Tatizo la vijana waliosomea mafuta na gesi kuzagaa mtaani wakati kila siku tunasikia miradi ya mafuta na gesi inazungumziwa na Serikali

Hilo ni moja lakini la pili, ni kwamba kuna mahali tunakwama kama nchi,
Jiulize ni kwa nini kila uchao serikali inaongeza mamlaka ambazo wafanyakazi wake wanalipwa pesa
kubwa tofauti na sekita nyingine za serikali/umma zilizokuwepo tangu enzi ya uhuru?
Mfano: Zamani tulikuwa na Sumatra,imegawanyika na kuzaa Latra,EWURA imezaa PURA,tuna mamlaka ya hali ya hewa,tuna mamalaka ya mawasiliano TCRA,Mamlaka ya mapato TRA na nyingine unazozijua
sasa fanya homework yako tafuta mishahara yao,ilinganishe na ya watumishi wengine wa umma.

Ukiishapata jibu hutashangaa kuona vijana wanahitimu kwenye fani muhimu kama hiyo ya mafuta na gesi
na bado wanaishia kulanda landa mitaani.
Maswali ukiwa nje ya system yanakuwa mengi ila ukiingia ndani
mnato wa asali unakufanya ushindwe kutikisa mbawa .na wewe unaanza kuomola kwa meno
na ukinogewa na maneno mdomoni unaishiwa unabaki kukodoa jicho ukiwa kwenye gari lenye kiyoyozi.
 
Vijana wewe na extra soft skills za kuwasaidia endapo changamoto za ajira zinapotokea.ni fikra potofu kusoma ili kuajiriwa ni lazima vijana watafute njia mbadala endapo wakikosa ajira mfano ujasiliamali, uandishi sanaa kilimo nk
Kumwambia muhitimu aliyehitimu kozi km petroleum and gas,biotechnology,molecular biology na microbiology kujikita kwenye sanaa na uandishi ni waste of knowledge hawa jamaa wanatakiwa wapewe sapoti na kipaumbele kama taifa tuweze kunufaika na taaluma zao...
 
Ajila× ni Ajira✓
 
Tunawahitaji sana hao watu ila tunakosa mifumo ya kuwatumia mwisho wa siku wanasotea mitaan.. mwisho wa siku tunazalisha kizazi cha wasomi wavuta bangi na walevi sababu ya stress na depression
 
Hapo kwenye ualimu nako changamoto kwa sasa, inategemea ualimu kasomea nini, labda masomo ya sayansi
Sayansi kwenyewe napo moto unawaka labda asomee physics na math ila kemia na biology wimbo ule ule na wana art..

Ajabu ni kwamba nchi still ina uhaba wa walimu lakin haitaki kuajili hahah
 
Ila kusema ukweli hii fani kwanza ni ngumu,pili sehemu za kuajiliwa hapa nchini ni chache,
Serikali ifanye maamuzi ya kila msomi awe na ruhusa ya kupewa hati ya kusafiria bila vikwazo.
Kuna swali moja pale uhamiaji,huwa linaniudhi sana ukienda kuomba hati ya kusafiria.
Unaulizwa eti unaenda wapi?
Huwa najiuliza,je hapa nchi ni gereza? kama siyo gereza wenye uwezo wa kwenda kusaka ajira nje ya nchi waruhusiwe
watumie visomo vyao kupata ajira huko nje,wanufaike na kuinufaisha nchi.
 
Thinking yako ni ya Industrial Revolution Age! Tuko kwenye Information Age!
Mnaosoma ili mkaajiriwe kwenye miradi ya Serikali mmepitwa na wakati!
Kuna wenzenu darasa la saba wamejiongeza wanauza petrol na diesel vijijini kwenye shughuli za kilimo na migodi!
Ukipita njia inayotoka Kahama hadi Masumbwe kuna madumu yamening'inizwa maporini kuashiria biashara ya "kupiga nyoka" katika magari yaendayo Rwanda na Burundi inafanyika!
Jitu lina degree ya petroleum na gas linapiga miayo mtaani hata mia halina!
Elimu ya kijinga ya kukariri theories ( tena mengi yanatamka seori)!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…