TFF imetoa taarifa ya mapato ya Mchezo wa watani wa Jadi Simba na Yanga ambao ulifanyika jumapili iliyopita tarehe 16/4/2023
Kujenga uwanja sio kuingia chooni nakutoka,team zenye zinawapigaji kibao
 
Sijui wanatumia akili gani.

Mfano Sasa timu inazunguka kutafuta washabiki wajae uwanjani. Timu inazunguka kuuza tiketi. Wanafanya promo Alafu wanaambulia fedha kiduchu.

Tff tu imechukua mamilioni kwa migongo mingi Sana.

Eti gharama za mechi m. 22. Kweli, gharama zipi hizo jamani huu Ni wizi mtupu. Je marefa waliongezeka? Au malipo yao Ni tofauti na mechi ya ihefu na polisi Tanzania.

Baadae Tff wakachukua m 18. Eti kuwapa fa. Kweli? Zanini Sana wakati gharama za mechi walishalipa tayari. Huu Ni wizi mtupu.

Hawakuridhika wakachukua Tena m 25. Eti bodi ya ligi. Kama gharama ya mchezo imelipwa, fa wakalipwa. Sasa na Hawa bodi hayo mamilioni ya Nini Sasa. Hii Ni malipo mengine kwa kitu kimoja.

Hawakuridhika wakachukua Tena Tff m 10 kweli acheni Basi.

Serikali ikachukua Kodi m 64 hawakuridhika wakachukua Tena gharama za uwanja m 47. Sasa kwanini gharama za uwanja zisiwe standadi. Kama Ni m 5 kwa kila mechi iwe ivyo. Haiwszekani malipo yaangalie kipato. Ivi zile sherehe za kitaifa, mabonanza na matumizi tofauti hulipia gharama hizo?


Serikali simamieni utumike utaratibu wa haki. Timu hizi hutumia gharama kubwa Sana kwa usajili, mishahara kambi na mapato yao hayatoshi hata kujiendesha. Wafadhili wao wakichoka Sababu waoga hawawezi kusema soka linarudi lilipokuwa mnakatisha Sana tamaa.
Oneni aibu.
Simba na Yanga ni chambo kinachotumiwa na mafisadi ya CCM wakisaidiwa na wafanyabiashara wa kigabachori kuwapumbuza watanzania ili nchi iendelee kupigwa.
 
Dawa ni kujitoa tu kwenye ligi yao ili wasitunyonye.
Maana hata tukijenga víwanja vyetu % ya mgao wa mapato ya kiwanja yatapunguzwa na kupelekwa kwengine.
 
Shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini limetoa taarifa ya mapato ya Mchezo wa watani wa Jadi Simba na Yanga ambao ulifanyika jumapili iliyopita tarehe 16/4/2023, wadau mbalimbali wametoa maoni yao kufuatia timu mwenyeji (Simba)kuambulia sh 188,987,181.10 tu katika mapato yote yaliyopatikana, kuna haja ya timu hizi kuwa na Viwanja vyao kukwepa Unyonyaji huu.

img-20230420-wa0026-jpg.2593943

Inashangaza kuona timu zimeanzishwa kabla wengi wetu hatujazaliwa eti bado hazina hata viwanja vya mazoezi.

Wacha ziendelee kuvuja jasho huku likitiririkia TFF , maana zinazidiwa hata na timu za shule za msingi zina viwanja japo kulingana na mazingira yao
 
Hivi mnazani GSM na Mo kupotezea suala la ujenzi wa uwanja ni wajinga sanaeee. Hakuna mfanyabiashara mwenye akili ya kibiashara atapoteza muda wa kujenga viwanja kwa hizi timu
 
Hata mjenge viwanja vyenu mtakwepa gharama za uwanja tu, hvyo vingine viko palepale
 
Ipo siku itajua kwmba bossi wako anachangia kukukwamisha ili uwendelee kumtumikia, unaweza akapnga mipango yako safiii ,akatokea mtu akawashauli wengine wakaaribu mipango yooote, waza cmba na yanga wakawa na viwanja selikali itapata nn kupitia hizo timu?
Na hii ndo sababu hutakuja sikia yanga/simba wanakiwanja.
 
Viongozi wa serikali hawawezi kuruhusu Simba na Yanga wajenge viwanja vyao kwa miaka hii ambayo bado Watanzania ni wajinga kwa sababu watakosa pesa za hapa na pale
 
Back
Top Bottom