TCRA mnaniharibia Kazi kuzima mitandao ya Kijamii. Mitambo ya Kiwanda inakufa

Mkuu hii mitambo ya wachina. Kupiga simu China sh ngapi kwa simu ya kawaida na Kutumia WhatsApp Call na Message Ni sh ngapi? Upo nyuma kimaendeleo wewe.
Jamani watu wameachwa nyuma bado,,,WhatsApp call au messenger ni MB kadhaa tuu tofauti na salio la kupiga kawaida.
Mimi siku hizi nawasiliana na Wadau wengi kutoka Ulaya,Asia,U.S.A kwa WhatsApp call au messenger call
 
Kumbe nikweli...kuliko kuzaliwa raia tz bora uwe kondoo australia utungeneze sufi watu wapate joto mabachelor apa tuko sawa
 
Hapa Kama robo saa nimeikosa JF tena na Internet. Sasa hata kwa email nakwama kufanya Kazi.
Simu inasema check your internet connection and try again hivi ninavyoandika sijui Kama hii meseji itakuja.
Ni Airtel natumia. Wafungue WhatsApp haraka.
Pole hii mpaka wiki 2
 
Pole, kuna kazi bila internet haziendi.na hatujui hii inaisha lini.
 
Mkuu,damka asubuhi sana kisha nenda kituo ulichojiandikisha kupiga kura. Ukipewa karatasi ya kura ya Urais nenda mwisho kabisa. Weka alama ya vema isiyoumiza ndani ya box. Tatizo lako litakuwa limeishia hapo.
 
NANI ALAUMIWE?

Je, ni kweli ni tisiaraei? Au ni wale 'vijana?' au ni 'wasiojulikana?'
 
Dash hii kitu inaumiza wengi basi tu...

Nna order ilibidi niwasiliane na mchina kuconfirm kesho,

na Pesa za watu mkononi,
ikiendelea wiki nitakuta mChina ananisubiri?!

Watu watanielewa?!

mbona siasa za wachache zinatuumiza hivi!!

Daah kati ya Siku nimegundua nipo kwenye Rubbish country ni leo
 
Na kwanini wazime mapema kiasi hiki!? Si wangesubiri baada ya uchaguzi.
 
Huu ukataji wa mitandao mmeikosesha sana mapato Serikali leo. Mifumo Mingi ya ukusanyaji mapato inatumia internet, nyie mnakata. TCRA hamna uchungu na nchi hii au mnapokea maagizo ya Nani kufanya hivi. Sisi watumishi chini tunatukanwa kama hatuna akili nzuri Kwa makosa yenu. Mngewatangazia watu basi wasije maofisini
 
Nenda google downloard proton VPN APK jisajili then upate huduma full, insta, youtube, Twitter in five mins.
 
Nitafute pm nikupe mbinu
 
Proton VPN inapiga kazi vizuri...(Whatsapp,Twitter,IG...,...,zinapatikana).Ukisha install wataku-direct kwenye login page...,kwa chini kuna register...,chagua hiyo then chagua free,..baada ya kujiregister utatakiwa kuchagua nchi na jiji unalotaka kutoke....
 
Tanzania rasmi yawa banana Republic, yaongozwa kidikteta kama equatorial guinea. Tulikwama wapi October 2015????!!
 
Ccm inashangaza hivi kweli haielewi hatua za watawala kuelekea mwisho wa utawala wao inavyokuwa!!!?[emoji848]
Hatua zao za mwisho huwa ni kuzima internet, na halijawahi kufanikiwa hata tawala moja
Mi navinjari na VPN wakuu[emoji23]
 
Unatatua tatizo ktk jamii au unataka kutatua tatizo la mtu, point yake ya msingi kwanini mitandao ya kijamii izimwe full stop
 
Hapa kwa kweli wametudhulumu... This is not fare.....

Inasikitisha sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…