Tetesi: Tetesi za usajili wa dirisha kubwa ligi kuu Tanzania bara 2025/2026

Kwa muono wako giant of Tanzania football ni team gani??na toa sababu 3 tu
Ni simba kwa sababu amefika mahali ambapo yanga hajafika napo ni kwenye top five ya vilabu bora barani afrika kama hujui umuhimu wa hiyo nafasi nenda kawaulize viongozi wenu wanajua umuhimu wake, yanga kujisifia kuchukua makombe mengi ya ligi kuliko simba mna tofauti gani na simba kujisifia kucheza robo fainali klabu bingwa mara nyingi kuliko yanga ikiwa hoja ni wote kucheza hatua hiyo bila kujali ni mara ngapi, tajeni mafanikio ambayo yanga anayo simba hana halafu mnapenda kujisahaulisha si juzi tu mlikuwa mnawaringishia simba medali za cafcc na kuwaita wao kina mwakarobo halafu leo hii mnasema mafanikio ni makombe tu sasa ninyi wakati mnajivunia medali hamkujua kwamba mafanikio ni makombe tu
 
Kubishana na hao watu ni kujivunjia heshima
 
Ukitumia rank kama kigezo cha ubora moja kwa moja itamuondoa Pyramids ambaye ndio bingwa wa CAFCL msimu ulioisha. Je wewe unaona Pyramids sio timu bora?
Ni timu bora kwa sababu wako nafasi ya sita na ubora wa timu ni pamoja na consistency siyo ubora wa msimu mmoja tu, by the way hivi unajua kuna vilabu vingi ulaya vimewahi kubeba ucl kabla ya arsenal ila ukivilinganisha arsenal bado ni wakubwa, halafu hapa tunalinganisha ubora kati ya simba na yanga ambao wote hilo kombe la cafcl hawana sasa yanga ana mafanikio gani ambayo simba hana
 
Kwamba Simba ni bora kuliko Pyramids? Aisee kweli wewe ni shabiki wa Simba asilia kabisa.
 
Kwavile furaha mtu apangiwi ni halali kufurahia chochote kile as long as kinakupa faraja ya moyo hata kama ni cha kijinga.
 
Kwavile furaha mtu apangiwi ni halali kufurahia chochote kile as long as kinakupa faraja ya moyo hata kama ni cha kijinga.
Hakuna ujinga katika furaha unless chanzo cha hiyo furaha ni tatizo kwa wengine.

Changamoto ya uwekezaji wa furaha kwenye huzuni za wengine ni tatizo si kwenye michezo tu, hata kwenye jamii, kuna watu hata wawe na kingi kiasi gani hawapati furaha kama wanayopata wengine wakiwa na majonzi.

Mtu ana makombe yote ya ndani, ila akisikia shabiki anafurahia simba kuwa club namba 5 kwa ubora Africa msimu wake mzima unaharibika anaanza kuteseka kutafuta namna kuonyesha kuwa kuwa nafasi ya 5 ndani ya Africa si sababu inayotosha kufurahi. Hahaha.
 
Wakati mnaiita hizo medal ni mabati, cafcc mliita ni ligi ya wadada, ila sasa hivi na nyie mnafurahi hizo medali mlizosema za mabati
 
Mtu yupo nafasi ya 5 africa ila akisikia shabiki anafurahia Yanga kuwa na makombe mengi ya ligi, anaanza kuteseka kutafuta namna kuonyesha ubingwa wa ligi sio sababu inayotosha kufurahia
Hahaha.
 
Ungesoma tulipoanzia, alisema ubingwa wa Yamga hauna umuhimu wa thamanj. Ila nashukuru wewe umetambua huo uthamani. Basi na mimi natambua uthamani wa Simba.
 
Mtu yupo nafasi ya 5 africa ila akisikia shabiki anafurahia Yanga kuwa na makombe mengi ya ligi, anaanza kuteseka kutafuta namna kuonyesha ubingwa wa ligi sio sababu inayotosha kufurahia
Hahaha.
Hahaha, Mashabiki wa Yanga wana hii kasumba sababu wanafukia mashimo, wenyewe wanaita kufyeka kichaka. Sasa wakifyeka hichi wakiinua kichwa wanakutana na chaka jingine. Ndo maana pamoja na fanikio la kufyeka chaka furaha inakosekana. Unamaliza kufyeka chaka la ugiant, unakutana na chaka la kufika hatua ya robo fainali mara nyingi, wakati unapambana nalo unakaribia kulifyeka unakutana na chaka la rank. Unafanyaje zaidi ya kupata huzuni?

Sisi mashabiki wa Simba huwa tunatangulia, hata tukikosa tunajua hili tulishapata mpaka tumelizoea. Yapo mafanikio mengi tunayatamani, hatujayafikia, tunatakiwa tuyafikie ili Yanga nao waone kumbe inawezekana wayafikie halafu wakiyafikia watusumbue na kelele za ugiant.

Mfano unadhani ukimuuliza shabiki wa Simba kati ya kubeba Nbc msimu huu na kufika nusu fainali klab bingwa atachagua kubeba NBC?
 
Anauzwa kwa $1M, bei ikifikiwa atauzwa.
Umeambiwa na nani atauzwa kwa $2M? Kuna kiongozi wa Yanga amesema, au kuna official statement?
Au umeambiwa na mashabiki tu wa kunogesha kijiwe na wewe umelibeba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…