TBT ya kibabe: Mabasi na vyombo vya usafiri Tanzania

Mzee hauna picha za basi ziliitwa Ilanga moto?? Hatari yake ilikua balaa. Walifungiwa wakati wa lile zoezi la Speed Governor.
 
Mwaka 2004 nilisafiri na basi la SCANDINAVIA kutoka Mwanza-Musoma-Silali-Nairobi-Namanga-Arusha-Moshi-Dar kwa wakati mmoja usiku na mchana
...Unakaguliwa passport usiku na askari wa Kenya.
Tulishakutana na vizuizi vya majambazi mara 3 pori la Namanga ndani ya mpaka.

Akaja huyu Mombasa raha... Naye akawa anapitia njia hiyo hiyo kuja huku Isebania -Sirari
 
Watu wa kale mlipata sana shida!!!! Kwaio pesa ilikua inatumwa kwa bus[emoji23]
...pesa inatiwa ndani ya bahasha ya kaki, inazungushiwa gundi bahasha yote kisha anapewa dereva.
Sasa jifanye kuchelewa kufika Ubungo stendi kupokea kibahasha chao...utapiga kwata kuwafuata gereji kwao wanakopaki.
Ila walikuwa waaminifu sana madereva wa enzi hizo.
Kongole kwa Scandinavia, Spider, Akamba na Mombasa raha kwa uaminifu wenu kipindi nasoma.
 
Umbeaaa huoooo.....utasutwaa
 
Super Najimunisa.....Majini 7
Enzi hizo Dodoma Shinyanga ni Vumbi tupu.
Basi Bwana,
Ilikuwa ni Mwaka 1999 natika Zangu Mwanza naenda Shule Morogoro nikaoanda Super najmunisa....Hahahah Acha Kabisa hili basi Sio Basi tuu ni Dereva Anaitwa “Rama Mtoto”
Alikuwa akiendesha Scania.93 ile nadhani!
Unaambiwa Kwanza Mpaka Matrafic walikuwa wanampenda...dogo alikuwa na control ajabu duu!
Basi Nimetoka mwanza tuko na Ligi ya Zuberi,Amit,
Tukaingia Shy chaaap,Hatukukaa sana Chombo Kikaoshwa....Hapo Zuberi na Amit wako mbele yetu[emoji3516][emoji41][emoji851][emoji30][emoji30]
Barabara ni vumbi tuu,Tukaanza Kumtafuta Mmoja baada ya Mwingine,Tunafika Tinde Amit huyu hapa...Chapa Rubber... tukaingia Nzega,Bado Zuberi haonekani...
Dogo anatembea anakuka Karanga tuu!
Mzee niko siti ya Mbele kabisa Nyuma yake,Tena yeye aliniambia Usilipe Nauli hela nipe Mimi! Nikampa.
Tunaingia Igunga...Zuberi huyu hapa nae anatoa Chombo...Sisi tukapaki kwanza...
Dereva Rama mtoto akasema tuondoke jamani,ngoma ikaanza...ni vumbi lakini Imechongwa....Piga piga Mara shelui Zeberi hiyu hapa....Akaombwa site,Overtake akakataa...[emoji3516][emoji3][emoji3][emoji3]Rama katulia tuu na Kitu Scania...
Ngoma Sekenke mlimani pale Rama akaomba tena Kwenye Mlima...[emoji30][emoji30][emoji30]Jamaa kambania kambania ile tunamaliza tuu ile S Rama akaingia kwenye tuta za Viazi[emoji23] Ngoma Imekubali mpaka watu wanashangilia Ile Overtake ya Kibabe! Jamaa Zeberi anachanganya wapi...Rama anatembea na Gia No.5 tuu Break ya Kwanza Singida tumekaa Pale Saa nzima Jamaa wooote mabadi yooote hayajatokea tuu Tukang’o chombo.
No.2 nyingine
Kama Kawaida dogo Rama Mtoto yupo Kwenye Super Najmunisa Tumekwama Manyoni kwenye Tope balaa!Sisi Tunaenda Dar,Tukakutana na Super najmunisa C.I.A ikiendeshwa na George
Wakati sisi tukiwa na NATO chini ya Dereva Mtoto Rama acha Kabisa!
Mlangoni yupo Mhindi Tajiri.
Baada ya Kushindikana Kupita na Magari yote yapo pale...Na Kamvua Kananyesha...Tukaambiwa tushuke tutembee...
Sawa tukashuka...Akabaki Rama peke yake kwenye Usukani....[emoji41][emoji851]
Akaanza Kuitoa Mashine...Kama Unavyojua Mlio wa Scania Mpaka Yule Tajiri Muhindi Akaanza Kutukana Kuionea Huruma Gari yake...[emoji51]
Ngoma Mpaka Imelala....
Rama Akairudisha nyuma eee bwanaeee...
Alipita nayo pale mkukuu inalala Kulia Na Kushoto jamaa yumoo tuu mpaka akaileta Upande wa Pili...
Halafu hao tukapanda tukaenda zetu[emoji851][emoji3516][emoji123][emoji91][emoji91]
Rama mtoto Super Najmunisa...Baadae Zuberi,Baadae nimesahau jina La Basi Alilokuwepo tena...
Alikuwa akishindana na Muhando(Marehemu kwa sasa)
Na Ukitaka Kumjua Ulikuwa unawnda Pale Ubungo Stendi Sehemu Inaitwa madereva Mashuhuru Utampata[emoji119]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…