TEC toeni tamko kukemea ubaguzi kwenye elimu

Mleta mada pia ukumbuke kwamba seminaries nyingi lengo lao hasa ni kulea miito ili vijana waje wawe watawa. Na kimoja wanachikiangalia ni afya ya akili. Hawataki kuwa na mapadri vilaza
 
Kama hivyo ndivyo, basi tuanze kufuta utaratibu wa shule zote za vipaji za serikali
Kama:

Ilboru,
Mzumbe
Kibaha
Msalato
Nk
Hawa si wanabagua kwa kuchagua watoto wenye uwezo mkubwa pekee?

Na mtu aliyepata division 3 na 4 pia aende akasome Sheria chuo kikuu cha Dar es salaam wasichague div 1 na 2 pekee mbona vyuo vingine wanasoma??
Nadhani tusianze na TEC tuanze na Serikali halafu wengine waige mfano.
 
TEC wanadeal na ishu za kitaifa na kimataifa, kwa taarifa yako mahamuzi ya mkuu wa shule au mwl wa darasa hata askofu hawezi kuingilia kati, mwl wa darasa akisema unaondoka unaondoka kweli hata ulalamike mpaka Vatican hawawezi kukurudisha.
 
Ulishindwa kufikisha maksi hamsini?
 
Yaaani unalitoto linacheza magemu kuliko hata kula unataka likasome kwenye St??? Kabla ya yote unapita mchujo hakuna kukaa na kiazi shuleni,,,,,,kama litoto lako kiazi we lipeleke kwenye ile garage ya mme wa monalisa
 
Pole kwa kuzaa mtoto kiilazs
 
Sadaka za makanisa na misikiti yenu huwa mnawaachia wachungaji, mitume na manabii feki halafu mnalalamikia sadaka za wakatoliki?!
 
Mpeleke FEZA mwanao akapate elimu isiyokuwa na ubaguzi mkuu na nina imani kuwa hata udini haupo pale.
 
Shule za katoliki hazibagui imani ya mtoto. Kama ana vigezo anachukuliwa. Na atafuata taratibu zote za pale kama kwenda kanisani, kusali rosary ni lazima...
Waislam baadhi wanaojua umuhimu wa shule hupeleka watoto wao pale.
Hawabadilishwi dini ila ni lazima kufata utaratibu wa kikatoliki wakiwa shuleni.
 
nashauri mchujo uwe mkali kufikia wastani wa 85 kwa masomo yote na 75 kwa masomo ya sayansi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…