Taratibu za kufuata ili kumiliki Silaha ya Moto Tanzania

Sawa ahsante
 
Nadhani Kuna haja ya kuwapima watu akili kwanza. Mental stability ni muhimu Sana katika umiliki wa silaha. Pia temperament ingepimwa isije kuwa ni mtu wa temper temper atufyatue kitaa tukimtania Ana bichwa bovu.

Secondly kuna haja ya kuwachunguza kwanza Ili kubaini kama kuna malicious intent mahali. Isije kuwa anajiandaa kumpiga mtu tukio.
 
Hahaha.. Una hoja mkuu.

Ila naihitaji kwa ajili ya ulinzi binafsi
😂😂
 
Duuh..hizi procedures zinachosha hakuna shortcuts.

#MaendeleoHayanaChama
 
Habari zenu wakuu.

Mwenye uelewa wa haya mambo ya kumiliki silaha hasa hizi ndogo kama bastola kwa ajili ya ulinzi binafsi naomba msaada wa kunijulisha taratibu zake zinavyokuwa.

Nazihitaji sana kwa sasa, nataka kufahsmu wapi pa kuanzia
Una akili timamu?
 
nenda kwanza ulipie silaha wao watakupa maelekezo nini ufanye,nenda kwa mtendaji wa kama upate mutsari wa wajumbe 10 wa kata yako,ambapo hiyo barua unaipeleka police ....mengine police watakuambia ufanye nini
 
Unawasilisha ombi lako kwa kamati ya Ulinzi (na usalama) ya Wilaya kipitia OCD then Kamati ya Ulinzi na Wilaya inakujadili na kukupendekeza kwa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa. Huo ndio utaratibu kwa ufupi.
Anaanza n kata anayoishi wajumbe watampa barua ya kuthibitisha ni mkazi wa kata yao na hata makosa yeyote
 
Hapo kwenye kupimwa akili na uelewa kwanza naunga mkono hoja,watu wachunguzwe kuanzia wanapoishi na jamii,
mamlaka zijiridhishe kwa hivyo
maana kuna watu wengine akiwa jombo kitu kidogo anataka kumwaga tackle la mtu
wakiona unafaa mkuki na podo sawa wakiona unafaa mashine yenyewe sawa
 
Duuh..hizi procedures zinachosha hakuna shortcuts.

#MaendeleoHayanaChama
NENDA KAGERA AU KIGOMA UTAPATA SILAHA BORA TENA ZA KISASA KWA BEI NAFUU KUTOKA CONGO, BURUNDI NA RWANDA.
HATA UKITAKA AK47 UTAPATA ILA KIMAAGUMASHI.
 
Kipengele cha kwanza ufafanuzi tafadhali. Kwanini uanze kununua silaha kwanza wakati huna uhakika kama maombi yako yatakubaliwa? Je, maombi yakikataliwa nini hatima ya silaha uliyoinunua?
 
Kipengele cha kwanza ufafanuzi tafadhali. Kwanini uanze kununua silaha kwanza wakati huna uhakika kama maombi yako yatakubaliwa? Je, maombi yakikataliwa nini hatima ya silaha uliyoinunua?
Haupewi, ni kuilipia tu kisha unapewa risiti.

Ikionekana hujakidhi vigezo, pesa utarudishiwa.

Ila ukiishainunua halafu ukafanya uzembe ikachukuliwa[emoji1787]mfano kuisahau sehemh, kumpa mtu mwingine au kuringishia watu. , hupewi hela wala silaha yenyewe tena.
 
Asante kwa ufafanuzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…