Nsingia kwenye mada moja kwa moja na kwa ufupi bila kuwachosha ndugu zangu wanaJF.
Naungana na ndugu Charles Kitwanga kuhitimisha kwamba mama Samia ni rais mzuri mwenye uwezo wa kuivusha nchi salama lakini amezungukwa na GENGE la watu (possibly SUKUMA GANG) wanaomshauri vibaya. Tangu Rais Samia aanze uteuzi wa viongozi, kwa kuondoa timu aliyoirithi kutoka kwa hayati Magufuli, nimekuwa nikifuatilia teuzi zake nimegundua ziko biased kwa misingi ya udini na ujinsia.
Mara nyingi kila anapofanya teuzi mpya, kuwahamisha wizara au kuwafuta kazi baadhi ya viongozi, anarudia tatizo lile lile. Nadhani huu ni mwendelezo mbaya kutoka kwa genge la watu wanaomshauri. Mfano, mzuri ni huu uteuezi aliofanya jana. Yaani uteuzi wake umejaa udini na ujinsia kila kona. Ifike mahali Rais Samia aache kusikiliza ushauri wa hili genge ili asijiingize kwenye tatizo la kuigawa nchi kidini bila sababu za msingi. Nashauri anapofanya uteuzi ajaribu kubalance kwa sababu watanzania wote wanamtazama na bahati mbaya wengine hawajuia kama anashauriwa bibaya. Wanadhani anafanya makusudi.
Nawasilisha.