BTW: kulikua na sheria au pendekezo la kulazimisha vituo vyote kujiunga TBC wakati wa taarifa ya habari saa mbili usiku, liliishia wapi sijui.
Mkuu hii sheria ipo hai na inasubiri muda tu.
Sheria iliyopitishwa Dodoma majuzi inampa waziri wa habari nguvu za kuagiza chombo chochote cha habari kutangaza habari kwa mujibu wake
Hii maana yake ni kuwa ipo siku utasikia waziri wa habari akiagiza vyombo vyote viungane na TBC katika prime time ili za kupikwa zisikomezwe vichwani mwa umma
Kwavile sheria ile ilipingwa na ilipitishwa kwa tuhuma za 'milioni 10' kinachofanyika ni kupitisha muda ili siku ikitangazwa isionekane jambo jipya bali utekelezaji tu wa sheria
Hii ni kuhakikisha mzozo wa sheria hiyo unafifia kabla ya kuzusha wa saa 2 usiku
Wanajua kuwa TBC imepoteza mashiko haina audience na imebaki hewani yenyewe
Inapata ruzuku na inafanya biashara,haiwezi kushindana na vyombo binafsi
TBC wasichojua, habari ni kama bidhaa inauzwa , ina wateja, inathamani ,ubora n.k.
Katika soko huria wananchi wana kiu ya habari, kutoa habari zisizo na ukweli, udanganyifu na ulaghai ni kuwafanya wajinga. Zama hizo zilikwisha na RTD
Siku hizi watu wana uwezo wa kuangalia EA, China, Middle east, ulaya na Marekani.
Nani ana muda wa kuangalia habari zilizochujwa, finyangwa, zilizoratibiwa Lumumba?
Hawa watu wanakaa vikao kwasababu hawajui mchawi wao ni wao wenyenyewe.
Huwezi kuuza nyanya zilizooza ukategemea 'rating' katika soko la ushindani
Wanachotakiwa ni kuwa huru na 'vyombo' vile vinavyowaelekeza nini cha kusema.
Wanatikiwa wasiwe biased , walete habari zinavyotokea na waache propaganda
Tido Mhando alijua nini maana habari. Alijua ni bidhaa na ilihitaji soko na ubora.
Kwasababu tu hakuendana na maagizo ya mtaa wa ''New street'' akaondolewa
TBC ni chombo cha chini, dhaifu kama unataka kufungua kichwa chako na kuhabarika
Watakaa vikao mpaka kupambazuke, mchawi wao ni wao wenyewe
Ni moja ya mashirika ya umma yanayohitaji kufutwa, hata ikifa leo nani ataathirika!
Pesa za kuendesha TBC zilielekezwe katika mikopo ya wanafunzi, TBC ifungwe tu