Taratibu za kufuata ili kumiliki Silaha ya Moto Tanzania

Tuma maombi kwenda serikali yako ya mtaa/ kijiji.

Ukipitishiwa yataenda ngazi ya kata, hapo ukifanikiwa ombi lako litapelekwa kwenye kamati ya ulinzi ya wilaya.
Kumbuka wenye nafasi kubwa ni ngazi yako ya kata, lakini ngazi ya wilaya ni pagumu kiasi.

Baada ya hapo utasubiri idhini ya umiliki.

USHAURI.

Usidhani kuwa uko salama zaidi kumiliki silaha, na kama huwezi ni heri kutifikiria kumiliki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1.Uwe na miaka 31 Au zaidi.

2.Nenda kwenye maduka yanayouza silaha Mzinga,Tanganyika arms au popote chagua silaha unayoipenda unalipia unapewa risiti lakini unaiacha na unapewa form ya kwenda kujaza.

3.Unaenda kuijaza kwanzia kata mpaka mwisho kwa OCD.kila muktasari wa vikao vinaambatanishwa

4.Ocd akiridhia anakupa namba inajazwa ambayo inakuwa ni namba ya silaha.

5 unapewa silaha na accessory zake unaweza kununua pia.risasi kwa mwaka ni 20 tu unless otherwise


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nashukuru kwa maelezo yako mkuu
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maelezo yako yamenipa mwanga kabisa wapi kwa kuanzia..shukrani sana
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiongozi habari, taratibu au sheria anazopaswa mwenye silaha ya moto kuzitii ni zipi ili aweze kuwa salama pasipo kuwa na uzembe wa matumizi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sheria anazopaswa kuzitii mtu mwenye silaha ni zipi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna kitu kama hicho mkuu unaaza kwaza kununua silaha ndipo ziaza taratibu za kisheria kumiliki chuma usipopewa kibali cha kumiliki bunduki utarudi dukani unaandika barua ya kurudishiwa pesa yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…