Uchaguzi 2020 Tarime: Tundu Lissu ampiga marufuku Kassim Majaliwa kufanya kampeni, Yadaiwa anavunja maadili ya uchaguzi

Nyani haoni kendezake, mbowe si ni kub ana hadhi ya waziri mkuu kivuli

Siamini kama nimesoma ulichoandika kutoka kwa mTanzania. Mkiitwa mjina yanayowakilisha sifa zenu mtasema mmetukanwa. Sheria inakataza viongozi wa serikali kufanya kampeni na imeenda chini mpk kwa mkuu wa wilaya.

Halafu mpumbavu (fool) mmoja anakuja hapa na kusema Mbowe ana hadhi ya waziri mkuu. Majaliwa ni Waziri Mkuu wa nchii hii. Sio Mbowe!! Ondoa ukoko katika akili yako, huenda ukawa ni mtu wa maana tu ila hapa unajichafua.
 
Mkuu tuwekewe vifungu tukasome sio kutuletea porojo
 
Hakuna popote ambapo Kasim Majaliwa amejitambulisha Kama waziri mkuu hata media hazimtaji kwa cheo chake zinamtaja kwa cheo Cha chama yani ni mjumbe wa kamati kuu kwa hyo tusikaririshwe vinginevyo angetuambia ni kanuni ipi ya Tume iliyovunjwa ili tuwadai nao Tume waje kutoa ufafanuzi juu ya hili
 
Hahaha sikujua nabishana na ccm, alitaka kufahamu kuhusu Mbowe, nikamjibu nawewe umekuja, duh.

Ndiyo kahamia Mbagala.
Ni kufanya mlingano tuu Kaka wala sikubishii, Lissu ni MTU smart sana lakini Kaka sitaki kuamini kwamba the rest of all Tanzania especially members wa CCM wote ni wajinga. SASA kamusi ya nchi ( Tundu Lissu) kasema Majaliwa kakosea, lakini hajamtaja Pinda,Mwanri,Nassari,Ndugai , Bashiru au Wasanii wa Muziki ambao wote wanazunguka Nchi nzima wakiwanadi wagombea wa CCM...SASA Sisi tusiojua vizuri tunaanzaga Kwa kufanya comparison and then tunahoji ili tueleweshwe zaidi..wala hakuna ubishani ndugu..Mimi na wewe ni kitu kimoja tunatofautiana mawazo tuu.
 
Hapo uliposema he is no longer a PM panaonyesha katiba ya nchi huijui vizuri

Bunge lilishavunjwa Mzee. Majaliwa ni Mbunge wa Ruangwa kwa tiketi ya CCM. Wabunge wote walilipwa Mafao yao hivo muda wao wa Ubunge kukoma.
Kama majaliwa siyo Mbunge anaendeleaje kuwa PM?
Wasikilize TBC kwenye taarifa zao kuhusiana na Kampeni za Majaliwa: Wanam- address Kama MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA CCM......Not as a Prime Minister!!!
 
Jikite kwenye hoja. Wewe jiulize anapiga kampeni Kama Nani? He huko anakozunguka anaendelea kutoa maagizo na kufanya kazi za kiutendaji wa serikali? Sina upande wowote kwenye hili najaribu kufafanua hoja kuu.
Hivi leo yuko wapi karagwe au geita
 
Kwamba Lissu ndiye peke yake anajua tafsiri ya sheria? Kama nawe unaamini hivyo iweje ahamasishe wapiga kura kuingia barabarani iwapo hatatangazwa mshindi?

Akili za kinyumbu tu.
Utaratibu wa kuingia barabara siyo kuvunja sheria Wewe! Na mkitaka watu wabakie majumbani, shindeni kwa halali kwenye Box la sivyo mtaongezewa maumivu zaidi ya haya mnayopata sasa!
 
Sio sahihi
Soma katiba
Spika bado ni Job Ndugai
Naibu spika bado ni Betina atulie akson
Waziri mkuu ni majaliwa
Mawaziri na manaibu waziri bado wapo kwenye nafasi zao hadi atakapo apishwa rais mpya.

Muwe mnasoma soma basi, msiwe wavivu kama maccm
 
Kwamba Lissu ndiye peke yake anajua tafsiri ya sheria? Kama nawe unaamini hivyo iweje ahamasishe wapiga kura kuingia barabarani iwapo hatatangazwa mshindi?

Akili za kinyumbu tu.
isome vizuri katiba vizuri siyo unakata mauno humu
 
Lema si alikua na mgombea urais, hata majaliwa akiwa jpm hakuna shida ,shida ni pale anapozunguka peke yake tz tunasheria nyingi mpaka zingine tunazisahau
 
Unaweza kuainisha matusi na uongo wake?
 
Na hata kwenye mikutano yake haipandishwi bendera ya taifa bali ya chama. Kwa mikutano niliyoiona mimi
 
Huyo majaliwa badala ya kufanya kazi za kiserikali anampigia kampeni Jiwe. Nani kampa hayo mamlaka?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waziri Mkuu wa Tanzania atakua mbunge wa kuchaguliwa na atapatikana Kwa kupigiwa Kura na wabunge baada ya jina lake kupendekezwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. mara nyingi ni chama chenye wabunge wengi ndicho kinatoa PM, Majaliwa kapata uteuzi kutoka Kwa Rais ambaye pia ni chairman wa CCM na alikuwa confirmed na wabunge walio wengi kutokea CCM. Na Kwa katiba ya CCM prime minister automatically anakua mjumbe wa NEC. Kumtenganisha PM na Siasa za chama Kwa wakati huu nahisi ni kumuonea bure.
 
Uko sahihi mkuu,hivi huu ni uchaguzi wa ndani ya ccm au ni uchaguzi wa vyama vingi??Eti mjumbe wa NEC kwa hiyo wajumbe wa kamati kuu ya Chadema nao wazunguke nchi nzima kumpigia kampeni Lissu??Kumbe yote waliyofanya kwa miaka mitano na Boss wake wanaona watu hawajawaelewa MLIYEKUWA HAMUMUTAKI KAJA NI YEYE YULEE ALIEONJA KIFO. Hangaikeni nae.
 
Sio sahihi
Soma katiba
Spika bado ni Job Ndugai
Naibu spika bado ni Betina atulie akson
Waziri mkuu ni majaliwa
Mawaziri na manaibu waziri bado wapo kwenye nafasi zao hadi atakapo apishwa rais mpya.

Muwe mnasoma soma basi, msiwe wavivu kama maccm

Inawezekana unasoma lakini HUELEWI. Ulichoandika hapa ni utopolo. Unaposema Spika bado ni Job Ndugai, sijui Tulia Ackson bado ni N/Spika......!!Kwa Bunge lijalo au lipi Kaka? Walokuwa Mawaziri Sasa ndo wanaomba Tena ridhaa ya kurudi Bungeni inawezekanaje waendelee kuwa Mawaziri?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…