Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Labda ndio mitambo mipyaNimeiangalia leo ni wingu nzito kama kawaida hata picha hazionekani vizuri!!
Khaa umetumwa? Wenzao waliwezaje wao washindwa?Nimepitia maoni. Nasikitika kwamba bado wengi mmejikita kwenye kulalamika zaidi badala ya kupendekeza angalau program ideas ili kulimaliza tatizo.
Nyuzi za malalamiko zipo nyingi sana na tayari yanafahamika. So nasisitiza tujielekeze zaidi kwenye mapendekezo kuhusu kinachotakiwa kufanywa huku tukitoa ideas ambazo zinaweza kufanyiwa kazi.
TBC ni mali yetu sote. Ni lazima tutoe mawazo yanayojenga ili ifanikiwe.
Naelewa tuko disappointed kwa sababu ya itikadi zetu na jinsi tunavyohisi hakuna fairness, lakini tuweke grudges pembeni na tuelekeze njia sahihi ya kupita.
Tusilalamike tu ili kuponya nafsi zetu. Tutoe constructive ideas ili kuiponya TBC yetu.
Njia pekee ya kuifanya TBC irudi kutazamwa na wananchi ni KUACHANA KABISA NA CCM na kubadili jina na ikiwezekana badilisheni hata jengo ili kuondoa kabisa laana mliyopewa , ukitaka kujua chuki ya wananchi kwa ccm , jaribu Leo hii kumfufua Bob Marley halafu tangaza kwamba anajiunga na TOT halafu muandalie onyesho la wazi uwanja wa Taifa au Mnazi Mmoja , uone hata kama ataambulia watu 10 , kuiunganisha TBC na ccm ni kosa ambalo halina msamaha .Ndugu WanaJF,
Kumekuwepo na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi na hata hapa JF kuhusiana na changamoto ya vipindi vya Televisheni ya Taifa (TBC1). Malalamiko hayo yameegemea zaidi katika eneo la ubora wa vipindi na ubunifu.
Kwa bahati nzuri, Mkurugenzi pamoja na Watendaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) ni wadau wakubwa wa JamiiForums na huwa wanafuatilia taarifa na mijadala mbalimbali inayoendelea hapa. Hivyo tukiitumia vyema nafasi hii, tutawasaidia kuboresha maeneo ambayo yanatakiwa kurekebishwa kwa haraka.
Naomba tutumie uzi huu kutoa maoni, ushauri na mapendekezo kuhusu aina ya vipindi na ubunifu ambao ukitumiwa utasaidia kuifanya televisheni hii ya taifa kuvutia kutazamwa na kufurahiwa.
Tumeshalalamika sana. Sasa ni wakati wa kuchukua hatua na kutaja suluhu kwa mifano ili kuimaliza changamoto hii kabisa.
Karibuni sana.
Tuachane na kwenye siasa kidogo. Hayo yameshasikika vya kutosha sasa naamini yatafanyiwa kazi.Njia pekee ya kuifanya TBC irudi kutazamwa na wananchi ni KUACHANA KABISA NA CCM na kubadili jina
Picha na sauti ni mbovu sana.Tuachane na kwenye siasa kidogo. Hayo yameshasikika vya kutosha sasa naamini yatafanyiwa kazi.
Hakuna mawazo mbadala nje ya hayo ya kisiasa ambayo TBC wanatakiwa kuyafanyia kazi?
Jina nalo ni tatizo? Unashauri iitwe jina gani?
Karibu.
Huyu jamaa anayejibu anatuchukulia poa. Mkuu wengi waluojitokeza sio waandishi wa habari bali ni wapenda habari. Wengine tumefunga mitambo ya kisasa, ma_ uhd tv, mi android tv box, ma satelite tv mbalimbali kunyaka habari ( kama mnavyoita mubashara), tunawaonea huruma hao wa vijijini mnaowatesa. Mnawapa picha za hovyo mpaka wanadhani tv zao mbovu kumbe ninyi ndio wabovu.
We demand quality news. Hivi TBS wana viwango vya utangazaji? ISO JE,.
Ningepewa mwaka 1 tu na ninyi mngetambua.
Natamani mpate kiongozi '" kichaa"' kwa usemi wa sasa.
Kwa kiwango cha teknologia ya habari ilikofikia na bei zake kufanya mnachokifanya ni kuidhalilisha Tanzania.
We have a lot of creative minds in this country.
........jihesabuni kuwa mnabahati sana..... mnakuwa wazembe hivi na bado mpo kazini na vichwa vipo mtaani....
Mrudisheni Tido Mhando akamilishe kazi aliyoianza hapo TBC au mpate mtaalam mwenye exposure ya kutosha kama aliyokuwa nayo Tido. Vinginevyo mmekosa ubunifu. Mnarudisha mavipindi ya zamani -club raha show ili iwejeAcheni kutumika kisiasa! Tunashindwa kuwelewa kama nyie ni Television ya Taifa au tawi la chama?
Ubora wa picha ni sifuri kabisa!
Nchi hii imejaa vijana zaidi ya 70% nyie asilimia 80 ya vipindi vyenu ni vya kizee!
Mnashindwa hata kuonesha mechi ya Taifa stars mmekalia ziara za viongozi wa chama wakitembelea matawi sijui kigoma gani huko!
Mmetangaza kufunga mitambo mipya ya kisasa na picha ndo kabisa zimerudi zile za kiwango cha chini kabisa!
Subirini na wengine wanakuja na mjiandae kwa POVU ZAIDI
Siasa ndio chanzo cha kifo cha TBC , kwahiyo ni lazima tukitaka kuwaokoa tuizungumzie sana , kubadili jina ni muhimu sana ili kuwaonyesha wananchi kwamba mmefungua ukurasa mpya , kisaikolojia ni muhimu sana , hiyo tv yenu imechafuka kiasi hata mkitoa ofa ya kutangaza bure bidhaa zinazotengenezwa na kiwanda changu sitakubali , maana najua huo ndio utakuwa mwisho wa mauzo ya bidhaa zangu , watu wanaogopa hata kuleta matangazo ya vifo kwenye tv yenu , hii ni hatari sana !Tuachane na kwenye siasa kidogo. Hayo yameshasikika vya kutosha sasa naamini yatafanyiwa kazi.
Hakuna mawazo mbadala nje ya hayo ya kisiasa ambayo TBC wanatakiwa kuyafanyia kazi?
Jina nalo ni tatizo? Unashauri iitwe jina gani?
Karibu.
Hii imebeba hoja zote. Kama wameleta mjadala huu kwa lengo la kupata USHAURI, washughulike na hayo, mengine yataboreshwa taratibu. TV ambayo inakula kodi za wananchi lakini inaacha kuonyesha mambo ya kuwafanya wananchi wafurahie kodi zao wanaonyesha vitu vya kufurahisha kikundi cha watu wachache. Mbona kipindi cha Tido Mhando tuliipenda, management ndo tatizo, inaendeshwa kwa remote.....Acheni kutumika kisiasa! Tunashindwa kuwelewa kama nyie ni Television ya Taifa au tawi la chama?
Ubora wa picha ni sifuri kabisa!
Nchi hii imejaa vijana zaidi ya 70% nyie asilimia 80 ya vipindi vyenu ni vya kizee!
Mnashindwa hata kuonesha mechi ya Taifa stars mmekalia ziara za viongozi wa chama wakitembelea matawi sijui kigoma gani huko!
Mmetangaza kufunga mitambo mipya ya kisasa na picha ndo kabisa zimerudi zile za kiwango cha chini kabisa!
Subirini na wengine wanakuja na mjiandae kwa POVU ZAIDI
Naona sasa umeamua kutapika nyongo kabisa, umejitahidi lakini umeona uuseme ukweli. Hii lugha ya serikali ya ccm imetafsiriwa visivyo, nchi zote zina serikali na kuna vyama vinavyotawala lakini tuitumie hii kauli jinsi inavyotakiwa. Ni kweli kabisa TV ibaki kua ya Taifa/serikali ambayo ni kwa watu wote hivyo ioneshe vipindi bila kuegemea upande mmoja.Lakini pia na ukweli usemwe. TBC haiwezi kuwa huru kiviile. Labda tuwashauri ccm waje na tv yao waache kuitumia TBC kichama. Wanatuharibia. Inaendeshwa kwa kodi za raia wote na wageni pia.
Hii dhana ya serikali ya ccm inatumika visivyo.
Mkuu, siyo namba 3 na kuendelea tu, hata namba zingine zina umuhimu katika kuboresha. Hata hayo wanayoyatoa wengine ni dawa pia kwa TV yetu ya taifa hata kama ni machungu. Kusanya yote mkae myafanyie kazi.Asante mkuu. Angalau wewe umetoa ushauri elekezi kuanzia namba 3 na kuendelea. Hiki ndicho nilichokilenga. Tutaje ideas kama hivyo. Asante.