TEUZI: Rais Samia ateua Wakuu wa Wilaya. Nassari, Dkt. Mashinji, Lijualikali, Msando, Nikki wa Pili ndani

TEUZI: Rais Samia ateua Wakuu wa Wilaya. Nassari, Dkt. Mashinji, Lijualikali, Msando, Nikki wa Pili ndani

Kwenye kudai katiba mpya binafsi namuamini zaidi yule askofu kuliko Chadema na genge lao la wahuni.
Wananchi kawaida tunataka katiba mpya iondoe huu upuuzi tena haraka lakini Chadema ni CCM-B so hawana jipya Zaid ya kuendekeza matumbo mpaka kusalitiana

Nakubaliana na sehemu ya andiko lako lakini hata CCM wanajua Chadema siyo CCM-B:

 
Mkuu hata Bashiru, Pole pole, Majaliwa na hata Mataga wakereketwa wanaihitaji katiba mpya. Anatakikana mratibu tu wa shughuli hii. Hayuko bora kuliko Chadema kwenye hili kwa sababu zilizoorodheshwa kwenye uzi huu hapa chini:


Au nasema uongo ndugu zangu?
Watu wengi wanahitaji Katiba bora lakini Chadema siyo chama chenye uwezo wa kuorganize watu wote towards a common goal.

Chadema ni chama ambacho siku zote huwa wanaona wao kama wao wanatosha kabisa, wao ndio wapenda haki, wazalendo wa kweli, wengine wote ni ovyo na wasaliti.

Ili Katiba mpya ipatikane bila machafuko inahitajika lobbying na ushawishi mpaka ndani ya CCM yenyewe.

Wakati kina Nyerere wanapambania Uhuru walijitahidi kuunganisha makundi yote ndani na nje ya nchi na ndio maana tulipata Uhuru bila kumwaga damu.

Lakini Chadema wao wao wakijifanya sisi ndio sisi tunapigania Katiba mpya, itaonekana ni suala lenye maslahi ya kisiasa kwa Chadema pekee na hakuna atakayejali.

Kumbuka nchi hii ina watu karibu 60M na walio wengi hawana vyama.
 
Watu wengi wanahitaji Katiba bora lakini Chadema siyo chama chenye uwezo wa kuorganize watu wote towards a common goal.

Chadema ni chama ambacho siku zote huwa wanaona wao kama wao wanatosha kabisa, wao ndio wapenda haki, wazalendo wa kweli, wengine wote ni ovyo na wasaliti...

Mkuu kwamba?

"Ili Katiba mpya ipatikane bila machafuko inahitajika lobbying na ushawishi mpaka ndani ya CCM yenyewe."

Si lazima kupatikana bila machafuko kama wenye nafasi za kuwezesha hilo wameshupaza shingo kwa muda wote huu. Wakijimilikisha nchi kama yao peke yao.

Panahitajika msukumo wa kutosha kuwafanya walioko madarakani kutambua pasipo na shaka yoyote kuwa sasa inatakikana katiba mpya!

Hapa ndipo mratibu mwenye nia, dhamira na organization iliyo bora zaidi anapohitajika. Kwenye hapa haipo haja ya kujidanganya, Chadema wako bora zaidi.

Ni wazi kuwa ngoma ikishanoga haitashangaza kumwona hata mama Samia, Shaka, na hata bwana Chongolo nao hadharani kuwa wanataka katiba mpya.

Huu ndiyo ulio ukweli mchungu.
 
Mkuu kwamba?

"Ili Katiba mpya ipatikane bila machafuko inahitajika lobbying na ushawishi mpaka ndani ya CCM yenyewe."...
Sawa tusubirie Chadema wapiganie Katiba mpya mpaka ipatikane.

Wengine tunasubiri kuwaona wakisusia chaguzi zote mpaka pale itakapopatikana tume huru kama walivyoahidi.
 
Kuna hoja ilioandikwa hapa,kulalamika na kuhoji iweje Mzanzibari kateuliwa kuwa mkuu wa wilaya,akataja Tanganyika.Pia akaendelea kudai Tamisemi haipo katika wizara za Muungano.

Nasema wazi hajakosea.Lakini kwa kuwa wengi wenu hawajamjibu,inaonekana mmekubaliana naye.,Sawa hakuna tatizo.Ila na sie Wazanzibari tunaye Rais wetu na makamu 2. Kazi ndogo tu,nasi tunao watanganyika kibao katika wizara ambazo sio za muungano.

Nyie mnaojidai watanganyika muondoeni nasi wazanzibari tutawaondoa.Pili ikiwa wizara ya mambo ya kigeni inaongozwa na mtanganyika,basi wizara ya mambo ya ndani iongozwe na mzanzibari au vice versa.

Lakini ninachojua mimi ni kuwa wote ni WATANZANIA.LABDA NI MMOJA WA WANACHAMA WA SUKUMA GANG.KWA TAARIFA YENU NYIE MNAOJIITA WATANGANYIKA,ZANZIBAR SIO MKOA NI NCHI UDUMU MUUNGANO WETU DAIMA NA MILELE INSHAALLAH.
 
Sawa tusubirie Chadema wapiganie Katiba mpya mpaka ipatikane.

Wengine tunasubiri kuwaona wakisusia chaguzi zote mpaka pale itakapopatikana tume huru kama walivyoahidi.

Kwa hakika hakuna haja ya kushiriki chaguzi viini macho hizi zisizokuwa na tume huru wala katiba mpya.

Huo nao ni ukweli mwingine mchungu.
 
Kwa hakika hakuna haja ya kushiriki chaguzi viuno macho hizi zisizokuwa na tume huru wala katiba mpya.

Huo nao ni ukweli mwingine mchungu.
Sawa tusubirie tuone namna CCM watakavyokubali kuunda Tume huru ya uchaguzi yenye uwezo wa kuwafurahisha Chadema.
 
Huu muungano ni tatizo. Watu wanaoonekana kubebwa zaidi, ndio wanaolalamika zaidi. Msipouvunja nyinyi wazee, tutauvunja sisi wanenu!
 
Huu muungano ni shida, faida za moja kwa moja kwa wananchi wa pande zote mbili hazipo.Ni muungano wa kinyonyaji tu.
 
Huu muungano ni tatizo. Watu wanaoonekana kubebwa zaidi, ndio wanaolalamika zaidi. Msipouvunja nyinyi wazee, tutauvunja sisi wanenu!

Zanzibar ni ujinga. Watu duni sana, maskini na wanajifanya kujua. Sioni faida yoyote ya muungano
 
Kuna hoja ilioandikwa hapa,kulalamika na kuhoji iweje Mzanzibari kateuliwa kuwa mkuu wa wilaya,akataja Tanganyika.Pia akaendelea kudai Tamisemi haipo katika wizara za Muungano...
Hii ni ndoa ya kulazimishwa
 
Mawaziri waliopo katika serikali ya Zanzibar na ambao unadai kuwa ni watanganyika ni wepi mbona hauwataji majina japo watatu au wawili tu. Kama mtanganyika kupata tu kiwanja Zanzibar ni vigumu inakuwa vipi iwe rahisi kuupata uwaziri? Mleta mada unatakiwa kutushukuru sisi watanganyika kwa kuwa na moyo wa utu, uvumilivu na upendo. Laiti ingekuwa ni swala la jino kwa jino yani kulipiza kila mnalotufanyia, naamini huu muungano ungekuwa ushasambaratika.
 
Kwa Zanzibar, mtanganyika kupata tu chumba/nyumba ya kupanga ni mtihani. Achilia kununua kipande cha ardhi ama kupata kazi ambavyo ni maufuku.

Huu muungano utazamwe upya.
 
Back
Top Bottom