Tatizo la vijana waliosomea mafuta na gesi kuzagaa mtaani wakati kila siku tunasikia miradi ya mafuta na gesi inazungumziwa na Serikali

Tatizo la vijana waliosomea mafuta na gesi kuzagaa mtaani wakati kila siku tunasikia miradi ya mafuta na gesi inazungumziwa na Serikali

Thinking yako ni ya Industrial Revolution Age! Tuko kwenye Information Age!
Mnaosoma ili mkaajiriwe kwenye miradi ya Serikali mmepitwa na wakati!
Kuna wenzenu darasa la saba wamejiongeza wanauza petrol na diesel vijijini kwenye shughuli za kilimo na migodi!
Ukipita njia inayotoka Kahama hadi Masumbwe kuna madumu yamening'inizwa maporini kuashiria biashara ya "kupiga nyoka" katika magari yaendayo Rwanda na Burundi inafanyika!
Jitu lina degree ya petroleum na gas linapiga miayo mtaani hata mia halina!
Elimu ya kijinga ya kukariri theories ( tena mengi yanatamka seori)!
Seori [emoji3][emoji3] hao watu ndo aina ya mto mada, bure kabisa. Yeye kaona mafuta na gesi tu, unajiuliza akili gani hizi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu huyo kijana ni bright na skilled?.mbona kazi za gas&oil zimejaa dunia nzima mwambie aombe nje ya tz..inashangaza sana vijana potentials kukomaa na kuajiriwa na Gov ambapo malipo ni kidogo wakati nchi nyingine fursa ni nyingi sana kwa skilled people.
Sio skilled hata chembe..... skills kazitoa wapi?
 
Meneja Wa Makampuni vijana vyuoni wamesomea petroleum mining and processing! Now, the country has no petroleum mines nor processing industry. Wafanyeje?! Wanajikuta nchi ina filling stations kama hizo Puma na wenzake. Waende huko kushika mkonge wa kujaza mafuta magari ya watu?! Mtihani kwelikweli. Yaani usome degree ya miaka 3 halafu ufanye kazi filling stations?!

Taifa iwaombe msamaha vijana

Jibu la mambo yote hayo ni serikali boss. Serikali ndio yenye maamuzi kwenye kuajiri. Na tunachotaka kuona ni hawa vijana wanaajiriwa hapa nchi kwasababu tuna miradi mingi tu. Kinacho ulizwa mbona miradi ipo na watu wa mafuta na gesi hawapewi kipaumbele? Jibu swali kama wewe ndio upo kwenye maamuzi ungefanyaje?
Hapo inshu kubwa ni hizi degree zinazoanzishwa vyuo vikuu kwa pressure za kisiasa. Nilimsikia Rutinwa (DVC wa UD) na yule waziri wa elimu wakijinasibu eti UD wanaanzisha tawi Bukoba, wamesecure ardhi ili kujenga chuo kitakachozalisha walimu wa Physics na Maths. As if hakuna walimu wa Physics na Maths walio mtaani na hawana kazi zinazoeleweka au hii nchi haina vyuo tayari vya kutosha kuzalisha walimu hao.

Hata hii petroleum engineering ilianzishwa kisiasa tu. Pale mlimani kuna maprofesa kazi yao kubwa ni kulobby wanasiasa na kuanzisha programmes mpya hata bila kuwa na vigezo vya kutosha. Huyo huyo dogo alikuwa akilalamika jinsi wanavyosoma vitu theory theory tu. Kumbe ili kukwiva na kuwa na sifa za kufanya kazi kama offshore driller duniani inahitaji mtaala na mafunzo tofauti kabisa.
 
Hizi course za petroleum hawa vipanga hawakupaswa kabsa kuzisoma, unakuta wadau wana one kali, GPA kali wapo mtaani aisee akati kuna course nyepesi mno wangezipiga wangekua na kitu mpaka sasa.

Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app
 
Nina mdogo wangu amemaliza mwaka huu shahada hii ya petroleum engineering pengine hii mada inanihusu sana. Ni miongoni mwa wale vijana bright kabisa division 1 point 4 form six aliyechaguliwa kusoma shahada hii selective pale mlimani.

Tunajenga nchi moja ya kijinga sana kuwaacha vijana wetu bora kabisa kusota mtaani. Nafikiri kama mzazi inabidi kumwandaa kijana wako kutopoteza muda na degree za wanasiasa bali mfundishe mapema stadi za maisha ikiwemo kilimo, biashara na ufundi mbalimbali.
mnasumbuka tu kuwapeleka watoto kusomea magesi na mafuta.mtoto wa maskini anatakiwa kwenda veta na akimaliza huko atajiajiri moja kwa moja badala ya kung'ang'ania madigree ya kipuuzi
 
Ud, Petrol. Eng. ilikua hot kinoma, ni intake ya vipanga tu, na wako wachache, nyie mpo 50, wao wapo 15

picha linaaza PT jamaa kapangiwa Urafiki Textile Mills, baada ya graduu jamaa kala benchi kitaa
Kuna principle ya maisha ambayo huwa waafrika tunaisahau.

Somea kitu ambacho una uhakika kuwa rasilimali yake ipo nyumbani kwako au nchini mwako. Tanzania ni nchi ya wakulima na wafugaji!! Ni heri kijana ukajikita kwenye masuala ya kilimo na ufugaji tu au hata fani za ufundi.
 
Wanaosoma diploma kwenye vyuo vya ufundi wapo more competent kuliko hao wanaotoka University hapa bongo.


Na makampuni hupenda kuajiri wenye diploma kwa kuwa mishahara yao huwa ni midogo kuliko wenye degree ilihali kazi wanazofanya zote ni zilezile. Mara chache sana kukuta vijana wenye diploma wakiwa wanazagaa mtaani.


Kuna mchizi mmoja nlikutana nae kwenye Research institute hapa daslaam, jamaa ana diploma ila yy ndio supervisor wa wanafunzi wote wanaotoka vyuo vikuu kwenda kufanya field pale.
Huu ni ukweli mchungu mkuu anachofanya degree na diploma anafanya hicho hicho ila vinana wetu wanasomea title na kupishana mishahara si sana aisee mfano tanesco pale wanapishana laki /laki na nusu hapo jua kwamba wa diploma anaingia site na huko ndo pesa ilipo bado hajapiga part time za installation na mazaga mengine kiukweli wanakunja parefu mno diploma hasa akiwa wa kujichanganya.

Kingine wakati wanakutana degree yule wa direct hawezi ku apply kazi ajira zikitoka maana hana hata cheti cha kumbeba wakati wa diploma akiona fursa imemnyookea kama hivyo anasimama masomo au anabadili shift kisha anazama kazini hapo anapiga pesa kiulainiii tu refer ajira zilizotoka miezi kadhaa nyuma biomedical, electrical n.k woote waliochukuliwa ni DIPLOMA na VETA.
 
CD9F6317-4E0D-4DEF-8929-5451433E37DA (1).jpeg

Leo November 1
 
Dogo wako ni smart sana !! Hyo course ni ngumu kama katoboa ni kichwa sana..yule Ontario na kizungu chake chote masomo yalimshinda akakimbia kweny forex alikuwa na sup mpaka anoona noma..hiyo course ni balaa yaani wanaosoma wako nondo .
UDSM ni nyoko, chuo kimejaa wakuda nguli wote unaowajua bongo hii!!! They are there to make students suffer nothing else. Yaani mhadhiri akikupa sup au carry over huwa ndo roho yake inaridhika.

Mitaala mibovu isiyoangalia soko la ajira linataka nini. Wanafunzi wa UDSM wanakalia vimbweta mpk suruali zinachakaa ili asi disco ila akitoka hapo kazi mtaani hakuna.


Why muwachukue wanafunzi wenye ufaulu mzuri sana kidato cha sita halafu muende kuwaharibia future yao kwa kuwapangia wasome kozi ambazo hazina ajira hapa nchini???


Hakuna jambo linalouma kama kukaza tako chuoni ili ufaulu halafu ukimaliza inakosa kazi. Inauma sana
 
Nimeona hili leo niliseme pengine viongozi wetu hawalifahamu swala hili:

Kweli kumekua na tatizo la vijana wetu waliosomea fani za mafuta na gesi kuzagaa mtaani tangu fani hizi zilipo anzishwa mwaka 2013. Asilimia 80 ya vijana waliosomea fani hizo hawaja ajiriwa mpaka sasa. Na walianza kuhitimu mwaka 2016.

Vijana wanahitimu lakini nafasi za kazi zinazotoka haziendani na idadi ya wahitimu.

Kila siku tunasikia miradi ya mafuta na gesi inazungumziwa lakini vijana hawa wa mafuta na gesi hawapati nafasi ya kwenye miradi hiyo.

Makampuni yetu ya serikali yakitangaza nafasi, zinazowahusu vijana wa mafuta na gesi zinakua ni chache sana hata kumi hazifiki.

Vijana wanazidi kuzeeka mtaani hawana pakujishikiza.

Viongozi wetu wanapaswa kuwatazama hawa vijana wa mafuta na gesi. Wengi wanajikatia tamaa kabisa hasa wanaposikia miradi inatangazwa kila siku ila ajira zinazotolewa na hiyo miradi hazihusu fani za mafuta na gesi.

Jamani jamani ni kweli keki ya mafuta na gesi ni tamu kiasi kwamba watu hupenda kung'ang'aniana lakini tunapaswa kuwapa ajira zao vijana hawa. Ajira zipo kote sekta binafsi na serikalini ila vijana hawa wanatengwa.

Serikali ingefanya jambo katika swala hili.

Mpaka nikawa najiuliza maswali ni kitu gani kinashindikana kuwaajiri vijana hawa. Walau ajira zilingane na idadi ya wanao hitimu kwasababu miradi tunaiskia kila siku.

Tuna mradi wa Helium. Na mingine mingi tu ya gesi na mafuta. Hivi ni kitu gani kinashindikana kuwakusanya hawa vijana wote wa mafuta na gesi na kuwatupia kwenye hiyo miradi.

Lakini wakati mwingine ikionekana fani zimeshakua na idadi kubwa ya wahitimu, pia ni jambo jema kuzibadilisha fani hizo ili ziendane na soko la ajira.

Hii ni orodha ya makampuni ambayo vijana wa mafuta na gesi wana nafasi ya kuajiriwa hapa Tanzania.
  • Shell Tanzania
  • Total Tanzania Ltd
  • East African Crude Oil Pipeline (EACOP) project In Tanzania
  • Swala Oil and Gas Tanzania Plc
  • Statoil Tanzania Limited
  • Ndovu Resources Ltd/Aminex Plc
  • CAROIL(T) limited
  • Equinor Tanzania
  • Songas Limited
  • Dodsal Resources & Mining Itingi (Tanzania) Pvt. Ltd
  • Maurel exploration Production Tanzania Limited
  • Artumas Energy Ltd. (Wentworth Resources Limited)
  • Lake Oil Ltd.
  • Pan African Energy Tanzania Ltd
  • Heritage Oil Tanzania Ltd
  • Tanzania Petroleum Development Corporation
  • Orca Exploration Group Inc.
  • Petrofuel
  • Barkat Gas
  • Oilcom (T) Limited Terminal
  • Swala Oil and Gas (Tanzania) PLC (SOGTP)
  • State Oil
  • Halliburton
  • Aminex PLC
  • Oryx Energies
  • Lake Group
  • PUMA
  • MOGAS
  • VIVO Energies
  • TPDC
  • EWURA
  • TBS
  • PURA
  • OIL COM
  • N.K
Ahsante sana
Vijana wengi wanamaliza degree wanajua wamemaliza, hawajui kuna international professional certifications ambazo makampuni makubwa yanaconsider mbali na hizo degree zao...
 
Huu ni ukweli mchungu mkuu anachofanya degree na diploma anafanya hicho hicho ila vinana wetu wanasomea title na kupishana mishahara si sana aisee mfano tanesco pale wanapishana laki /laki na nusu hapo jua kwamba wa diploma anaingia site na huko ndo pesa ilipo bado hajapiga part time za installation na mazaga mengine kiukweli wanakunja parefu mno diploma hasa akiwa wa kujichanganya.

Kingine wakati wanakutana degree yule wa direct hawezi ku apply kazi ajira zikitoka maana hana hata cheti cha kumbeba wakati wa diploma akiona fursa imemnyookea kama hivyo anasimama masomo au anabadili shift kisha anazama kazini hapo anapiga pesa kiulainiii tu refer ajira zilizotoka miezi kadhaa nyuma biomedical, electrical n.k woote waliochukuliwa ni DIPLOMA na VETA.
Bro hadi madaktari na wafamasia, watu waliosoma diploma clinical medicine na pharmacy wakimaliza tu fasta wanaajiriwa mahospitalini ila mliosugua gaga miaka 4 au 5 mnaendelea kusota kitaani.

Waajiri wanaona bora wachukue watu wa diploma ili kuokoa kiwango cha mishahara.
 
Mimi ningeshauri kuwa katika mitaala ya vyuo hapa nchini ingekuwa mwanafunzi akimaliza mwaka wa pili basi aende akafanye kazi kwenye field yake kwa muda wa mwaka mzima kisha ndio arudi chuoni mwaka wa mwisho ili ahitimu. Imgesaidia sana kubadili mindset za vijana. Hapo UDSM wanafunzi wanakariri tu madesa ila vitendo ni zero. Mtu anahitimu hali ya kuwa si competent kwenye vitendo. Nimesoma pale miaka mingi iliyopita so napajua vizuri. Huwezi kumwambia mwanafunzi anayesomea kozi ngumu kama hiyo ya mafuta na gesi au uinjinia wowote ule aende field miezi miwili tu halafu utegemee awe competent kwenye hiyo degree yake.
 
Mwanafunzi wa COET pale UDSM analazimishwa asome zaidi ya kozi 13 hadi 15 kwa semister moja ,unategemea atakuwa competent kweli?? Kuna jamaa zangu walikuwa pale COET walikuwa wakinambia kuwa wao wanachagua tu kozi 8au 9 za kuzifanyia mtihani zinazobaki wanaingia chumba cha mtihani ilo waandike majina tu kisha wanatoka wakijua kuwa ni sup so watakwenda kusapua kwenye september conference.
 
mimi ni kati ya wale niliosoma na kufanya kazi kwenye haya makampuni ya mafuta na gesi. Tatizo kubwa ninaloliona ni sheria yetu ya Local Content, yaani kuwajali kwanza wazawa kuganya kazi kwenye hii miradi. Hii sheria ya 2017 ni nzuri sana ukiisoma lakini kwa bahati mbaya haifuatwi. wageni ndio wanaajiriwa kwenye haya makampuni. hayo makampuni karibia yote yana maofisi/makao makuu huko kwao ulaya, huwa wanaleta watu wao hapa na kufanya kazi. Pia unakuta watz ambao hata hawajasomea au kuwa na uzoefu kwenye mambo ya mafuta na gesi wanaajiriwa kisa tu wana michongo/watoto wa wa kubwa na kuachwa wale watoto wa maskini wenye uzoefu na waliosomea hoo fani.
 
Unaweza kuzitaja kampuni hizo?
Unajua nivizuri ulivyoanzisha uzi kubali pia facts nyingine uongeze uzoefu.
Mkuu sblandes ameelezea vizuri sana hapo juu,kuna taasisi nyingi duniani zinazotoa elimu na kukuthibitisha kwamba wewe umekidhi viwango vya usalama vinavyotakiwa,hapo suala la elimu yako haliwezi kukubeba
kama hujafuzu mitihani yao ya usalama,na pindi unapofuzu inakupa kibali cha kufanya/kuomba kazi si tanzania tuu bali dunia nzima.
Shida kubwa tuliyonayo wabongo ni kwamba ukishalishwa tangopori kwamba ukiwa injinia wewe ni mtu mkubwa
na wewe unabweteka na kuanza kulalamika bila kujiongeza.
Ningefurahi kama mtu,angeomba ushauri wa namna ya kufanya hizo certification ili kuiongezea thamani hiyo degree yako ya petrolium.
Mkuu kama ulivyokazia jambo la Safety training courses ni mandatory ni jambo muhimu hata kama ungekuwa muhandishi tu wa habari labda utatumwa kufanya coverage ya offshore project.
1.Kwanza hutaruhusiwa kupanda hiyo chopper unless una valid certificate ya HUWET.(Helicopter Under Water Escape)
2.Ukiweza kufika huko kwenye oil fields LAZIMA ufanyiwe debriefing na Safety officer na ajilidhishe kama huyo journalist amekidhi viwango vya kufanya tour ndani ya Platform hiyo.

Tukirudi kwenye kazi za offshore,Jambo la Safety ndio kitu kikubwa na kinachosisitizwa sana kuliko jambo lolote.
1.Safety kwa mtu mwenyewe.
2.Safety kwa mitambo
3.Safety for Environment
Kukamilisha hayo mambo matatu ni kila sekunde,kila dakika,kila saa,kila siku hadi unapoenda likizo au mnapomaliza project.
Ikija tokea INCIDENT na ikadhibitishwa,ni jambo lisilokubaliwa,lakini likitokea kuna procedures za kufuatilia chanzo au probable causes kwa kutumia Y tree system, na kutafuta njia ya kudhibiti hilo jambo lisitokee tena.
Ili kupunguza sintofahamu hatufanyi kazi kwa kukurupuka au kujikomba,la hasha.
Kwanza kuna planning ya kazi unayotaka kufanya,Pili unatengeneza procedures yaani hatua kwa hatua ya kufanya kazi hiyo,tatu kuna Risk assessment katika kila hatua ya kuifanya kazi,na namna kupunguza au kuondoa kabisa risk,ndio itoke
kibali yaani Permit to Work tena kwa muda kadhaa kwa siku hiyo.

Bado kuna safety drills nyingi tu kwa uchache 40 drills kila kwa mwezi ,baadhi ya common drills.
Fire Fighting on board drill
Man overboard
Abandon the Platform or Rig
Pollution to contain drill
General Alarm drill
Rescue boat drill
H2S drill
Security drill

Safdty ndio msingi wa kazi offshoe sababu ya mazingira yake hatarishi.
Kwa kusisitiza safety,angalau kila week by observation ugundue jambo au kitu kisicho salama, unamtaadharisha huyo mtu,una kireport bila kumtaja jina mtu kwa maandishi tunaita Behavior Based Safety( BBS).
Kwa kumalizia tu Safety haikwepeki katika offshore sio option ni jambo la msingi na lazima.
 
mimi ni kati ya wale niliosoma na kufanya kazi kwenye haya makampuni ya mafuta na gesi. Tatizo kubwa ninaloliona ni sheria yetu ya Local Content, yaani kuwajali kwanza wazawa kuganya kazi kwenye hii miradi. Hii sheria ya 2017 ni nzuri sana ukiisoma lakini kwa bahati mbaya haifuatwi. wageni ndio wanaajiriwa kwenye haya makampuni. hayo makampuni karibia yote yana maofisi/makao makuu huko kwao ulaya, huwa wanaleta watu wao hapa na kufanya kazi. Pia unakuta watz ambao hata hawajasomea au kuwa na uzoefu kwenye mambo ya mafuta na gesi wanaajiriwa kisa tu wana michongo/watoto wa wa kubwa na kuachwa wale watoto wa maskini wenye uzoefu na waliosomea hoo fani.
Hata kama mimi ndio mzungu siwezi kuajiri mtu ambaye hana uzoefu au ujuzi kwenye hizi kazi. Tembelea karakana za pale COET- UDSM...ni aibu wallahi.

Yaani karakana toka tulipozirithi kutoka kwa mkoloni muingereza mpk leo zipo vilevile. Hakuna teknolojia yoyote mpya halafu unategemea mwanafunzi akitoka pale akakabidhiwe kitengo kikubwa cha ufundi kwenye mradi wa ma trilioni?
 
mnasumbuka tu kuwapeleka watoto kusomea magesi na mafuta.mtoto wa maskini anatakiwa kwenda veta na akimaliza huko atajiajiri moja kwa moja badala ya kung'ang'ania madigree ya kipuuzi
Sa unakuta ni mtoto wa maskini lakini ndio anajiweza sana darasani na automatically mtu wala hawi conscious na umaskini wake, si mzazi wa mtoto au mtoto mwenyewe.
 
Asante kwa ufafanuzi,ila mimi sina uhakika na hilo,siweziongelea nyanja nyingine ila kwa upande wa oil and gas
sijaonana na mtu yeyote wa hapa Tanzania aliyesaidiwa na ERB ..
Veta havizalishi engineers hata siku moja ,veta wanazalisha technicians na artisans WA ngazi ya CERTIFICATES , hawana entitlement ya kuitwa engineers hao , tena sidhani kama wana fani za mafuta na gesi pale ,sidhani .
 
Back
Top Bottom