Tatizo la vijana waliosomea mafuta na gesi kuzagaa mtaani wakati kila siku tunasikia miradi ya mafuta na gesi inazungumziwa na Serikali

Tatizo la vijana waliosomea mafuta na gesi kuzagaa mtaani wakati kila siku tunasikia miradi ya mafuta na gesi inazungumziwa na Serikali

Nimeona hili leo niliseme pengine viongozi wetu hawalifahamu swala hili:

Kweli kumekua na tatizo la vijana wetu waliosomea fani za mafuta na gesi kuzagaa mtaani tangu fani hizi zilipo anzishwa mwaka 2013. Asilimia 80 ya vijana waliosomea fani hizo hawaja ajiriwa mpaka sasa. Na walianza kuhitimu mwaka 2016.

Vijana wanahitimu lakini nafasi za kazi zinazotoka haziendani na idadi ya wahitimu.

Kila siku tunasikia miradi ya mafuta na gesi inazungumziwa lakini vijana hawa wa mafuta na gesi hawapati nafasi ya kwenye miradi hiyo.

Makampuni yetu ya serikali yakitangaza nafasi, zinazowahusu vijana wa mafuta na gesi zinakua ni chache sana hata kumi hazifiki.

Vijana wanazidi kuzeeka mtaani hawana pakujishikiza.

Viongozi wetu wanapaswa kuwatazama hawa vijana wa mafuta na gesi. Wengi wanajikatia tamaa kabisa hasa wanaposikia miradi inatangazwa kila siku ila ajira zinazotolewa na hiyo miradi hazihusu fani za mafuta na gesi.

Jamani jamani ni kweli keki ya mafuta na gesi ni tamu kiasi kwamba watu hupenda kung'ang'aniana lakini tunapaswa kuwapa ajira zao vijana hawa. Ajira zipo kote sekta binafsi na serikalini ila vijana hawa wanatengwa.

Serikali ingefanya jambo katika swala hili.

Mpaka nikawa najiuliza maswali ni kitu gani kinashindikana kuwaajiri vijana hawa. Walau ajira zilingane na idadi ya wanao hitimu kwasababu miradi tunaiskia kila siku.

Tuna mradi wa Helium. Na mingine mingi tu ya gesi na mafuta. Hivi ni kitu gani kinashindikana kuwakusanya hawa vijana wote wa mafuta na gesi na kuwatupia kwenye hiyo miradi.

Lakini wakati mwingine ikionekana fani zimeshakua na idadi kubwa ya wahitimu, pia ni jambo jema kuzibadilisha fani hizo ili ziendane na soko la ajira.

Ahsante sana
Hilo ni moja lakini la pili, ni kwamba kuna mahali tunakwama kama nchi,
Jiulize ni kwa nini kila uchao serikali inaongeza mamlaka ambazo wafanyakazi wake wanalipwa pesa
kubwa tofauti na sekita nyingine za serikali/umma zilizokuwepo tangu enzi ya uhuru?
Mfano: Zamani tulikuwa na Sumatra,imegawanyika na kuzaa Latra,EWURA imezaa PURA,tuna mamlaka ya hali ya hewa,tuna mamalaka ya mawasiliano TCRA,Mamlaka ya mapato TRA na nyingine unazozijua
sasa fanya homework yako tafuta mishahara yao,ilinganishe na ya watumishi wengine wa umma.

Ukiishapata jibu hutashangaa kuona vijana wanahitimu kwenye fani muhimu kama hiyo ya mafuta na gesi
na bado wanaishia kulanda landa mitaani.
Maswali ukiwa nje ya system yanakuwa mengi ila ukiingia ndani
mnato wa asali unakufanya ushindwe kutikisa mbawa .na wewe unaanza kuomola kwa meno
na ukinogewa na maneno mdomoni unaishiwa unabaki kukodoa jicho ukiwa kwenye gari lenye kiyoyozi.
 
Vijana wewe na extra soft skills za kuwasaidia endapo changamoto za ajira zinapotokea.ni fikra potofu kusoma ili kuajiriwa ni lazima vijana watafute njia mbadala endapo wakikosa ajira mfano ujasiliamali, uandishi sanaa kilimo nk
Kumwambia muhitimu aliyehitimu kozi km petroleum and gas,biotechnology,molecular biology na microbiology kujikita kwenye sanaa na uandishi ni waste of knowledge hawa jamaa wanatakiwa wapewe sapoti na kipaumbele kama taifa tuweze kunufaika na taaluma zao...
 
Nitoshe kusema ewe kijana ambaye hujaenda chuo.....kabla ya kuapply fani fanya uchunguzi kwanza sio unaapply kwa kufuata mkondo.....!! Fani nzur kwa sasa ni
1) ualimu wa awali shule ya msingi
Naweza sema hii ndio top inayohit kwa sasa mana serikal inawahitaji hawa kila shule na ni koz iliyoanzishwa mwaka juz watu wanakula ajila kaz yako kucheza na watoto wa chekechea mpunga unaingia hafu hauna daftar za kusahihisha...pia waweza kujiajil kwa kuanzisha day care center ambazo kwa sasa zinalipa kutokana na watu kutokuwa na muda wa kuwalea watoto wao
2)Fani za kompyuta(all field)
Now tunaenda ulimwengu wa kidgtal tunahitaji wataaalamu weng wa kompyuta na hata serikal inampango wa kuanzisha koz za kompyuta kuanzia shule za msing na sekondar na uzur vtabu vya ICT vimeshapokelewa na mashule wanaosubiriwa wataalamu...Hii pia unajiajil kama web developer na hata kutengeneza app janja kwa ajil ya kukuongezea kipato...!!
All in all aliyesomea field inayohusiana na kompyuta hafu akalalamika amekosa ajila ntamshangaa sana...!
3) Mechanical engineering(field zote)...Nayo iko poa mana waweza kujiajil na kupata kipato....!! Watu wanazid kununua magar basi nawale wanaotengeneza wanatakiwa sana na hii kaz inaapply kwenye viwanda vyote unavyovjua lazma mechanical engineer wapo..!
NB
Kama nngepata muda wa kuchagua now nngesoma mojawapo ya hiz koz hasa compyuta
Ajila× ni Ajira✓
 
Nina mdogo wangu amemaliza mwaka huu shahada hii ya petroleum engineering pengine hii mada inanihusu sana. Ni miongoni mwa wale vijana bright kabisa division 1 point 4 form six aliyechaguliwa kusoma shahada hii selective pale mlimani.

Tunajenga nchi moja ya kijinga sana kuwaacha vijana wetu bora kabisa kusota mtaani. Nafikiri kama mzazi inabidi kumwandaa kijana wako kutopoteza muda na degree za wanasiasa bali mfundishe mapema stadi za maisha ikiwemo kilimo, biashara na ufundi mbalimbali.
Tunawahitaji sana hao watu ila tunakosa mifumo ya kuwatumia mwisho wa siku wanasotea mitaan.. mwisho wa siku tunazalisha kizazi cha wasomi wavuta bangi na walevi sababu ya stress na depression
 
Hapo kwenye ualimu nako changamoto kwa sasa, inategemea ualimu kasomea nini, labda masomo ya sayansi
Sayansi kwenyewe napo moto unawaka labda asomee physics na math ila kemia na biology wimbo ule ule na wana art..

Ajabu ni kwamba nchi still ina uhaba wa walimu lakin haitaki kuajili hahah
 
Ila kusema ukweli hii fani kwanza ni ngumu,pili sehemu za kuajiliwa hapa nchini ni chache,
Serikali ifanye maamuzi ya kila msomi awe na ruhusa ya kupewa hati ya kusafiria bila vikwazo.
Kuna swali moja pale uhamiaji,huwa linaniudhi sana ukienda kuomba hati ya kusafiria.
Unaulizwa eti unaenda wapi?
Huwa najiuliza,je hapa nchi ni gereza? kama siyo gereza wenye uwezo wa kwenda kusaka ajira nje ya nchi waruhusiwe
watumie visomo vyao kupata ajira huko nje,wanufaike na kuinufaisha nchi.
 
Attachments

  • Screenshot_20221031-195845_Chrome.jpg
    Screenshot_20221031-195845_Chrome.jpg
    111.2 KB · Views: 9
Nimeona hili leo niliseme pengine viongozi wetu hawalifahamu swala hili:

Kweli kumekua na tatizo la vijana wetu waliosomea fani za mafuta na gesi kuzagaa mtaani tangu fani hizi zilipo anzishwa mwaka 2013. Asilimia 80 ya vijana waliosomea fani hizo hawaja ajiriwa mpaka sasa. Na walianza kuhitimu mwaka 2016.

Vijana wanahitimu lakini nafasi za kazi zinazotoka haziendani na idadi ya wahitimu.

Kila siku tunasikia miradi ya mafuta na gesi inazungumziwa lakini vijana hawa wa mafuta na gesi hawapati nafasi ya kwenye miradi hiyo.

Makampuni yetu ya serikali yakitangaza nafasi, zinazowahusu vijana wa mafuta na gesi zinakua ni chache sana hata kumi hazifiki.

Vijana wanazidi kuzeeka mtaani hawana pakujishikiza.

Viongozi wetu wanapaswa kuwatazama hawa vijana wa mafuta na gesi. Wengi wanajikatia tamaa kabisa hasa wanaposikia miradi inatangazwa kila siku ila ajira zinazotolewa na hiyo miradi hazihusu fani za mafuta na gesi.

Jamani jamani ni kweli keki ya mafuta na gesi ni tamu kiasi kwamba watu hupenda kung'ang'aniana lakini tunapaswa kuwapa ajira zao vijana hawa. Ajira zipo kote sekta binafsi na serikalini ila vijana hawa wanatengwa.

Serikali ingefanya jambo katika swala hili.

Mpaka nikawa najiuliza maswali ni kitu gani kinashindikana kuwaajiri vijana hawa. Walau ajira zilingane na idadi ya wanao hitimu kwasababu miradi tunaiskia kila siku.

Tuna mradi wa Helium. Na mingine mingi tu ya gesi na mafuta. Hivi ni kitu gani kinashindikana kuwakusanya hawa vijana wote wa mafuta na gesi na kuwatupia kwenye hiyo miradi.

Lakini wakati mwingine ikionekana fani zimeshakua na idadi kubwa ya wahitimu, pia ni jambo jema kuzibadilisha fani hizo ili ziendane na soko la ajira.

Ahsante sana
Thinking yako ni ya Industrial Revolution Age! Tuko kwenye Information Age!
Mnaosoma ili mkaajiriwe kwenye miradi ya Serikali mmepitwa na wakati!
Kuna wenzenu darasa la saba wamejiongeza wanauza petrol na diesel vijijini kwenye shughuli za kilimo na migodi!
Ukipita njia inayotoka Kahama hadi Masumbwe kuna madumu yamening'inizwa maporini kuashiria biashara ya "kupiga nyoka" katika magari yaendayo Rwanda na Burundi inafanyika!
Jitu lina degree ya petroleum na gas linapiga miayo mtaani hata mia halina!
Elimu ya kijinga ya kukariri theories ( tena mengi yanatamka seori)!
 
Back
Top Bottom