Tatizo la vijana waliosomea mafuta na gesi kuzagaa mtaani wakati kila siku tunasikia miradi ya mafuta na gesi inazungumziwa na Serikali

Seori [emoji3][emoji3] hao watu ndo aina ya mto mada, bure kabisa. Yeye kaona mafuta na gesi tu, unajiuliza akili gani hizi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio skilled hata chembe..... skills kazitoa wapi?
 

Hapo inshu kubwa ni hizi degree zinazoanzishwa vyuo vikuu kwa pressure za kisiasa. Nilimsikia Rutinwa (DVC wa UD) na yule waziri wa elimu wakijinasibu eti UD wanaanzisha tawi Bukoba, wamesecure ardhi ili kujenga chuo kitakachozalisha walimu wa Physics na Maths. As if hakuna walimu wa Physics na Maths walio mtaani na hawana kazi zinazoeleweka au hii nchi haina vyuo tayari vya kutosha kuzalisha walimu hao.

Hata hii petroleum engineering ilianzishwa kisiasa tu. Pale mlimani kuna maprofesa kazi yao kubwa ni kulobby wanasiasa na kuanzisha programmes mpya hata bila kuwa na vigezo vya kutosha. Huyo huyo dogo alikuwa akilalamika jinsi wanavyosoma vitu theory theory tu. Kumbe ili kukwiva na kuwa na sifa za kufanya kazi kama offshore driller duniani inahitaji mtaala na mafunzo tofauti kabisa.
 
Hizi course za petroleum hawa vipanga hawakupaswa kabsa kuzisoma, unakuta wadau wana one kali, GPA kali wapo mtaani aisee akati kuna course nyepesi mno wangezipiga wangekua na kitu mpaka sasa.

Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app
 
mnasumbuka tu kuwapeleka watoto kusomea magesi na mafuta.mtoto wa maskini anatakiwa kwenda veta na akimaliza huko atajiajiri moja kwa moja badala ya kung'ang'ania madigree ya kipuuzi
 
Ud, Petrol. Eng. ilikua hot kinoma, ni intake ya vipanga tu, na wako wachache, nyie mpo 50, wao wapo 15

picha linaaza PT jamaa kapangiwa Urafiki Textile Mills, baada ya graduu jamaa kala benchi kitaa
Kuna principle ya maisha ambayo huwa waafrika tunaisahau.

Somea kitu ambacho una uhakika kuwa rasilimali yake ipo nyumbani kwako au nchini mwako. Tanzania ni nchi ya wakulima na wafugaji!! Ni heri kijana ukajikita kwenye masuala ya kilimo na ufugaji tu au hata fani za ufundi.
 
Huu ni ukweli mchungu mkuu anachofanya degree na diploma anafanya hicho hicho ila vinana wetu wanasomea title na kupishana mishahara si sana aisee mfano tanesco pale wanapishana laki /laki na nusu hapo jua kwamba wa diploma anaingia site na huko ndo pesa ilipo bado hajapiga part time za installation na mazaga mengine kiukweli wanakunja parefu mno diploma hasa akiwa wa kujichanganya.

Kingine wakati wanakutana degree yule wa direct hawezi ku apply kazi ajira zikitoka maana hana hata cheti cha kumbeba wakati wa diploma akiona fursa imemnyookea kama hivyo anasimama masomo au anabadili shift kisha anazama kazini hapo anapiga pesa kiulainiii tu refer ajira zilizotoka miezi kadhaa nyuma biomedical, electrical n.k woote waliochukuliwa ni DIPLOMA na VETA.
 
Dogo wako ni smart sana !! Hyo course ni ngumu kama katoboa ni kichwa sana..yule Ontario na kizungu chake chote masomo yalimshinda akakimbia kweny forex alikuwa na sup mpaka anoona noma..hiyo course ni balaa yaani wanaosoma wako nondo .
UDSM ni nyoko, chuo kimejaa wakuda nguli wote unaowajua bongo hii!!! They are there to make students suffer nothing else. Yaani mhadhiri akikupa sup au carry over huwa ndo roho yake inaridhika.

Mitaala mibovu isiyoangalia soko la ajira linataka nini. Wanafunzi wa UDSM wanakalia vimbweta mpk suruali zinachakaa ili asi disco ila akitoka hapo kazi mtaani hakuna.


Why muwachukue wanafunzi wenye ufaulu mzuri sana kidato cha sita halafu muende kuwaharibia future yao kwa kuwapangia wasome kozi ambazo hazina ajira hapa nchini???


Hakuna jambo linalouma kama kukaza tako chuoni ili ufaulu halafu ukimaliza inakosa kazi. Inauma sana
 
Vijana wengi wanamaliza degree wanajua wamemaliza, hawajui kuna international professional certifications ambazo makampuni makubwa yanaconsider mbali na hizo degree zao...
 
Bro hadi madaktari na wafamasia, watu waliosoma diploma clinical medicine na pharmacy wakimaliza tu fasta wanaajiriwa mahospitalini ila mliosugua gaga miaka 4 au 5 mnaendelea kusota kitaani.

Waajiri wanaona bora wachukue watu wa diploma ili kuokoa kiwango cha mishahara.
 
Mimi ningeshauri kuwa katika mitaala ya vyuo hapa nchini ingekuwa mwanafunzi akimaliza mwaka wa pili basi aende akafanye kazi kwenye field yake kwa muda wa mwaka mzima kisha ndio arudi chuoni mwaka wa mwisho ili ahitimu. Imgesaidia sana kubadili mindset za vijana. Hapo UDSM wanafunzi wanakariri tu madesa ila vitendo ni zero. Mtu anahitimu hali ya kuwa si competent kwenye vitendo. Nimesoma pale miaka mingi iliyopita so napajua vizuri. Huwezi kumwambia mwanafunzi anayesomea kozi ngumu kama hiyo ya mafuta na gesi au uinjinia wowote ule aende field miezi miwili tu halafu utegemee awe competent kwenye hiyo degree yake.
 
Mwanafunzi wa COET pale UDSM analazimishwa asome zaidi ya kozi 13 hadi 15 kwa semister moja ,unategemea atakuwa competent kweli?? Kuna jamaa zangu walikuwa pale COET walikuwa wakinambia kuwa wao wanachagua tu kozi 8au 9 za kuzifanyia mtihani zinazobaki wanaingia chumba cha mtihani ilo waandike majina tu kisha wanatoka wakijua kuwa ni sup so watakwenda kusapua kwenye september conference.
 
mimi ni kati ya wale niliosoma na kufanya kazi kwenye haya makampuni ya mafuta na gesi. Tatizo kubwa ninaloliona ni sheria yetu ya Local Content, yaani kuwajali kwanza wazawa kuganya kazi kwenye hii miradi. Hii sheria ya 2017 ni nzuri sana ukiisoma lakini kwa bahati mbaya haifuatwi. wageni ndio wanaajiriwa kwenye haya makampuni. hayo makampuni karibia yote yana maofisi/makao makuu huko kwao ulaya, huwa wanaleta watu wao hapa na kufanya kazi. Pia unakuta watz ambao hata hawajasomea au kuwa na uzoefu kwenye mambo ya mafuta na gesi wanaajiriwa kisa tu wana michongo/watoto wa wa kubwa na kuachwa wale watoto wa maskini wenye uzoefu na waliosomea hoo fani.
 
Mkuu kama ulivyokazia jambo la Safety training courses ni mandatory ni jambo muhimu hata kama ungekuwa muhandishi tu wa habari labda utatumwa kufanya coverage ya offshore project.
1.Kwanza hutaruhusiwa kupanda hiyo chopper unless una valid certificate ya HUWET.(Helicopter Under Water Escape)
2.Ukiweza kufika huko kwenye oil fields LAZIMA ufanyiwe debriefing na Safety officer na ajilidhishe kama huyo journalist amekidhi viwango vya kufanya tour ndani ya Platform hiyo.

Tukirudi kwenye kazi za offshore,Jambo la Safety ndio kitu kikubwa na kinachosisitizwa sana kuliko jambo lolote.
1.Safety kwa mtu mwenyewe.
2.Safety kwa mitambo
3.Safety for Environment
Kukamilisha hayo mambo matatu ni kila sekunde,kila dakika,kila saa,kila siku hadi unapoenda likizo au mnapomaliza project.
Ikija tokea INCIDENT na ikadhibitishwa,ni jambo lisilokubaliwa,lakini likitokea kuna procedures za kufuatilia chanzo au probable causes kwa kutumia Y tree system, na kutafuta njia ya kudhibiti hilo jambo lisitokee tena.
Ili kupunguza sintofahamu hatufanyi kazi kwa kukurupuka au kujikomba,la hasha.
Kwanza kuna planning ya kazi unayotaka kufanya,Pili unatengeneza procedures yaani hatua kwa hatua ya kufanya kazi hiyo,tatu kuna Risk assessment katika kila hatua ya kuifanya kazi,na namna kupunguza au kuondoa kabisa risk,ndio itoke
kibali yaani Permit to Work tena kwa muda kadhaa kwa siku hiyo.

Bado kuna safety drills nyingi tu kwa uchache 40 drills kila kwa mwezi ,baadhi ya common drills.
Fire Fighting on board drill
Man overboard
Abandon the Platform or Rig
Pollution to contain drill
General Alarm drill
Rescue boat drill
H2S drill
Security drill

Safdty ndio msingi wa kazi offshoe sababu ya mazingira yake hatarishi.
Kwa kusisitiza safety,angalau kila week by observation ugundue jambo au kitu kisicho salama, unamtaadharisha huyo mtu,una kireport bila kumtaja jina mtu kwa maandishi tunaita Behavior Based Safety( BBS).
Kwa kumalizia tu Safety haikwepeki katika offshore sio option ni jambo la msingi na lazima.
 
Hata kama mimi ndio mzungu siwezi kuajiri mtu ambaye hana uzoefu au ujuzi kwenye hizi kazi. Tembelea karakana za pale COET- UDSM...ni aibu wallahi.

Yaani karakana toka tulipozirithi kutoka kwa mkoloni muingereza mpk leo zipo vilevile. Hakuna teknolojia yoyote mpya halafu unategemea mwanafunzi akitoka pale akakabidhiwe kitengo kikubwa cha ufundi kwenye mradi wa ma trilioni?
 
mnasumbuka tu kuwapeleka watoto kusomea magesi na mafuta.mtoto wa maskini anatakiwa kwenda veta na akimaliza huko atajiajiri moja kwa moja badala ya kung'ang'ania madigree ya kipuuzi
Sa unakuta ni mtoto wa maskini lakini ndio anajiweza sana darasani na automatically mtu wala hawi conscious na umaskini wake, si mzazi wa mtoto au mtoto mwenyewe.
 
Asante kwa ufafanuzi,ila mimi sina uhakika na hilo,siweziongelea nyanja nyingine ila kwa upande wa oil and gas
sijaonana na mtu yeyote wa hapa Tanzania aliyesaidiwa na ERB ..
Veta havizalishi engineers hata siku moja ,veta wanazalisha technicians na artisans WA ngazi ya CERTIFICATES , hawana entitlement ya kuitwa engineers hao , tena sidhani kama wana fani za mafuta na gesi pale ,sidhani .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…