uchumi2018
JF-Expert Member
- Mar 4, 2018
- 1,657
- 2,406
Hilo ni moja lakini la pili, ni kwamba kuna mahali tunakwama kama nchi,Nimeona hili leo niliseme pengine viongozi wetu hawalifahamu swala hili:
Kweli kumekua na tatizo la vijana wetu waliosomea fani za mafuta na gesi kuzagaa mtaani tangu fani hizi zilipo anzishwa mwaka 2013. Asilimia 80 ya vijana waliosomea fani hizo hawaja ajiriwa mpaka sasa. Na walianza kuhitimu mwaka 2016.
Vijana wanahitimu lakini nafasi za kazi zinazotoka haziendani na idadi ya wahitimu.
Kila siku tunasikia miradi ya mafuta na gesi inazungumziwa lakini vijana hawa wa mafuta na gesi hawapati nafasi ya kwenye miradi hiyo.
Makampuni yetu ya serikali yakitangaza nafasi, zinazowahusu vijana wa mafuta na gesi zinakua ni chache sana hata kumi hazifiki.
Vijana wanazidi kuzeeka mtaani hawana pakujishikiza.
Viongozi wetu wanapaswa kuwatazama hawa vijana wa mafuta na gesi. Wengi wanajikatia tamaa kabisa hasa wanaposikia miradi inatangazwa kila siku ila ajira zinazotolewa na hiyo miradi hazihusu fani za mafuta na gesi.
Jamani jamani ni kweli keki ya mafuta na gesi ni tamu kiasi kwamba watu hupenda kung'ang'aniana lakini tunapaswa kuwapa ajira zao vijana hawa. Ajira zipo kote sekta binafsi na serikalini ila vijana hawa wanatengwa.
Serikali ingefanya jambo katika swala hili.
Mpaka nikawa najiuliza maswali ni kitu gani kinashindikana kuwaajiri vijana hawa. Walau ajira zilingane na idadi ya wanao hitimu kwasababu miradi tunaiskia kila siku.
Tuna mradi wa Helium. Na mingine mingi tu ya gesi na mafuta. Hivi ni kitu gani kinashindikana kuwakusanya hawa vijana wote wa mafuta na gesi na kuwatupia kwenye hiyo miradi.
Lakini wakati mwingine ikionekana fani zimeshakua na idadi kubwa ya wahitimu, pia ni jambo jema kuzibadilisha fani hizo ili ziendane na soko la ajira.
Ahsante sana
Jiulize ni kwa nini kila uchao serikali inaongeza mamlaka ambazo wafanyakazi wake wanalipwa pesa
kubwa tofauti na sekita nyingine za serikali/umma zilizokuwepo tangu enzi ya uhuru?
Mfano: Zamani tulikuwa na Sumatra,imegawanyika na kuzaa Latra,EWURA imezaa PURA,tuna mamlaka ya hali ya hewa,tuna mamalaka ya mawasiliano TCRA,Mamlaka ya mapato TRA na nyingine unazozijua
sasa fanya homework yako tafuta mishahara yao,ilinganishe na ya watumishi wengine wa umma.
Ukiishapata jibu hutashangaa kuona vijana wanahitimu kwenye fani muhimu kama hiyo ya mafuta na gesi
na bado wanaishia kulanda landa mitaani.
Maswali ukiwa nje ya system yanakuwa mengi ila ukiingia ndani
mnato wa asali unakufanya ushindwe kutikisa mbawa .na wewe unaanza kuomola kwa meno
na ukinogewa na maneno mdomoni unaishiwa unabaki kukodoa jicho ukiwa kwenye gari lenye kiyoyozi.