Taratibu za kufuata ili kumiliki Silaha ya Moto Tanzania

Taratibu za kufuata ili kumiliki Silaha ya Moto Tanzania

Naimani mko poa wakuu. Jamani me nahitaji kumiliki bastola tu maana kuna people zina mazoea mabaya sana. Tunachukuliana poa poa huku mtaani, watu wakuda sana!

Hasa me nataka nimiliki gun lengo sio niue mtu no! Nikipiga hata juu kumtisha inatosha.

Ila wakuu kiukweli kuna some people wanazingua sana yan, wanamazoea mabaya sana. Yan hapa ndo naelewa kwann wazungu wanapenda kuishi kwenye maeneo tulivu yasiyo na mchanganyiko wa watu wengi.

NB: Naomba kuelekezwa tu hatua za kufuata ili niweze kumiliki CHUMA
 
Ili umiliki ile unahitaji uwe mtu hivi!
Sio kwaajili yakupiga juu au kuwatisha watu wapate story yakuongea kitaa
 
Sawa nakutakia kila kheri kama hujaoa, ila ukitaka kuoa usitegemee utampata mwenza labda ufiche kuwa unacho na kama umeshaoa nakushauri uachane na huo mpango maana naona una hasira za haraka haraka.
 
Wewe inainesha ni mtu wa kupanic sana, kwa utaratibu na vikao vya halali unaweza usipate kibali. Ila kwa nguvu ya fedha labda unaweza kupata.

Halafu toa sababu ya msingi ya kutaka kumiliki silaha.
 
Hadi sasa umeangalia movies ngapi za James Bond?! Lini umemamliza kuangalia spy series?! Au ndo umetoka kuangalia 24 klwahiyo ushajiona ndo Jack Bauer flani hivi sio?! Au usikute ndo unaji-fantasies na Jason Bourne!
 
inunue kwanza na kuiacha hapo ulipoinunulia, kuna mlolongo mrefu wa vibali, kuanzia serikali ya mtaa mpaka mkoani. nilichukua miezi 15 kuipata baada ya kuwa nimelipia, pengine sasa hv mamabo yamebadilika
 
Nenda polisi kituo kilicho karibu nawe watakuelekeza kila kitu.
Kama uko Dar nenda Makao pale

Sent using Jamii Forums mobile app
Utaratibu wa kumiliki silaha Bongo unaweza kusema uliwaambia unataka kumiliki silaha ili ukavanmie Ikulu! In short, ukishajaza fomu, inaanzia kwenye Serikali ya Mtaa kabla ya kwenda ngazi ya kata na hatimae wilayani na kisha mkoani ambako maamuzi yanaenda kuidhinishwa na vigogo wa polisi na usalama wa taifa!
 
Wajemeni eeh

Kuuliza si ujinga na kuuliza njia ndio kujua njia!

Nahitaji bastola, kwa self defence tu, si vinginevyo! Sababu; najiona vulnerable mno huko 'uswekeni' ninakoishi. Hamna umeme, na majirani wanahesabika, BTW, practicing targets zipo za kutosha huko!

Najua humu kuna wengi tu wanaomiliki silaha kikazi, na wanaomiliki silaha kwa sababu kama zangu mie,..tatizo sijui "a" wala "be" nianzie wapi, meaning sheria na taratibu zikoje Bongo kumiliki silaha, hivi kuna duka la silaha Bongo?

Wapi?

Mfano; nikipata semi auto M92 Beretta yenye uwezo wa rounds 12 au 15 inatosha, au kuna 'limit' ya silaha ya aina gani naruhusiwa kuwa nayo? natamani kuagiza nje lakini nahofia nisijebanwa na sheria za uingizaji silaha...







Sheria ya umiliki wa Bunduki Tanzania


Mikoani utaanzia kwa watendaji mtaa halafu unapitsha katani. Then Kuna makaratasi ya kujaza police . Ukiwa umeishainunua Lakini na unaiacha dukani na namba zake zinatumika ktk makaratasi hayo ya police.
Baada ya hatua hiyo utabaki kusubiri kujadiliwa na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya, na baadaye ya mkoa. Hapa ujihadhari na maswali ya mtego mtego, Ukipita mtihani huo unabaki kusubiri wa taifa wakupitishie kibali chako. Kama ni shortgun na rifle taratibu zinakomea mkoani, lakini pistol mpaka wa taifani wajiridhishe.
 
Kwema?

Mimi ni mfanya biashara wa vifaa vya ki electroniki ofisi zangu kwa siku huwa tunakua na pesa za mauzo cash. Ambazo huwa tunazihifadhi kwa ajili ya kuwekwa Bank kesho yake.

Sasa vibaka na wezi wanatufanyia michezo sana mwanzo waliniibia zaidi ya Milioni 10 na vifaa vingine hyo ilikua mwaka jana na trials za kuniibia tena zaidi ya tano maana pesa huwa nakuja nazo nyumbani kuweka kwenye Safe Box.

Nitakuja kuandika uzi wa experience niliopitia baada ya kuibiwa ukiangalia nilikua sijasimama vizuti na niliwezaje kurudi kwenye map.

Sasa ndugu zangu naomba kwa anaejua ni taratibu gani za kufuata ili kumiliki silaha kihalali kwa ajili ya self defense yangu na mali zangu.

Asante
 
Bunduki unazunguka Sana. Nenda Mlingotini- Bagamoyo kwa Babu. Atakayeiba tu anakua mkeo unajilia unavyotaka
 
Habari za jioni wadau Nataka kumiliki silaha either bunduki au bastola so nilikua naomba kwa wenye uzoefu naomba kujua sehemu naweza kununua silaha na bei zake na ni vibali gani vinahitajika hadi niweze kumiliki silaha niatashukuru sana kama nitaweza kupata maelekezo
 
Habari za jioni wadau Nataka kumiliki silaha either bunduki au bastola so nilikua naomba kwa wenye uzoefu naomba kujua sehemu naweza kununua silaha na bei zake na ni vibali gani vinahitajika hadi niweze kumiliki silaha niatashukuru sana kama nitaweza kupata maelekezo
 
... karibu kila mji (makao makuu ya mikoa) kuna duka la silaha. Nenda dukani utapewa utaratibu.
 
Back
Top Bottom