Hua nasema kila siku humu.
Mbowe, Lipumba, Zitto wanadhooficha harakati za demokrasia nchi hii.
Haiwezekani chadema wasitengeneze succession plan ya mtu mwingine mwenye uwezo kumrithi Mbowe halafu wanataka tuwakabidhi nchi yetu, hivi si watabadili katiba watawale milele?
Zitto amejipa cheo cha juu ambacho hakipigiwi kura, eti kiongozi mkuu wa chama na mshauri mkuu wa chama. Hataki uchaguzi, hapo anataka uchaguzi huru kwenye nchi huku yeye hauonyeshi huo uhuru kwenye chama chake.
Wapinzani wa nchi hii ndio wanaua demokrasia. Demokrasia wanaiongea mdomoni lakini mioyoni mwao ni madikteta wakubwa, hawataki upinzani kwenye chama, hawataki uchaguzi kwenye vyama na hata wakifanya uchaguzi ni geresha tu ila wao wako pale pale.
Hivi wao demokrasia ni uchaguzi mkuu wao washinde ila kwenye vyama hakuna demokrasia?
Vyama vya siasa Tanzania ni family party, sio political party. Vinatumika kwa maslahi ya viongozi wake. Zitto anaitumia ACT kwa maslahi yake, Chadema Mbowe anaitumia kwa maslahi yake.
Nchi hii CCM majanga, upinzani vimeo.