kutaka kumiliki silaha husika na aina ya silaha.
kamati ya ulinzi na usalama ya mtaa/kijiji itajadili ombi lako na kuliwasilisha kwa kamati ya ulinzi na usalama ya kata ambayo m/kiti ni mtendaji wa Kata na katibu ni OCS (MKUU WA KITUO KIDOGO CHA POLISI).

Baada ya kujadiliwa, kamati hiyo itawasilisha muhtasari wa kijiji/mtaa na ule wa kata kwa mkuu wa polisi wa wiliya(OCD)/manispaa atawasilisha kwenye kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya.

Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ndiyo yenye mamlaka ya mwisho ya kubariki maamuzi ya kamati za mtaa/kata au kubatilisha.
 
Back
Top Bottom