Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
TBC Wanatafuta Mchawi wakijua mchawi wao ni wao wenyewe
Ukiweka TBC na TV yoyote hata ya mtaani tu,rating ya TBC itakuwa chini
Hakuna anayeangalia habari za TBC kwasababu hazina ukweli, zinapinda ukweli, zimegemea CCM , zinalenga kutetea serikali, zina nia ya kukandamiza upinzani na kubwa ni udanganyifu danganyifu tu
TBC imekuwa tawi la CCM na serikali yake dhidi ya ukweli wa habari zilivyo katika jamii
Watu wanakumbuka uchaguzi mkuu, mikutano ya CCM ilikuwa wazi, ya wapinzani umeme hakuna
Kama unavyoona magazeti ya CCM na serikali yalivyo susiwa na umma TBC haiko mbali
Ni chombo kinachotumiwa kama 'chombo cha dola' kikiacha misingi yake ya kuhabarisha na kugeuka kuwa chombo cha propaganda, uongo na ulaghai tu.
TBC inaendeshwa kwa maagizo ya vyombo vingine na si maagizo ya tasnia ya habari au taaluma
Viongozi wanaisusia si kwasababu inawatendea ubaya! ni kwasababu habari zao haziwezi kufikia umma kutokana na poor rating na audience ya TBC. Nani ana muda wa kuangalia uongo na uzushi
Watakaa vikao sana hakuna watakachopata zaidi ya kujidanganya tu
Wamuulize Tido ilikuwaje! Tido 'aliwekwa' kando kwasababu hakusimama na wanaodhibiti TBC kama Uhuru, Mzalendo na Habarileeeo.
Ukimuona mtu anaangalia habari za TBC, ujue uwezo wake wa kupambanua mambo una shaka
Hata wapiga propaganda wanaikimbia seuse mtu mwenye akili timamu
TBC hata ikifungwa leo haina athari zozote katika tasnia ya habari nchini na sijui kama kuna mtu atajua hawapo hewani, sijui!
Mkuu hii sheria ipo hai na inasubiri muda tu.BTW: kulikua na sheria au pendekezo la kulazimisha vituo vyote kujiunga TBC wakati wa taarifa ya habari saa mbili usiku, liliishia wapi sijui.
Hatari, bila kuforce hakuna mtu anaweza kununua?Wanafanya kuforce kuleta ofisini... wanalazimisha kuyauza ofisini.
Wamwombe msamaha Tido. Hawajui kwao ni kule waja leo warudi leo!Sasa kama wanaripoti mambo yasiyo na uhalisia nani aangalie hyo kitu?
Mbona Tido aliwezesha TBC kuwa na mvuto?
Watuambie ruzuku huwa wanafanyia nini, badala ya kutumia ruzuku kutafuta na kutengeneza habari, huenda wanaripana poshoUonngozi wa juu wa TBC na wafanyakazi wengine wa kituo hicho usiku wa kuamkia leo wamefanya kikao cha dharura kuangalia sababu za kudorora kwa kituo hicho kikubwa cha TV ambacho kimemalizika saa 11 alfajiri.
Pamoja na mengine kitu kilichoonesha kuwaumiza kichwa zaidi ni jinsi gani kituo kikubwa kama hicho kinachopata ruzuku kubwa kutoka serikalini kinakuwa na ratings za mwisho huku kikizidiwa na vituo ambavyo havina hata miaka mitano hewani.
Mkurugenzi amesisitiza sana na kuwaomba wafanyakazi wa TBC kama ikitokea rais anapiga tena simu kwenye kituo chochote cha TV basi iwe TBC na ikiwa anatuma kadi ya salamu basi iwe TBC.