TBT: Foleni ya kwenda kwa Babu wa Loliondo

TBT: Foleni ya kwenda kwa Babu wa Loliondo

Ilikuwa sio poa 🔥
images.jpeg
 
Nakumbuka baba yangu aligeuza fuso la mizigo akawa anabeba abiria kutoka A town mbaka loliondo kwa Babu

Mungu mkubwa Mzee alifanikiwa kwa ule upepo
 
Hii ilidhihirisha kuwa watanzania ni wajinga.ukiwaambia hata mkia wa fisi unatibu magonjwa yote ukiula wataamini.
Na waliotoka mataifa mengine unasemaje?
maana walifika hapo pia kupata kimoja.
 
Mpaka leo watu wa namna hiyo wapo wengi tu, kama huamini nenda kwa wauza dawa za asili/mitishamba uone,,,, hasa wale maarufu 🫣🫣🙌🏽
 
Hakuna formula yoyote man, mti wa Moringa ni jamii ya miti dawa inayojulikana kimataifa, ipo kwenye kundi moja na akina aloe vera,mlonge, na mwenzake muarobaini, miti yote hii inatambulika kuwa ni tiba kwa magonjwa mbalimbali ya binaadamu na wanyama na pia ndege, issu iliyokuwepo pale loliondo ilikuwa ni ku exagerate ubora wa tiba hiyo, na kuufanya mti wa moringa kuwa unique kuliko miti hiyo mingine, hata wewe ukiweza kuutangaza muarobaini kwa namna ile utapiga hela vizuri tu.
Hilo sio tatizo kila mtu miti anaijua

Changamoto ni vichanganyio mfano chai ya muarobaini inatibu igonjwa fulani ili ikamilike inabidi utie ndimu kama kichanganyio ili formula ikamilike

Hicho ndicho nilichomaanisha mkuu.

Uganga una siri zake
 
Ukijichanganya tu ukaenda loliondo huku nyuma watu wanapigia mstari kuwa una ngoma
 
Hiyo ilionesha Watanzania wengi ni wagonjwa, waliokosa kuelimika na waliokata tamaa ya maisha

Ilifikia kipindi mtu anamwondoa mgonjwa wake Hospitali ya Taifa Muhimbili eti anampeleka Kwa huyo Mzee huko Loliondo akanywe Kikombe cha dawa🙌

Sasa hivi wamehamia Kwa Mitume wananyweshwa Maji na kukanyaga mafuta 🙆

Tuna safari ndefu kama Nchi
Mkuu usilaumu watu

Chukulia mfano ndio wewe unaumwa upo mihimbili dawa zote zimedunda

Alafu unaangalia ITV chanel credible watu wanakunywa dawa wanapona na wewe ni bilionea kifo unakiona hiki hapa

Utashindwa kukodi hrlkopta uende loliondo?
 
Back
Top Bottom