Uchaguzi 2020 Tathmini yangu juu ya Uchaguzi Mkuu 2020: Hakuna sababu nzuri ya kukataa kuteua wabunge wa Viti Maalum CHADEMA

Mbona hoja tulishaifunga? Nyie mnawashwa na CHADEMA. Mbona tulishawashauri mchukue wanawake wa ofisi ya NEC, wa polisi na wa wakurugenzi wa wilaya.
 
Sikutarajia kama mama Aron unaweza kuhalalisha uharamia hata kama una nia njema.

Hujasoma hoja yangu.

Kura za Chadema zilizotangazwa, inadaiwa ni kidogo kuliko kura halisi.
Wabunge wa viti maalum wanatokana na kura hizo kidogo.
Kwa hiyo, kupeleka wabunge hakuna uhusiano na kura zinazodaiwa kuibiwa.
Kura zinazodaiwa kuibiwa zinahusiana na wagombea ubunge wa jukwaani.
Umenisoma?
 
Mbona hoja tulishaifunga? Nyie mnawashwa na CDM. Mbona tulishawashauri mchukue wanawake wa ofisi ya NEC, wa polisi na wa wakurugenzi wa wilaya.
Unadai "hoja tulishaifunga."
Ilifungwa kwa mujibu wa kikao gani?
Mbona kura za vikao vya Kamati Kuu ya Chadema haziungi mkono unachokisema?
Fanya utafiti kwanza.
No reserach no right to speak.
 
Ndugu Mama Amon, uelekeo wa upinzani uko 'crystal clear'. Hawakubali kupoozwa kwa nafasi zozote za uongozi na serikali hii kwani machoni pao ni serikali batili.

Strategy iliyopo ni kuwaachia kila kitu CCM kisha kuomba pressure kutoka nje. Mambo yatakapo anza kuwa magumu, wananchi watailaumu CCM na serikali yake pekee. Katika wakati huu wa udhaifu wa dola, upinzani utakua na nafasi nzuri zaidi ya kudai mabadiliko.
 
Chadema hawaja argue kuhusu uhalali wa hizo kura chache bali hawaungi mkono mchakato mzima kutokana na kasoro nyingi zilizojitokeza, kwahiyo uelewa ni muhimu ktkt hili.
 
Kwa heshima, sikubaliani na kauli yako hii hapa.
Kwani mwajiriwa aliyelipwa milioni tatu hapo juu, akazipokea, na kisha akaendelea kudai ziada, alikuwa ameunga mkono ufedhuli wa mwajiri mkorofi?

Mfano wako ni disingenous. Katika Bunge lililopita kulikuwa na takriban wabunge 115 wa upinzani kati ya jumla ya wabunge 384 ( asilimia 30 ya wabunge walikuwa wa upinzani) lakini bado walikuwa wanaburuzwa tu. Wakikubali kuteua wabunge 19 wa viti maalum, jumla itakuwa 21 ambayo ni asilimia 5.8 ya wabunge wote. Kwa mfano ulioutoa ni kama huyo mwajiriwa akubali kupewa shilingi 580,000.00 wakati anastahili milioni 10, kiasi ambacho hakitoshi kumlipa mwanasheria wa kumtetea. Na mwajiriwa akipokea hiyo 580,000 ndio ajue hatapata zaidi maana mwajiri anajua kuwa ana njaa.Ni bora akatae na arudi Mahakamani ili mwajiri abanwe ili alipwe stahili yake yote. Ndio maana wapinzani wanagomea viti hivyo unavyotaka wapokee. Kwa idadi hiyo bora wajikalie nje tu wakati wanatafuta njia mbadala wa kudai stahili yao.

Amandla...
 
Ni mwandishi mzuri na umeshawishi vizuri, asante. Lakini bado sijaelewa kwa nini umeegemea upande mmoja wa kura za Urais na kusahau kura za Ubunge?

Kilichowapa CHADEMA viti 19 wasivyostahili (wamepunjwa) si kura za Urais kama unavyojaribu kudadavua, kilichopelekea CDM kupewa hizo nafasi 19 ni kura za Wagombea Ubunge wote wa CDM isipokuwa katika majimbo ambayo hakukuwa na uchaguzi wa nafasi hiyo baada ya kuenguliwa wagombea wao kwa hila.

Sasa unaiba kura za chama A kwenye majimbo na kuwaongezea chama B, unawatangaza washindi haramu wa chama B, kisha unatumia kura haramu ulizowapunja chama A kuwapa Wabunge wa viti maalum? Hebu kasome wanavyopatikana Wabunge wa viti maalum halafu rudi tena na hoja yako.
 

Tuanzie hapo kwenye msitari. Pressure kutoka nje ni mkakati dhaifu sana kwa mujibu wa Gene Sharp (kitabu nimeambatanisha). Pili, Bunge sio serikali. Serikali sio mahakama. Hapa tuongelee Bunge. Kupeleka wabunge wa iti maalum Bungeni ni sehemu ya mkakati wa ndani ya nchi. Tuanzie ndani, sio nje. Na tatu, soma kitabu hiki kwa umakini halafu tupanue mjadala (attached)...
 

Attachments

Fomula ya kukokotoa idadi ya viti maalum hata kama ikihusisha kura za ubunge haina madhara kwa hoja yangu. Pointi yangu ni kwamba, hizi kura kidogo zilizobaki baada ya kitendo kinachoitwa wizi wa kura ndizo zimezaa viti maalum. Ni kura halali na viti maalum ni viti halali. Kura zinazoitwa haramu ni zile zinazodaiwa kuibwa kutoka upande A na kwenda upande B. Hizo ziendelee kutafutwa. Sina shida ni hilo la pili. Umenisoma?
 
Moja ya kazi ngumu kwa sasa nchi hii ni kuwashauri CHADEMA kuhusu hili. Wakubwa wamekosa ugali huku kukiwa na fursa ya wadogo kupata ugali.
 
CHADEMA hawatambui MCHAKATO MZIMA hivyo hata hiyo halali unayosema wewe kwao ni batili kwa kuwa sio walichotarajia. Hivyo viti maalum 19 wawape TISS tu hakuna namna.
 
Ni bora akatae na arudi Mahakamani ili mwajiri abanwe ili alipwe stahili yake yote. Ndio maana wapinzani wanagomea viti hivyo unavyotaka wapokee. Kwa idadi hiyo bora wajikalie nje tu wakati wanatafuta njia mbadala wa kudai stahili yao.

Nilichofanya ni reasoning by analogy. Utaratibu huu unaanzia kwenye ufanano, na sio kwenye utofauti. Pointi yangu ni kwamba, hivyo viti 19 ni haki ya chadema ambayo inaweza, na inapaswa, kuchukuliwa ili kiwe kianzio cha kudai haki baki. Wabunge hawa wataongeza nguvu ya uchumi ya chama, lakini sio kwa sababu wamependelewa na serikali. Bali kwa kuwa wanayo haki ya kuwa wabunge kutokana na kura halali za Chadema. Wale wagombea ubunge wa jukwaani wanaodai kwamba waliporwa waendelee na hoja. Tena waombe msaada wa kifedha kutoka kwa wabunge hawa wa viti maalum ili kuimarisha mapambano. Umenisoma?
 

Mama Aron nimekupata sana sikuwa na shaka na ulichomaanisha toka mwanzo. Mchakato mzima kwetu ni haramu, kwa hiyo hata hizo kura chache kwetu ni sehemu ya hilo zoezi haramu. Kitendo chochote cha kwenda kushiriki ni kuhalalisha huo uharamia. Kitendo cha kushiriki ni kukubaliana na mchakato mzima, hakuna nafasi yoyote ya kufafanua hilo kwa wananchi huku nje, ndio itakuwa ndani ya hilo bunge kibogoyo? Ukiniambia unashauri wakale hela hapo sawa, sio kwa hizo sababu zako nzuri.
 
Kwa serikali hii bunge + mahakama + serikali = SERIKALI.

Kwani walitumbia wenyewe A + B + C = C pia

C + A + B = A mwisho A + C + B = B

Hence A = B = C.
 
Mama Amon, theories huwa zinakinzana dada, sijaamua ktk hili suala nitumie theory gani; hichi wanachofanya Chadema na ACT kinaweza kuwa msaada mkubwa kwa nchi siku zijazo, kuchezea uchaguzi na kura za watu ni hatari kwa amani na mustakabali wa nchi.

Kwa kuzingatia signature yangu wewe uko sahihi na Chadema wako sahihi, nami pia niko sahihi maana "we define things as we are, not as they are".

Vv
 
Unadai "hoja tulishaifunga."
Ilifungwa kwa mujibu wa kikao gani?
Mbona kura za vikao vya Kamati Kuu ya Chadema haziungi mkono unachokisema?
Fanya utafiti kwanza.
No reserach no right to speak.

Wao cdm kama chama waamue watakacho, lakini sisi wafuasi wao tuko wazi kwamba hatukubali washiriki kuhalalisha haramu. Wanaweza kupambana kusaka faida za muda mfupi, lakini wasitegemee tena sisi kujitokeza kupiga kura. Wabaki huku nje tudai tume huru ya uchaguzi na katiba mpya. Haya ni madai halali, na sioni yakipatikana kwa hivyo viti 19 kwenda bungeni. Sio lazima msimamo huu uwe bora, lakini ndio msimamo sahihi kwa mazingira haya.
 
Mchakato mzima kwetu ni haramu, kwa hiyo hata hizo kura chache kwetu ni sehemu ya hilo zoezi haramu.
Hapa ndipo nimepata kujua kwa nini tunapishana. Kuna mawili:

1. Mtazamo wangu ni kwamba, hizo kura chache zilizotangazwa na NEC ni halali, wakati zile kura nyingi zinazodaiwa kuhamishiwa upande mwingine ni haramu.

2. Lakini, wewe unasema kuwa, kwa vile mchakato mzima ni haramu, na kwa kuwa hizo kura chache ni sehemu ya mchakato haramu, basi hata hizo kura kidogo ni haramu.

Lakini, huoni kuwa mantiki ya samaki mmoja akioza wote wameoza haikubaliki kimantiki na kisheria?



 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…