Uchaguzi 2020 Tarehe 28/10/2020: Siku ya kuweka Historia kuu Tanzania

Umenena vyema Lord Denning!
 
Kujitegemea ni mchakato na hatujajitegemea kwa asilimia 100, ila tumeanza hatua kwa hatua kukusa mapato ya ndani, kuziba mianya ya uvujaji wa mapato, kuimarisha makusanyo, utegemezi wa wahisani kwenye bajeti umepungua,uchaguzi huu tumeugharimia kwa asilimia 100, ujenzi wa meli kadhaa na vivuko, madaraja, barabara , huduma za jamii.
 

hahhaa aiseee mm kura lazima nipige, lazima nihakikishe kwenye ushindi wa jpm na mm nakua mmoja wapo
 
Busara gani unayotumia kujenga nchi??? Kujenga uwanja wa kimataifa Chatto wakati kuna maelfu ya shule wanafunzi wanakaa chini na hawana hata vitabu??? Wakati kuna maeneo wanakunnywa maji ya tope???

Maendeleo gani unayosema tuchague??? Mipango miji tu mmeashindwa kufanya nchi imejaa squatters!

Hivi unaona ni busara kujenga flyover inayojaa maji kwa mfugale alafu jangwani mmejenga kituo na barabara kwenye Mkondo wa maji??
 
Hivi unajua unaongea na watu wenye upeo wa namna gani??? Hizo data zenu za kupika ishieni kuzitumia kudanganyana kwenye korido zenu za Lumumba huko!! Ni mapato gani ya ndani yamekua??? Kama korosho huuzi nje, Mbaazi huuzi nje, biashara zinafungwa na makampuni ya wawekezaji yanakimbia na watu wanapoteza kazi. Sasa unaweza kusemaje??

Kwani kugharamia uchaguzi kuna gharama gani??? Bil 300 nayo ni hela???
 
hahhaa aiseee mm kura lazima nipige, lazima nihakikishe kwenye ushindi wa jpm na mm nakua mmoja wapo
Kama unajali kweli hii nchi na vizazi vijavyo huwezi kuwa na msimamo wa kumpigia kura magufuli
 
Tano tena kwa JPM, kazi iendelee!
Ukisema tano tena jua ni tano tena za mateso, kukosa ajira kwa vijana, kuuliwa kwa sekta binafsi, kuondolewa kwa dawa nyingi kwenye Bima ya afya na kukosa kwa pensheni kwa wastaafu wetu
 
Kama unajali kweli hii nchi na vizazi vijavyo huwezi kuwa na msimamo wa kumpigia kura magufuli

yaaani mm nkampigie mtu mwenye mdomo mchafu na kuvunja sheria? kwanza kaniblock twitter baada ya kutoa maoni yngu kuhusu magufuli, hapo hajashika nchi tu kashaanza kublock watu, kule youtube ndo kabisaaa chadema channel wamfunga comments
 
Usipumbazwe na propaganda mfu za Mawakala wa Mabeberu, ambao wameshaahidiwa pepo na mabwana zao. Nyerere alitutoa katika ukoloni wa kisiasa. Ni jukumu la kizazi hiki kupigania uhuru wa kiuchumi na wa kujitegemea bila kuathiriwa na ukoloni mambo leo unaotaka kupoka na kujimilikisha njia zetu za uchumi, kwa kupitia mawakala wao!

Miaka mitano mingine kwa Jemedari si jambo la hiari. Ni jambo la lazima ili kulinda utaifa, utamaduni, amani na utulivu kwa maslahi yetu na ya ya Taifa kwa ujumla.
 
Mawakala wa Mabeberu ni kina nani??? Embu fafanua??
 
Ukisema tano tena jua ni tano tena za mateso, kukosa ajira kwa vijana, kuuliwa kwa sekta binafsi, kuondolewa kwa dawa nyingi kwenye Bima ya afya na kukosa kwa pensheni kwa wastaafu wetu
Usihofu, mimi ninaamini ni tano ya amani tele, JPM ana aminika akiahidi anatekeleza! Naomba unifafanulie kidogo kuhusu dawa kuondolewa bima ya afya naona unairudia sana!
 
Naomba ukumbuke pia Chato ni sehemu ya Tanzania, hivyo inayohaki ya kujengwa na kuendelezwa kama sehemu zingine! Usisahau kuna utalii mkubwa wa Burigi, jirani na Geita, ni eneo la kimkakati kukuza uchumi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…