Tetesi: TEC haifurahishwi na mwenendo wa Serikali kuhusu makubaliano ya bandari na DP World

Suzy Elias

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2021
Posts
1,067
Reaction score
6,200
Duru ndani ya TEC hawafurahishwi na namna Serikali ilivyokubaliana na DP Word kuhusu usimamizi wa bandari yetu/zetu.

"....Wahashamu wengi hawaungi mkono sintofahamu hiyo na huenda Katibu akaelekezwa aandae Waraka mahsusi kulisemea hilo hivi karibu."

"....nadhani baadhi ya vipengere ndani ya makubaliano yake hata wao yamewaogofya kama ilivyo kwa Watanzania wengi! Na ndiyo maana wao kulitolea tamko hilo jambo ni suala la wakati tu."

".....zoezi la kuwahoji mawakala wao Serikalini unaendelea ili wajiridhishe kabla ya kutoa tamko."

"....Mhashamu Rais nadhani bado anapitia madodoso ya safari iliyopita kule Vatican lakini kwa mjibu wa Mkurugenzi wa Miito Padre ( jina kapuni) amealikwa kesho yaani leo kwenye mkutano uhusuo mkataba ule. Nimeongea na Padre ..... hata Baba Askofu wake ameshangazwa na makubaliano yale tena akiyaita ya AJABU NA YANAYOWEZA KUKUBALIKA KWA WATU WAJINGA!"
 
Naona sasa ni muda wa nyoka kutoka shimoni....
Awamu ile watu walipokuwa wanapotezwa walikuwa wako kimya kweli.
Wengine walifunga hadi safari kwenda magogoni kupeleka zawadi za sanamu ya bikira Maria.
 
Naona sasa ni muda wa nyoka kutoka shimoni....
Awamu ile watu walipokuwa wanapotezwa walikuwa wako kimya kweli.
Wengine walifunga hadi safari kwenda magogoni kupeleka zawadi za sanamu ya bikira Maria.
Mi nachokaga hapo tu, sikuwahi kuwasikia awamu ile ila sasahivi hadi pini ikidondoka watatoa waraka hawa jamaa ni wanafki sijapata kuona
 
Wajitokeze hadharani tuwasikie wote siyo unaleta umbea wako usio na chanzo zaidi ya uzushi wako
 
Mwacheni Mama Afanye KAZI Yake
 
Hao ni wapumbavu na wajinga kenge hao wanataka vatican na yule kiongozi wao supporter wa ushoga ndio waje kuichukua bandari?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…