TCRA mnaniharibia Kazi kuzima mitandao ya Kijamii. Mitambo ya Kiwanda inakufa

TCRA mnaniharibia Kazi kuzima mitandao ya Kijamii. Mitambo ya Kiwanda inakufa

Mkuu hii mitambo ya wachina. Kupiga simu China sh ngapi kwa simu ya kawaida na Kutumia WhatsApp Call na Message Ni sh ngapi? Upo nyuma kimaendeleo wewe.
Jamani watu wameachwa nyuma bado,,,WhatsApp call au messenger ni MB kadhaa tuu tofauti na salio la kupiga kawaida.
Mimi siku hizi nawasiliana na Wadau wengi kutoka Ulaya,Asia,U.S.A kwa WhatsApp call au messenger call
 
Hakika Kitendo chenu Cha kuzima WhatsApp kimeniuzi na kuniumiza Sana.

Nimepata hitilafu kwa mitambo ya kiwanda. Nikiwa napokea maelekezo ya Nini Cha kufanya kupitia Whatsapp ghafla mmeifungia.

Mmenipa hasara kubwa Sana.

Ninyi mngeacha WhatsApp. Mtu akivunja sheria mumuadhibu.
Kumbe nikweli...kuliko kuzaliwa raia tz bora uwe kondoo australia utungeneze sufi watu wapate joto mabachelor apa tuko sawa
 
Hapa Kama robo saa nimeikosa JF tena na Internet. Sasa hata kwa email nakwama kufanya Kazi.
Simu inasema check your internet connection and try again hivi ninavyoandika sijui Kama hii meseji itakuja.
Ni Airtel natumia. Wafungue WhatsApp haraka.
Pole hii mpaka wiki 2
 
Hakika Kitendo chenu Cha kuzima WhatsApp kimeniuzi na kuniumiza Sana.

Nimepata hitilafu kwa mitambo ya kiwanda. Nikiwa napokea maelekezo ya Nini Cha kufanya kupitia Whatsapp ghafla mmeifungia.

Mmenipa hasara kubwa Sana.

Ninyi mngeacha WhatsApp. Mtu akivunja sheria mumuadhibu.
Pole, kuna kazi bila internet haziendi.na hatujui hii inaisha lini.
 
Hakika Kitendo chenu Cha kuzima WhatsApp kimeniuzi na kuniumiza Sana.

Nimepata hitilafu kwa mitambo ya kiwanda. Nikiwa napokea maelekezo ya Nini Cha kufanya kupitia Whatsapp ghafla mmeifungia.

Mmenipa hasara kubwa Sana.

Ninyi mngeacha WhatsApp. Mtu akivunja sheria mumuadhibu.
Mkuu,damka asubuhi sana kisha nenda kituo ulichojiandikisha kupiga kura. Ukipewa karatasi ya kura ya Urais nenda mwisho kabisa. Weka alama ya vema isiyoumiza ndani ya box. Tatizo lako litakuwa limeishia hapo.
 
NANI ALAUMIWE?

Je, ni kweli ni tisiaraei? Au ni wale 'vijana?' au ni 'wasiojulikana?'
 
Dash hii kitu inaumiza wengi basi tu...

Nna order ilibidi niwasiliane na mchina kuconfirm kesho,

na Pesa za watu mkononi,
ikiendelea wiki nitakuta mChina ananisubiri?!

Watu watanielewa?!

mbona siasa za wachache zinatuumiza hivi!!

Daah kati ya Siku nimegundua nipo kwenye Rubbish country ni leo
 
Na kwanini wazime mapema kiasi hiki!? Si wangesubiri baada ya uchaguzi.
 
Huu ukataji wa mitandao mmeikosesha sana mapato Serikali leo. Mifumo Mingi ya ukusanyaji mapato inatumia internet, nyie mnakata. TCRA hamna uchungu na nchi hii au mnapokea maagizo ya Nani kufanya hivi. Sisi watumishi chini tunatukanwa kama hatuna akili nzuri Kwa makosa yenu. Mngewatangazia watu basi wasije maofisini
 
Dash hii kitu inaumiza wengi basi tu...

Nna order ilibidi niwasiliane na mchina kuconfirm kesho,

na Pesa za watu mkononi,
ikiendelea wiki nitakuta mChina ananisubiri?!

Watu watanielewa?!

mbona siasa za wachache zinatuumiza hivi!!

Daah kati ya Siku nimegundua nipo kwenye Rubbish country ni leo
Nitafute pm nikupe mbinu
 
Proton VPN inapiga kazi vizuri...(Whatsapp,Twitter,IG...,...,zinapatikana).Ukisha install wataku-direct kwenye login page...,kwa chini kuna register...,chagua hiyo then chagua free,..baada ya kujiregister utatakiwa kuchagua nchi na jiji unalotaka kutoke....
Njia ni kama ifuatavyo

Kitu cha kwanza jaribu kuingia google kupitia opera au chrome au uc mini au nyingijnezo yaani jaribu kuingia google kupitia hizo njia google ikifunguka tu yaani hakikisha google search inafunguka google ikifunguka kati ya hizo fuata hatua ya 2

Hatua hiyo ni kudownload vpn kwa google unadownload kupitia google kwa sababu playstore au appstore pashafeli download huko kwenye google kisha ukishadownload install

Pia usisahau kuallow installation from unknown sources

Kila la kheri!
 
Tanzania rasmi yawa banana Republic, yaongozwa kidikteta kama equatorial guinea. Tulikwama wapi October 2015????!!
 
Ccm inashangaza hivi kweli haielewi hatua za watawala kuelekea mwisho wa utawala wao inavyokuwa!!!?[emoji848]
Hatua zao za mwisho huwa ni kuzima internet, na halijawahi kufanikiwa hata tawala moja
Mi navinjari na VPN wakuu[emoji23]
 
Naona post yako ipo kama ya kiudaku hivi;
option1: wewe unamiliki Kiwanda unashindwa kuweka simu shs 10,000 kwenye simu upige hata kama ni China au marekani tena huko hiyo hela unapada madakika kibao.
Option 2: Si ungeandika tatizo la kiwanda chako hapa usaidiwe; wapo maingeneer humu wamepumzika wanasubiri kupiga kura kesho. Describe ni mashine gani, model #, inafanya kazi gani, na nini haikifanyi kwa sasa au unahitaji msaada gani
Unatatua tatizo ktk jamii au unataka kutatua tatizo la mtu, point yake ya msingi kwanini mitandao ya kijamii izimwe full stop
 
Hapa kwa kweli wametudhulumu... This is not fare.....

Inasikitisha sana!
 
Back
Top Bottom