Tatizo la kurudiwa kutangazwa kwa nafasi za kazi za Assistant Lecturers

Ungekua sio mjinga ungeenda kusoma hiyo masters ili upate hiyo kazi.
Ni kipi kimekufanya usiende hiyo masters kama sio ujinga PROMAX.
Usiwadharau vijana 😀😀😀
 
Ungekua sio mjinga ungeenda kusoma hiyo masters ili upate hiyo kazi.
Ni kipi kimekufanya usiende hiyo masters kama sio ujinga PROMAX.
Usiwadharau vijana 😀😀😀
We unajua elimu yangu?! Na unajua professional yangu?! 😃 ndo mana nasemaga vijana wa kiafrika hasa afrika mashariki mmejawa na jeuri, ujuaji na ujinga ujinga mwingi! Kalagabaho masalakulangwa wewe!
 
Unapresent kama utakavyokuwa unafundisha.
Yaani kivp hapa ? Mwifwa ...kwa hyo ukiingia kwny presentation ukapresnt Kama unapresent research inaweza kula kwako au ?? Au unavaa uhusika wa teaching demonstration,, like unawauliza maswali ,?
 
Unapresent kama utakavyokuwa unafundisha.
Sasa mwanangu Mwifwa panel itakupimaje uwezo wako wa kumiliki darasa ( class management) au wakt unapresent utajuaje Kama hapa unaonesha uwezo wa kulimiliki darasa ,,au ndio kuangalia vimitego wanakuwekea panel au hakunaga vimitego kweny presentation Nini? mfn. Wanaongea panel au hawako serious kukusikiliza WANAFANYA yao labda kulala au kuchezea simu ? Kwa hyo utatakiwa kuwanyamazisha Kama wanaongea au utawaacha ??? Au WANAFANYA mambo zao hutawastopisha au utaendelea na pindi lako?
Tusaidiane maoni Mwifwa na tuulizie kwa wengne
 
Halaf kweny presentation unatakiwa kuprisent ka unapresent research au unafundisha kabisa KUNA TOFAUTI YA PRESENTATION NA TEACHING DEMONSTRATION???
Kama walivyoeleza wenzangu hapo juu. UNAFUNDISHA na si vinginevyo.

Unachagua topic yoyote ambayo iko kwenye kada husika, kisha unalifundisha jopo (wao ndio wanakua wanafunzi wako kwa wakati huo).

Fikiria mlivyokua mnafundishwa MAGAZIJUTO, Hesabu za hasi na chanya, colonial economy, human rights, historia ya lugha, n.k na walimu wenu, nawewe utakua ukifanya hivyo. (Kwa njia zinazotumika vyuoni lakini, mambo ya projekta)
 
Degree ikiangiaga 3.5 anaweza kuwa Lecturer. Ila uaminif wa malekcha na wakupende tu. Mbon udsm malekcha wa 3. 5 Degree wapo
 
Naomba nikujibu kuhusu kulimudu darasa. Class handling.

Nitaanzia mbali kidogo.
Wanapomtafuta mtu wa kufundisha, wanaangalia mambo mengi. Wanaangalia contents (je, vitu kichwani vimo), wanaangalia uwezo na maarifa ya kuvifikisha (hivyo vitu) kwa wengine pamoja na mbinu zingine za kiufundishaji (pedagogical skills).

Hayo wanaweza kuya assess kupitia namna unavyofundisha au kwa kupitia aina fulani ya maswali ambayo watakuuliza. (Kumbuka kuna maswali yanayohusiana na ulichofundisha ili ku assess kama una contents, na maswali mengine ambayo yana assess mambo mengine).

Turudi kwenye swali lako. Kulimudu darasa.
Kwa kifupi, kulimudu darasa ni mjumuisho wa mambo yote yatakayofanyika ili kulifanya darasa liwe katika mazingira mazuri ya wanafunzi kujifunza. Hii inajumuisha utulivu, utaratibu, n.k.

Msimamizi mkuu wa haya (wakati wa ufundishaji) ni mwalimu.

Namna ambayo wanaweza kuitumia ku assess uwezo wako wa kulimudu darasa.
Zipo njia nyingi, ila miongoni mwao ni;-
Kama unafundisha kwa sauti ndogo. Wao watajiuliza sasa huyu mtu atawezaje kulimudu darasa zima kwa hiki kisauti kidogo namna hii. Ni lazima usikike ili darasa lijue ni nini unafundisha.

Unaweza kuulizwa, je, wewe kama mwalimu na upo darasani unafundisha, wakati huo nusu ya wanafunzi wako wanachezea simu zao. Utafanya nini ?

Yapo mambo mengi, naishia hapo nikiamini angalau umepata idea juu ya hoja yako.
 
Degree ikiangiaga 3.5 anaweza kuwa Lecturer. Ila uaminif wa malekcha na wakupende tu. Mbon udsm malekcha wa 3. 5 Degree wapo
Una uhakika juu ya hili la wakufunzi wenye GPA ya 3.5 (undergraduate) kuwapo UDSM mkuu ?

Sera ya chuo katika kuajiri watumishi wa kitaaluma inaitaja GPA ya 3.8 kama kiwango cha chini cha ufaulu. Sisi tunaiamini hii.
Ili utuaminishe vinginevyo, kwamba wapo wenye 3.5, unatakiwa kuja na "very good evidence".
Tunazisubiri hapa.
Karibu
 
Yaani kivp hapa ? Mwifwa ...kwa hyo ukiingia kwny presentation ukapresnt Kama unapresent research inaweza kula kwako au ?? Au unavaa uhusika wa teaching demonstration,, like unawauliza maswali ,?
Uwasilishaji wa kufundisha, lengo kuu kuhamisha maarifa ukiyonayo kwenda kwa wasikilizaji(wanaotafuta hayo maarifa).

Kuwasilisha utafiti huwa ni kuwasilisha majibu ya utafiti, unawasilisha kile ulichokibaini kwenye utafiti.

Hadi hapo si umeona utofauti wa kufundisha na kutoa majibu ya utafiti?
 
Hayo maswali unayouliza ni NDIO.

Sasa utakuwaje mwalimu/mkufunzi mzuri usipoweza kumiliki darasa?

Watu walale, wachati, wapige stori badala ya kukusikiliza uwaache tu?

Hapana, hapo inabidi uoneshe uwezo na mbinu za kukabiliana na hiyo changamoto. Unaweza ukawa unafundisha watu wakawa hawaelewi mwisho wa siku wakaishia kusinzia, sasa utatumia mbinu gani waelewe? hapa ndio skills zinahitajika. Utafanyaje watu wakusikilize na wasipige stori? hapa ushawishi mbele ya hadhira unahitajika ili wakupe attention ya kukusikiliza.

Ahmet sema neno hapa, wewe ushapiga presentation za usahili
 
Halaf kweny presentation unatakiwa kuprisent ka unapresent research au unafundisha kabisa KUNA TOFAUTI YA PRESENTATION NA TEACHING DEMONSTRATION???
Huu mwandiko mbovu kama una ufaulu wa kufanya usahili uko. Mwandiko level ya kidato cha tatu
 
Wakuu kwema, samahani hivi kama ulifanya oral ya kuwa let's say TA na kwa bahati mbaya ukakosa nafasi then ukakaa kwenye database, je unaweza kupata kazi katika fani nyengine kama warden, examination officer, register nk kama unafit hizo sehemu au mpka ipatikane post kama ileile ulioombea??
Mwongozo tafadhari
 
Sometimes wanakupa muda mchache kama dakika Tano tu, kwaiyo inabidi uwe short and clear, try to use examples
 

Kanzidata ya TA sijasikia mtu aseme amepata nafasi kwa kukaa huko.

Kada ni sawa, kinachomatter ni Qualification tu, kama Warden, Exam officer n.k wanataka sifa moja basi ukiwa na hiyo sifa halafu upo kanzidata, basi utapata nafasi
 
Kanzidata ya TA sijasikia mtu aseme amepata nafasi kwa kukaa huko.

Kada ni sawa, kinachomatter ni Qualification tu, kama Warden, Exam officer n.k wanataka sifa moja basi ukiwa na hiyo sifa halafu upo kanzidata, basi utapata nafasi
Ahaa sawa nimekupata kaka
 
Nazani kanzidata ipo ,,ikitokea umekosa NAFASI ya kuwa TA ,,lkn si unataakuma fulan unaweza tokea NAFASI inataka taaluma yako ,na Upo kweny kanzidata ulifanya vzr si unaweza pata NAFASI ,,lkn mfn ulifanya vzr lkn nafasi Zilikuwa chache akapata mwingine,,ikitokea wanataka kuongeza mtu ndani ya miezi 6 na ww Upo si watakuchukua Ahmet
 
@Ahmet tusaidie uzoefu wa presentation za TA katka kumiliki darasa ..kwa mtazamo wako Nia ni kujifunza na kuwasaidia wengne
 
Bro Mwanamaji nimepata madini ambayo natamani niendelee kukuuliza ili niendelee kujifunza vitu ...naona maelezo mazuri sana kk ..[emoji122][emoji122]
 
Huyo jamaa nazni alikuwa anaongelea TA wa Institutes ambao wanataka minimum GPA 3.5 ILA kwa vyuo vikuu minimum ni 3.8 GPA
 
K
Kanzidata ya TA sijasikia mtu aseme amepata nafasi kwa kukaa huko.

Kada ni sawa, kinachomatter ni Qualification tu, kama Warden, Exam officer n.k wanataka sifa moja basi ukiwa na hiyo sifa halafu upo kanzidata, basi utapata nafasi
Kanzidata ipo mkuu hujasikia ni kwa sababu zilikua hazitangazwi na utumishi mwaka huu ndo wamezimwaga sana kwaiyo kanzidata lazima iwepo mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…