Tatizo la kununua Umeme wa LUKU: Waziri Kalemani amsimamisha kazi kwa siku 10 Meneja wa TEHAMA wa TANESCO

Nanunua luku ya kudumu muda mrefu.. sipendi nunua nunua ya kila mara.. nimekomboleka hapo..

Poleni..
Umekomboka vipi.kudumu mrefu maana yake nini. ungesema haina kikomo.ya muda itakwisha tu na unaweza kununua siku mitambo imelala kama wakati huu. jiongeze
 
Navyoona Mimi amekurupuka kwa kuwasimamisha bila ya ku solve kwanza tatizo.
Hao waliosimamishwa huenda ndo key players na Wana Access katika Manipulation za Database za mtandao mzima.
Ni vizuri angewaacha wafanye kazi watoe incident Report,halafu ndo awasimamishe.
Pamoja na hayo lazima kuwe na Backup plan endapo kukitokea tatizo Kama hili "Backup Plan "iko Automated.
Kitengo Cha Programing na Electronic Team nzima lazima iwe na Utaalamu ambao ni "Asymetrical"mfano akiondoka A1,A2 anaweza ku manipulate sawasawa na A1.
Suala la kuwasimamisha kazi bila tatizo kutatuliwa naona Muheshimiwa kalichukulia hasira na kisiasa na Kama binadamu na kiongozi hakuna jinsi ambapo angeweza ku strike balance bila kufanya hivyo.
Hawa wakitoa technical Reasons zozote wakarudishwa kazini Basi kimantiki Mheshimiwa Waziri ataonekana Ni mwenye maamuzi ya jazba ,wakati namjua Ni msomi kwa kushuka chini kwa level hiyo
 
Kwa nini waziri anafanya kazi ya Mtendaji Mkuu? Anasimamishaje watu kabla ya kufanya uchunguzi? Na wakishindwa kurudisha katika muda aliotoa atawafanya nini? Au wakirudisha lakini wakasababisha madhara mengine atakubali kuwajibika?

Amandla...
 
Kusimamishwa kazi siku 10 maana yake nini?

Mshahara wake utakatwa hizo siku ambazo hajafanya kazi au inakuaje? Ni kama vile kapewa mapumziko
Hii hata mimi sijawahi kuisikia mtu anahusishwa na hujuma anasimamishwa siku 10?hapa kuna namna mama anatakiwa afanye anazidiwa kete hapa ahtuke mapema usalama wa taifa tunawategemea sana kwa sana
 
Sasa hivi watu wanajiamini.
 
ina maana hawakuwa na backup kweli ni uzembe wa juu kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…