1. Naenda kanunue SILAHA kwanza au ujue ni Aina gani ya bunduki unavyo taka kumiliki na specification zake
2. Naenda Kituo cha Polisi kuanzia ngazi ya Wilaya sio vituo vidogo kaombe fomu ya kumiliki silaha inatolewa bure
3. Utajaza taarifa zako binafsi ikiwa pamoja na taarifa za bunduki, Aina na muundo wakepamoja na maker. Pia utaeleza matumizi ya bunduki hiyo
4. Utapeleka fomu kwa mtendaji wa kijiji, kamati itakaa kukujadili na kuandika muhtasari wa kikao pamoja nawajumbe kusaini kwenye fomu yako ya maombi
5 utapeleka fomu kwa mtendaji wa KATA, nao watafanya kama mtendaji wa kijiji
6. Utapeleka fomu kwa OCD -Mkuu wa Polisi Wilaya husika ulipo chukulia fomu nae ataiwadilisha kwa Mkuu wa Wilaya ambeye ndie mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wataijadili kwenye kikao na kutia saini kwenye fomu hiyo na kuituma kwa RPC - Kamanda wa Polisi Mkoa
7. Fomu hiyo itajadiliwa tena kwenye kamati ya ulinzi na usalama Mkoa ikiongozwa na RC baada ya hapo fomu hiyo itatumwa kwa DCI kwa hatua ya mwisho.