Taratibu za kufuata ili kumiliki Silaha ya Moto Tanzania

Taratibu za kufuata ili kumiliki Silaha ya Moto Tanzania

Kwanza kabisa naomba nitoe pole kwa watanzania wenzangu wote tulioguswa na msiba wa Dada yetu Regia....R.I.P
Direct to the point, kwa tathmini yangu naona vibaka wanazidi kuwa wengi huku uraiani na wala siwashangai hawa vibaka ila naishangaa hii serikali iliyoshindwa kuwafungulia mianya ya ajira.

Kwa wingi wa vibaka hawa sasa si vibaya kubuni mbinu za kujihami,nafikiria kuwa na kasilaha kamoto japo kadogo,nimejaribu kutafuta kwenye website kibao za nchi yetu kuhusu requirements and procedures za mtu kuweza kumiliki hii kitu sijaona.Kindly mwenye uelewa katika hili naomba kujua requirements na procedure za kumiliki silaha ni zipi?Kadirio la processing costs pamoja na Bei ya baadhi ya silaha.
 
Kuna thread ya jambo hili humu jaribu kusearch
ila ni utaratibu wenye mlolongo mrefu na ambao unazidi kuwa mgumu kila siku.
uwe na akili timamu na pia sababu za ukweli za kuhitaji ulinzi binafsi.

Nenda pale Tanganyika Arms stesheni ama Mzinga Coperation makao makuu ya jeshi la wananchi utapewa form ambazo ukijaza utaanzia kwamjumbe wa shina watafanya kikao na kuforward maombi yako kwa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya na huko ukiitwa kwa interview then watakuforward ngazi ya mkoa kwa uhakiki zaidi na hatimae kwa DCI
Lakini kwa nchi hii utaratibu huo unaweza kuwa mgumu ama mwepesi kulingana na mfuko wako na pia influence yako kwawahusika.

Hivyo waweza kupata kirahisi, au kiugumu au usipate kabisa!!
Silaha ndogo ni wastani wa milioni moja na nusu hadi tatu kwa manunuzi halali na risasi ni kama 1,400 tu kwa moja na kisheria unatakiwa upate si zaidii ya pc 25 kwa mwaka
 
kuna thread ya jambo hili humu jaribu kusearch
ila ni utaratibu wenye mlolongo mrefu na ambao unazidi kuwa mgumu kila siku.
uwe na akili timamu na pia sababu za ukweli za kuhitaji ulinzi binafsi
Nenda pale Tanganyika Arms stesheni ama Mzinga Coperation makao makuu ya jeshi la wananchi utapewa form ambazo ukijaza utaanzia kwamjumbe wa shina watafanya kikao na kuforward maombi yako kwa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya na huko ukiitwa kwa interview then watakuforward ngazi ya mkoa kwa uhakiki zaidi na hatimae kwa DCI
Lakini kwa nchi hii utaratibu huo unaweza kuwa mgumu ama mwepesi kulingana na mfuko wako na pia influence yako kwawahusika
Hivyo waweza kupata kirahisi,au kiugumu au usipate kabisa!!
Silaha ndogo ni wastani wa milioni moja na nusu hadi tatu kwa manunuzi halali na risasi ni kama 1,400 tu kwa moja na kisheria unatakiwa upate si zaidii ya pc 25 kwa mwaka

Asante kwa ushauri wako mkuu
 
umesahau kama uko tz?ukienda kisheria utachemka,nenda tanganyika arms au kule arusha,muone muhusika yoyote na umweleze shida yako.atakutajia bei na kukueleza siku ya kwenda kuchukua tu mambo mengine yote wanafanya wenyewe,hakuna jambo rahisi kama kupata silaha ktk nchi hii ndugu yangu pesa yako tu.
 
Silaha yenyewe unaenda kufanya nayo uhalifu au ni kukabiliana na hao vibaka ulosema wameongezeka mitaani?
 
Mtafute mwanasheria .... ataprocess vitu vyote, wewe kai yako kwenda atapokwambia uende.
Kama ni high profile lawyer atakuprocess mpaka kibali cha kubeba.
 
Nisaidieni utaratibu ukoje hadi nitinge nayo dar,maana nipo ugaibuni na nahitaji ninunue moja.maana hizo za Tanganyika arms mh!sio zenyewe wakuu.na pia ipi ni nzuri kwa self defence(kufukuzia vibaka/majambaza) maana malima kanitisha,kama ndo mambo yenyewe hayo huko bongo,heri nije na kimguu changu cha kuku
 
Go for "Glock 19 (9mm)". Hii in ubora sawa na AK 47.
 
umenena mkuu.Glock ndio kila kitu na be yake ni tzs milioni.mbili na nusu
 
Hata ukiipata wauzaji wataituma kwenye agent aliyeteuliwa kuhifadhi silaha. Huwezi kuja nayo wewe kama wewe na hata ukikubaliwa lazima u-hand it over to pilot then ataikabidhi kwa bohari la silaha. Kwa hapa kwetu ni Tanganyika arms. Wataihifadhi mpaka hapo utakapokamilisha taratibu za kuimiliki.

Kuna vikao vya ulinzi na usalama vya kijiji hadi mkoa vitakavyokaa na kukupitisha ili umiliki silaha. Then Mwenyekiti wa ulinzi na usalama mkoa atapeleka jina lako Wizarani then kama una bahati utapewa KIBALI thereafter unaenda Tanganyika Arms kuchukua msala wako.
Kwa wanaomiliki silaha ni kitu hatari sana! Huna uhuru hata kidogo. Ukiacha nyumbani lazima uwe na uhakika wa safety locker. Ukiwa nayo kwenye gari omba vibaka wasiipitie! Ukiiweka kiunoni omba watu wasiione na usiingie nayo bar!

Usiwe na hasira za haraka! Yaani jamaa anatoka huko atokako kapanda ile mbaya afu anamshika your my wife makalio! Lazima uchomeo ka mguu ka kuku (Yule askari pale Moshi alikasirishwa akenda kuchukua SMG kwenye corola). Achilia mbali wale wenye mabinti ukute kapindwa kwenye ua wa pale home! Saa nyingine wale wenzetu wanakufata wanakwambia hawajajia kingine wanataka JEMBE na ukibisha wanakutoa roho. Si kitu muhimu sana kuwa nacho kwa kweli.
 
Mkubwa,ngoja niigoogle nione,naweza nkawa natembea nayo kweli hiyo?let me check

Nimekupatia ushauri wa kwanza na wa mwisho. Hautajutia baadaye na utanikumbuka sana tu. Risasi za 9mm zinapatikanika kiurahisi zaidi na Glock yenyewe ndo umefika hapo. Bongo wanauza 2.7millioni.
 
Hata ukiipata wauzaji wataituma kwenye agent aliyeteuliwa kuhifadhi silaha. Huwezi kuja nayo wewe kama wewe na hata ukikubaliwa lazima u-hand it over to pilot then ataikabidhi kwa bohari la silaha. Kwa hapa kwetu ni Tanganyika arms. Wataihifadhi mpaka hapo utakapokamilisha taratibu za kuimiliki.
Kuna vikao vya ulinzi na usalama vya kijiji hadi mkoa vitakavyokaa na kukupitisha ili umiliki silaha. Then Mwenyekiti wa ulinzi na usalama mkoa atapeleka jina lako Wizarani then kama una bahati utapewa KIBALI thereafter unaenda Tanganyika Arms kuchukua msala wako.
Kwa wanaomiliki silaha ni kitu hatari sana! Huna uhuru hata kidogo. Ukiacha nyumbani lazima uwe na uhakika wa safety locker. Ukiwa nayo kwenye gari omba vibaka wasiipitie! Ukiiweka kiunoni omba watu wasiione na usiingie nayo bar! Usiwe na hasira za haraka! Yaani jamaa anatoka huko atokako kapanda ile mbaya afu anamshika your my wife makalio! Lazima uchomeo ka mguu ka kuku (Yule askari pale Moshi alikasirishwa akenda kuchukua SMG kwenye corola). Achilia mbali wale wenye mabinti ukute kapindwa kwenye ua wa pale home! Saa nyingine wale wenzetu wanakufata wanakwambia hawajajia kingine wanataka JEMBE na ukibisha wanakutoa roho. Si kitu muhimu sana kuwa nacho kwa kweli.

Ujumbe mzuri sana huu kwa Kimeo anayetafuta hicho kitu.
 
Go for Gock 19 mkuu ni compact size. Siyo kubwa sana na wara sioi ndogo sana.
 
Nimekupatia ushauri wa kwanza na wa mwisho. Hautajutia baadaye na utanikumbuka sana tu. Risasi za 9mm zinapatikanika kiurahisi zaidi na Glock yenyewe ndo umefika hapo. Bongo wanauza 2.7millioni.

Mshauri pia aache starehe na awe anawahi nyumbani mapema wasije wakamnyang'anya. Hawakawii kumtaka awape JEMBE mkuu! Mi namshauri aachane na hii kitu kama hajatulia!
 
Tanganyika arms wanauza ghali mno ukitaka bei nzuri nenda duka la jeshi ( mzinga ) badala ya kununu 2.7m utapata kwa 1.5m . Tembelea mzinga hakika hutarudi Tanganyika arms.
 
Tanganyika arms wanauza ghali mno ukitaka bei nzuri nenda duka la jeshi ( mzinga ) badala ya kununu 2.7m utapata kwa 1.5m . Tembelea mzinga hakika hutarudi Tanganyika arms.

Nimewasoma wakuu,lakini pia vibaka wakikuotea wanaweza wakakufanya kitu mbaya kama huna hiyo kitu,tatizo pia mtaani wanaamini eti ninayo kwavile tu mi ni mjeshi.mgogoro mkubwa ni namna ya kuitunza maana inabidi iwe sehemu ya mwili wako
 
Bora waendelee kuamini hivyo hivyo na wala usijishughulishe kuinunua!
Ngoja kwanza! Mjeshi hajui taratibu za silaha! Hajui mzinga wanauza silaha! Yuko mamtoni wala hajawahi kuona silaha anaomba ushauri kwa raia! YOU MUST BE JOCKING!
Tulia wewe fanya kazi acha kuota!
 
Rejea post yangu ya awali,nimesema nipo wapi na ninataka ushauri gani
 
Nimewasoma wakuu,lakini pia vibaka wakikuotea wanaweza wakakufanya kitu mbaya kama huna hiyo kitu,tatizo pia mtaani wanaamini eti ninayo kwavile tu mi ni mjeshi.mgogoro mkubwa ni namna ya kuitunza maana inabidi iwe sehemu ya mwili wako
Nunua browning 7mm ni ndogo kama pen hivyo ukiiweka mfukoni wala haitakusumbua kwa vile ina uzito kiduchu
 
Back
Top Bottom