Uchaguzi 2020 Tathmini yangu juu ya Uchaguzi Mkuu 2020: Hakuna sababu nzuri ya kukataa kuteua wabunge wa Viti Maalum CHADEMA

1. Asilimia 88 ya mawakala wa CHADEMA walizuiwa/ kutolewa vituoni kabla na baada ya zoezi la kupiga kura.

2. CHADEMA nchi nzima hawakupata nakala za matokeo ya uchaguzi kutokana na mawakala kukatazwa kuingia vituoni au kufukuzwa vituoni hivyo hizo kura X/Y or Z hazifahamiki zipi ni halali na zipi si halali.

3. Wakati wa kuhesabu kura vituo vilivamiwa na maafisa wa polisi kwa kujaza kura zilizokuwa kwenye mabegi na sehemu zingine fomu za matokeo zilijazwa namba tu bila kuzingatia idadi hata ya wapiga kura kwenye kituo husika.

4. Wasimamizi wa uchaguzi kwenye vituo kadhaa waliingia na kura kwenye mabegi zikiwa zimejazwa kwa mgombea wa chama tawala.

5. CHADEMA wanahoji uhalali wa kura zilizotangazwa kwa kuzingatia swali kuwa ni zipi kati ya zilizokuwa kwenye mabegi ya wasimamizi wa uchaguzi au zilizopigwa na wananchi ?

6. Kama CHADEMA hawakuwa na wakala vituoni wakati wa kuhesabu kura je kura halali za kwao ni zipi alizopata mgombea wa ccm au walizopewa wao na tume nani anauthibitisho kuwa ni za kwao wakati hawakuwa na mtazamaji vituoni ?

Kwa kuzingatia kuwa uchaguzi ni mchakato na unahalalishwa na uwazi na haki katika hatua zote msingi wa CHADEMA kukataa kuchagua wabunge wa viti maalumu ni " Mchakato mzima wa kupiga kura na kuhesabu kura" kuwa haukufuata sheria na uligubikwa na mambo ambayo yaliondoa uhalali wa mchakato wenyewe na matokeo ya mchakato.
Hoja ya CHADEMA siyo idadi ya kura ila ni mchakato mzima wa upigaji kura.
 

Mosi, hoja ya kudai Katiba, Tume Huru nk, kwa upande mmoja, na hoja ya kutuma wabunge wa viti maalum bungeni, kwa upande mwingine, ni hoja mbili tofauti.

Pili, kupeleka wabunge wa viti maalum sio kikwazo kwa hoja ya kwanza.

Na tatu, chama kinaendeshwa kwa vikao.

Wananchi walioko nje ya vikao wanapaswa kuonyesha utii kwa maamuzi halali.

Hata viongozi walio kwenye vikao pia wanapaswa kuongozwa na katiba na kanuni, na sio mihemuko.
 

Najua mengi kati ya haya uliyoyaandika.

Lakini, nashauri kutofautisha maembe na machungwa.

Pia nashauri kujiepusha na mantiki ya samaki mmoja akioza wote wameoza.

Turudi kwenye hoja yetu:

Kura za Chadema zilizotangazwa na NEC ni kidogo kuliko uhalisia au ni nyingi zaidi ya uhalisia?

Kama ni kidogo kuliko uhalisia, ni kura halali au kura haramu?

Kama ni kura halali, kwa nini wabunge wa viti maalum wanaotokana na kura hizo wawe haramu?

Nashauri tupeleke wabunge, halafu tuendelee kupigania masuala mengine.

Hakuna athari.
 

Kwenye hili kila mmoja ana utashi wake, sio lazima kwenye msimamo wangu niwe sahihi, lakini nitakuwa mjinga kuacha ninachoamini, niamini unachoamini ww hata kama sikiamini.
 
Kwenye hili kila mmoja ana utashi wake, sio lazima kwenye msimamo wangu niwe sahihi, lakini nitakuwa mjinga kuacha ninachoamini, niamini unachoamini ww hata kama sikiamini.

Self-imposed irationality aside, lengo la kujenga hoja ni kubadilisha imani ya msikilizaji kwa kutumia nguvu ya ushahidi.

Kwa hiyo, nakualika ukapime uzito wa ushahidi katika hoja zangu.

Kama ukishawishika, sio dhambi kubadili imani yako ya sasa.
 
Pengine hoja yako wangeielewa zaidi kama ungewapa maarifa ya namna ya "kukomboa" hizo kura ambazo wanasema ziliibwa.Je wanazikomboaje? maana mfano wa madai kati ya mwajiri na mwajiriwa ambao umeutoa naona ,kwa mawazo yangu,hausadifu kwenye hoja hii.
 
Tujielekeze kwenye hoja.
Tusitoke nje ya mstari.
Achana na hayo mambo madogo.
Jibu lako hili nalifananisha na jibu la mbunge mmoja alipofuatwa na mpiga kura wake alipohoji mambo ya maendeleo mpiga kura akaambiwa achana na siasa wewe kunywa pombe.
 
Pengine hoja yako wangeielewa zaidi kama ungewapa maarifa ya namna ya "kukomboa" hizo kura ambazo wanasema ziliibwa.Je wanazikomboaje? maana mfano wa madai kati ya mwajiri na mwajiriwa ambao umeutoa naona ,kwa mawazo yangu,hausadifu kwenye hoja hii.

Hoja yangu ni rahisi sana.

Haina uhusiano na zoezi la kutafuta kura zinazodaiwa kuibiwa.

Mimi naongelea zile kura chache, ambazo kwa mtazamo wangu, ni kura halali.

Na mfano wangu wa mwajiri na mwajiriwa unafaa katika mipaka hiyo.

Kuhusu kura zinazodaiwa kuibwa kuna nadharia nyingi.

Baadhi ya nadharia ni dhaifu mno.

Nadharia nyingine zina uzito.

Lakini, niseme wazi: mpaka sasa hakuna nadharia ambayo nimeisikia ikitajwa inayoweza kuzalisha ushahidi wa kimahakama unaoweza kusaidia "kukomboa" hizo kura zinazodaiwa kuibiwa.

Lakini, hii sio hoja yangu kwa leo.
 
Jibu lako hili nalifananisha na jibu la mbunge mmoja alipofuatwa na mpiga kura wake alipohoji mambo ya maendeleo mpiga kura akaambiwa achana na siasa wewe kunywa pombe.

Hata hujaelewa nilichosema.
KUna mtu alijaribu kukuondoa kwenye mada.
Ukaanza kuongelea mleta mada badala ya mada ya bandiko hili.
Hivyo tu.
Usiende mbali.
 
Pili hoja yako ya mgogoro wa Mwajiri na mwajiriwa ni irrelevant kwenye hoja yako ya kura za CHADEMA kwa sababu mwajiriwa ana njia ya kutafuta haki yake wakati CHADEMA hawana tena hiyo Avenue
 
Hata hujaelewa nilichosema.
KUna mtu alijaribu kukuondoa kwenye mada.
Ukaanza kuongelea mleta mada badala ya mada ya bandiko hili.
Hivyo tu.
Usiende mbali.
Umemjibu mtu tofauti na mimi probably
 
Pamoja na maelezo yako marefu, kindendo cha kutojua kwamba wabunge wa viti maalumu wanatokana na jumla ya kura za wabunge wa chama husika na badala yake wewe ukaona wanatokana na jumla ya kura alizopata mgombea wa chama husika, hapo tu tayari hoja yako nzima ni "null and void"

Tafuta hoja nyingine uje nayo.
 
Sioni hoja katiba mpya ikijadiliwa bungeni. Kwenda bungeni ni kuhalalisha uhuni, hilo halibadiliki.

Hatuko tayari kuheshimu maamuzi ya vikao ambayo yatakuwa yanabariki chaguzi za kihuni. Vikao vinapaswa kuheshimu Misimamo yetu wafuasi wao. Tulikaa kimya tukaishia kuletewa Lowasa kwa maamuzi ya vodafasta. Tunaangalia mustakabali wa chaguzi ambazo maamuzi yetu ya kuchagua yataheshimiwa, na sio chaguzi za kihuni zifanyike kisha tuendelee kushiriki kwenye mabunge ya hivyo. Kuliko waende bungeni, bora waende mahakamani kudai kura za wabunge na madiwani zihesabiwe upya, hapo tutawaunga mkono.
 
Kwa hali ilivyo kura halali hazifahamiki ni zipi na majibu nimetoa pale juu.

CHADEMA hawahoji upungufu wa kura au wingi wa kura wanahoji uhalali wa kura zenyewe kutokana na zoezi la kupiga kura kufanyia katika mchakato batili.
 

Sorry, unaandika kama vile unadondosha maneno ambayo yanakosa muunganiko wa kimantiki.

Can you paraphrase your argument to make it more formal and palatable?

napendelea hoja zenye muundo haka huu:

Tindo ni mtu (major premise)
KIla mtu atakufa (minor premise)
Kwa hiyo, siku moja, Tindo atakufa (conclusion)

Katika muundo huu inakuwa rahisi kufuatilia anachosema mwenzako.
 
Hakuna atakayemfukuza, na ushauri huo tumeutoa kwa chama, yeye aendelee na wajibu wake lakini ajue fika hatuafiki mchakato huu wa kishenzi. Ni juu yake kusaka maisha ya familia yake, ila sisi tunaangalia mustakabali wa chama.
Hilo ndilo neno kwani uchaguzi umekwisha na waliochaguliwa wameapa wakiendelea kuwajibika kwa wapiga kura. Kinachohitajika ni kwa viongozi wa upinzani, nanyi wafuasi, kutathmini, kwa kina, makosa yaliyofanyika kiasi cha kufanya vibaya SANA kweye Uchaguzi uliomalizika.

Kadiri viongozi wa upinzani, hasa CHADEMA, nanyi wafuasi, mnavyoendelea kulalamikia matokeo na kuilamu NEC, ndivyo mnavyowapa morali viongozi wa CCM kuisimamia vizuri Serikali yake ili Ilani ya Uchaguzi itekelezwe ipasavyo. Na utekelezaji ukifanikiwa, ni wazi Uchaguzi Mkuu, 2025, upinzani usahau kupata hata kata moja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…